Jee tutafika?

mweongo

Member
Aug 23, 2010
62
228
Nimefika mahali pa kusema kweli watanzania hatuna uchungu na taifa hili. Hali inasikitisha kwenye nyanja zote za maisha. Elimu Afya, Miundombinu, Mipango miji, Maji Viwanda. nk...

Elimu: Hakuna taifa lolote lililoendelea duniani bila kuwekeza kwenye elimu. Viongozi wetu na hata sisi wananchi wenyewe tunalijua tatizo hili lakini hakuna anaechukua hatua yoyote. Kila wakati mara kubadili mitaala, au tutumie kiswahili nk. Elimu yetu inazalisha watu wajinga kwa kiasi kikubwa. Kijana wa form 4 hawezi kuandika hata barua ya kiswahili ya kuomba ajira. Graduate hawezi kujieza kwenye usaili. Hivi na elimu hii tunaelekea wapi? Siku hizi watu wote wenye uwezo kidogo wanapeleka watoto wao kwenye shule binafsi ambazo angalau zinanafuu kidogo
ukilinganisha na zile za kayumba na zinafundisha kwa kingereza. Watoto hao ndio watakao chukua nafasi zote nzuri za ajira hapo baadae mtoto wa masikini ataishia kuwa mwalimu nesi polisi mwnajeshi machinga nk.. Kwanini kuwe na matabaka katika utoji elimu? Hivi viongozi wetu hawaoni hatari inayotukabile ya kuwa na taifa ambalo 80% ya wahitimu hawajui lolote?!

Afya: Kweli mpaka leo wakina mama wakijifungua wanalala wawili kitandani au sakafuni? Tujiulize shangingi linaweza kununua vitanda vingapi? kwanini hatuhashimu afya za watoto wetu na mama zetu. kwanini hali hii wakati uwezo upo wako wapi viongozi wa kuonyesha njia au kwa vile wao wanatibiwa India.


Miondo Mbinu: Nchi hii ni kubwa sana, reli ndio usafiri wa uhakika na rahisi kote duniani.hata hizi ajali za mabasi za kila siku zisingekuwepo maana watu wangetumia treni. leo hii reli ya mjerumani na mchina zimetundisha. hivi kweli tunashindwa kujenga mtandao mpya wa reli unounganisha nchi nzima na kupata bishara ya usafirishaji toka kwa nchi jirani? kwenye kampeni tulisikia reli mpya itajengwa hadi kigoma na mwanza. lakini nadhani hakuna hata faili lilofunguliwa kwa jambo hilo. Tuliahidiwa fly over dsm. Wenzetu Nairobi wameshajenga sisi ni porojo tu. hela ya misaada na mikopo inalipa mishahara na posho. mabilioni ya epa, radar, majengo ya benki kuu, downs ndege ya raisi nk.. yangejenga kilomita ngapi za reli? Tunazoziita high way zimejaa matuta wanachi wanaandamana kila siku kujegwe matuta barabani hivi njia nzima ikiwa matuta kuna faida gani ya kujenga barabara ya lami. Nchi za wenzetu high way hazina matuta na speed ya chini ni 80km ph. hapa kwtu 30km ph.

Mipango miji: kwenye miji yetu, sehemu walizojenga wazungu wakoloni ndio nzuri hadi leo! mfano DSM Oysterbay, upanga, Masaki nk.. sisi Mnzese sinza buguruni. miji yetu ni vurugu tupu. Hivi viongozi wetu na wataalamu wakienda nje hawoni miji ya wenzetu ilivyopangiliwa. Hata kuiga tu hatuwezi jamani tatizo letu ninini?

Mika 50 ya uhuru maji ya bomba shida umeme wa uhakika hakuna viwanda alivyo anzisha nyerere hakuna tuna reli hakuna, elimu ndio kabisa kwenda wapi?

Hakuna nchi isiyokuwa na mafisadi duniani. lakini kunakua na mipango mzuri ya kuendeleza taifa katika elimu afya viwanda mindo mbinu nk.. lakini hapa bongo hakuna lolote ni ubafsi tu uliotawala. katiba mpya itusaidie kuweka mikakati ya kuedeleza taifa hili. hali ni mbaya sana.




 
andiko zuri.... ; on the other hand, kueleza matatizo ni rahisi zaidi kuliko kuyatatua...ingesaidia sana kama ungependekeza mikakati angalau michache ya ku-address hii appalling situation to start with..
 
Back
Top Bottom