Jee kesho 9 December Wamrima munasherehekea uhuru gani? Cunfuse.com | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jee kesho 9 December Wamrima munasherehekea uhuru gani? Cunfuse.com

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Dec 8, 2011.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1]Nchi ya Tanzania Bara ndani ya Tanzania ?[/h]Written by Mrfroasty (Ufundi) // 04/12/2011 // Makala/Tahariri // 2 Comments

  Kwanza tuanze na mwenge wa uhuru.
  Huu mwenge ni wa uhuru gani? Tanzania ina mataifa mawili tu katika katiba ya nchi,yaani Zanzibar na Tanzania ambayo ni muungano.Je mwenge wa uhuru ni mwenge unaohusu uhuru wa Zanzibar? au unahusu uhuru wa muungano?
  muungano hauna uhuru,
  Kwahio mwenge wa uhuru si wa Zanzibar wala muungano ambazo serikali mbili ndizo zilizomo katika katiba ya Tanzania, kwahivyo mwenge na sherehe za uhuru wa Tanganyika hauhusiani kabisa na shughuli za muungano wa Tanzania kwani hio nchi haipo wala haitambuliwi tena,
  hawa jamaa wamekuwa wakiutembeza na kuishangilia siku ya uhuru wa Tanganyika kwa fedha za muungano tokea mwaka 1964,ambapo fedha hizo si halali kuziendeshea shughuli za Tanganyika isiyokuwepo ndani ya Tanzania aidha Zanzibar inabidi ilipwe zaidi ya dola billioni moja kwa makosa yote ya uhalifu na utumiaji fedha za muungano kwa shughuli za Tanganyika au Tanzania Bara ambazo hazipo katika katika ya nchi.
  Sherehe za uhuru:
  Kuna habari imetoka gazeti la habari leo ambazo rais wa marekani ametuma salamu za hongera kwa rais kikwete kwa kutimiza miaka 50 ya uhuru wa Tanzania, (miaka 50 ya uhuru wa Tanzania?) uhuru wa Tanganyika 1961-2011 ni mika 50 na uhuru wa Zanzibar hapo ilikuwa ni mika 3 baadae yaani jan 12-1964. hapo inakuwa uhuru wa Zanzibar una miaka 47 sasa, na huo uhuru wa Tanzania wa kutimiza miaka 50 ulikujaje hapo wakati bado Zanzibar ilikuwa inatawaliwa na sultani?
  Kwahio hawa jamaa wanautangazia uhuru wa Tanganyika au wanaitangazia Tanganyika au shughuli za Tanganyika kimataifa kama ni Tanzania hali ya kuwa ni Tanganyika ndani ya Tanzania na kuiba mamilioni ya fedha za Zanzibar hivihivi yaani.
  Obama si mchawi kuwa anaweza kuamka tu agaagulia kuwa Tanzania inafanya uhuru wake miaka 50 dec 6,kwanza Tanzania sio nchi ya kufanya sherehe za uhuru kwani Tanzania haina uhuru bali sherehe za muungano badala ya sherehe za uhuru,hivyo viongozi wa Tanganyika ndio wanaopeleka habari nchi zote duniani kuwa Tanzania inafanya uhuru wake miaka 50 hali ya kuwa ni Tanganyika. hilo ni kosa kubwa sana kuishirikisha serikali ya Tanganyika katika shughuli za muungano wa Tanzania.
  Hii hapa tena uhai tosha kua katika michuano ya kombe la CECAFA linaloendelea hivi sasa hapo dar,viongozi wa tff wa bara wanapeleka matokeo ya mechi zote za timu ya taifa ya Tanzania Bara kama wanavyoiita kilimanjaro stars kuwa ni kama matokeo ya timu ya taifa ya Tanzania,ambapo katika world ranking yataingizwa na matokeo yanakuwa ni timu ya taifa ya Tanzania ndio wanaocheza michuano hio na sio Tanzania Bara,hapo chini nimekutumia website ya fifa uiangalie ili uipeleke kwa wahusika kwavile Zanzibar pia inacheza hio michuano lakini matokeo yake hayawekwi katika fifa bali matokeo ya Tanzania Bara ambayo sio timu ya taifa ya Tanzania yanawekwa kama timu ya taifa ya Tanzania.
  Je ni kigezo gani kinachopelekea wao waingizwe katika kuwa ni Tanzania hali ya kuwa ni bara? na hayo wamekuwa yakifanyika kila mwaka wakati timu ya taifa ya bara inapocheza katika mechi yoyote ile.mbali na kuwa timu hio ilikufa tokea muungano wa Tanzania ulipoanzishwa na wao hawakutakiwa kushiriki tena maisha yao,hio pia ni corruption kubwa sana ya katiba hivyo wanatakiwa wailipe zanziabr bilioni moja dola ambazo wamekuwa wakizitumia katika njia chafu tokea mwaka wa kwanza wa muungano.
  Wao tff walipeleka habari kuwa Zanzibar ilikufa utaifa wake tokea muungano wa mwaka 1964, je wao tnganyika wanaweka matokeo yao ya taifa la Tanzania Bara linalocheza CECAFA na mpinzani wake wa kundi jingine ni nchi ya Zanzibar iweje wao taifa lao la tnanzania bara halikufa katika muungano wa mwaka 1964 na wetu sisi uwe ulikufa? iweje wao wanashiriki mara mbili kama timu ya taifa ya Tanzania ya muungano na pia timu ya Tanzania Bara pia kama muungano?
  Utaifa gani wa Zanzibar wanaodai ulikufa mwaka 1964 baada ya muungano? Kama baada ya muungano tu Zanzibar walikuwa sio nchi tena mbona ni miaka ya hivi karibuni wabara bado walikuwa wanaingia Zanzibar na pasport za mchele.je kama Zanzibar ilikuwa sio nchi tena mwaka huo 1964 ilikuwaje waingie ndani ya nchi ya Zanzibar na pasport?lakini hata mwishowake walipoamua kuondoa pasport kwenda Zanzibar kwavile ni part ya muungano hakuna sheria njingine yoyote iliyotungwa inayosema kuanzia sasa kwenda Zanzibar itakuwa ni bila pasport na Zanzibar kuanzia sasa itakuwa sio nchi tena,hakuna hakuna hata kipenegele kimoja kilichowekwa hapo kuwa Zanzibar ilikufa utaifa wake baada ya kuondoa pasport iweje utaifa ulikuwa umekufa mwaka 1964 baada ya muungano?
  Katika maoni ya katiba hivyo vyama vya akina chadema na vinginevyo wanadhani hio katiba inaweza kuibada Zanzibar kudai chake. hivyo vyama ni vyama vilivyozaliwa katika muungano tu,havihusiani katika masuala ya kuibana au kuiathiri Zanzibar katika masuala yake kama nchi,
  ahsante.
  Michezo:
  Nilishtushwa na habari hizi ambazo nadhani wazanzibar walikuwa muda wote hawajaamka nazo.Kwakifupi kila mwaka hufanyika mashindano ya mpira wa miguu kwa timu za taifa za nchi za Africa mashariki na kati (aidha huwepo pia baadhi ya timu waalikwa kutoka nchi moja au mbili za upande mwingine wa Africa).
  Lakini muhimu timu za taifa za nchi mshiriki “kwa mujibu wa sheria ya CECAFA chama cha soka cha Africa Mashariki na kati ni kuwa nchi hizo ziwe huru ambazo hazitawaliwi tena na ziwe na nyimbo na bendera y waandaaji wa mashindano hayo ya mwaka jana na mwaka huu ni Tanzania Bara(ambao hio nchi ya Tanzania kwa bahati mbaya hawana bendera ila wanaitumia bendera yetu ya muungano na pia hawana nyimbo ya taifa pia wanaitumia tena kwa kosa jingine nyimbo yetu ya taifa ya Tanzania).
  Hilo ni kosa kubwa sana muheshimiwa kufoji kitu kisichokuwepo katika sheria ya nchi,kuiingiza nchi ndani ya nchi pasipo kushirikishwa Zanzibar hilo ni kosa kubwa sana.Kila mwaka nchi wanachama zinatakiwa kulipia uwanachama wao wa nchi za CECAFA “tena kwa mara nyingine Tanzania Bara inalipiwa pesa hizo kutoka pesa za muungano bila Zanzibar kushirikishwa,aidha kunakuwa na kiasi fulani cha fedha ambacho nchi wanachama hupatiwa na CECAFA hapo kwa mara nyingine tena Tanzania Bara inapokea rushwa ikiwa kama ni nchi wakati nchi hio ni kivuli ndani ya Tanzania.
  Mara nyingi kumekuwa na kawaida wahamiaji haramu kutoka ethiopia na somalia huwa wanakamatwa kutoka misituni walikojificha na kufikishwa mahakamani pamoja na watanzania ambao huwa wanawaingizwa nchini kwa njia za panya pia hufikishwa mahakani,
  Ndugu muheshimiwa “nchi ya Tanzania Bara imeandaa mashindano ya CECAFA kwa mwaka wa pili mfululizo wanawaalika watu”nchi nyingine”kuja kucheza mipira”yaani kufanya kazi ya kulipwa pesa nyingi” kinyume na sheria za nchi) kama waandaaji wa mashindano hayo ni Tanzania Bara basi nchi hio haitambulikani kwa mujibu wa sheria ya Tanzania kwahivyo kuwaalika watu kuja nchini,tena kufanya kazi bila ya kibali cha muungano basi hilo ni kosa kubwa sana,huwezi kumualika mtu kama sio raia wa nchi,raia gani wa nchi ya Tanzania Bara waliowaalika hao watu kuja kucheza mipira?
  Hawa watu wa bara wana nchi yao ya Tanzania Bara ndani ya Tanzania kwa muda wa miaka mingi sana,wamekuwa na timu nyingi za taifa za vijana wa marika mwalimbali wa Tanzania Bara ambao huwa wanakaa hoteli kwa muda kila mara,kusafiri,kupewa posho,kuzilipia timu zinazokuja kucheza nazo na viongozi pamoja na marefaree ,ambapo tokea Tanganyika ilipokuwa na kuunda Tanzania nchi ya Tanzania Bara imekuwa ikiingia katika mashindano hayo kwajina la Tanzania(taifa stars) mpaka miaka michache tu iliyopita waZanzibari walipopiga marufuku jina hilo lisitumiwe kwavile linawashirikisha wachezaji kutoka bara peke yao,kutokana na hali hio walibadilisha jina kutoka taifa stars na kuita timu ya soka ya Tanzania Bara “kilimanjaro stars”.
  Kutokana na wizi “corruption walizozitumia hawa jamaa wa bara kwa miaka mingi, serikali ya Zanzibar inabidi iwapige faini ya zaidi ya dola billioni moja za kimarekani kwa makosa yote hayo waliyokuwa wakiyafanya kwa miaka yote na wanaendelea kuyafanya hadi sasa,aidha muungano utakuwa hapo ndio umekwisha kutokana na wenzetu kufanya makosa za jinai kwa muda wa miaka mingi sana na kuiibia au kutumia mali za muungano ikiwemo zanzibar kwa muda mrefu sasa.
  Ikiwezekana ndugu waheshimiwa wabunge wetu waliopo bungeni waje kwa haraka hapo nyumbani wakutua na wenzao wawakilishi ili suala hili hawa jamaa wasitufanya mabaradhuli kila siku.
  Miungano hio yao sheria za mbio za mwenge tayari zimepitwa na wakati,miungano mingi ya kijanja janja imevunjika hao waaanzilishi wao russia ,yugoslavia,bosnia na sehemu nyingi imekwisha pitwa na wakati,hawa wenzetu wa bara wanadhani kuwa muungano kuwa labda kuna kipengele cha sheria kinachosema muungano ni lazima?
  Hakuna kifungu chochote cha sheria za muungano kuwa ni lazima/kwanguvu na lazima iwe maisha huo muungano,wenzetu hawajui kuwa Zanzibar ni nchi kamili na inaheshimu tu muungano lakini inao uwezo wa kuamka siku moja na kutangaza rasmi kuwa Zanzibar imejitoa katika muungano wa Tanzania na kuwa ni nchi huru inayojitegemea na kuanzisha embassy zake nje na kuwaita wawekezaji kuja hapo nyumbani.
  Pia kila mwezi wa Dec 09 wanasherehekea uhuru wa Tanganyika nchi ambayo haipo tena,na isitoshe wanatumia wimbo wa taifa na bendera ya taifa na kugharimu mamilioni ya fedha za muungano kwa sherehe hizo ambazo hio nchi wala haipo,kwahio wenetu bado wana nchi ya Tanganyika lakini pia hio Tanganyika inabadilika katika mpira wanaiita Tanzania Bara ,au kuna Tanzania Bara na Tanganyika pia ndani ya Tanzania? je pesa za kugharamia shughuli za kusherehekea uhuru wa Tanganyika kwa miaka yote hio sio hizi pesa zetu za muungano?
  Tanganyika inapesa zozote zile ilizoziwacha kufanyia na kugharamia shughuli hilo ghali mno kila mwaka?au kunawafadhili wanao zifadhili sherehe hizo za Tanganyika?kutokana na hali kama hizi muungano tayari muda mrefu umekwisha hapa inabidi wazanzibar wakate huu mzizi wa fitna,hata wananchi wa Zanzibar wanaoishi bara hawachukuliwi na wenzao kama watanzania hadi leo wanawaita wapemba na kuwanyanyasa tu.
  Kama ikiwezekana mwaka huu kwa mara ya kwanza Zanzibar zasimshirikishe mtu yoyote katika katika sherehe hizi,kwani kunaunguza mamilioni ya fedha ya nchi yetu kwa upande wa muungano,hizi sherehe za mwaka huu zitakuwa kubwa sana kwahio kutakuwa na majeshi na magari yao,watu kutoka mikoa yote ya nchi ambao watakuwa wakilala mahoteli ya kifahari na kula chakula kizuri kwa fedha zetu za muungano kwaajili ya nchi ambayo haipo.
  Isitoshe kwa upande wao nchi yao ya Tanzania Bara haipo nchini lakini inashirikiki mashindano ya mpira kwa timu za taifa,pia vilabu vyao kila mwaka vinashiriki mashindano ya vilabu vya soka kwa nchi za Africa mashariki na kati ambapo kwahivi sasa yanga ya Tanzania Bara ndio mabingwa wao.
  Lakini kama wao wanaitambua Tanzania Bara na kuingiza mashindanoni suala kwanini wao wanashindidwa kufanya hisani kwa wenzao wazanzibar timu yao ya taifa ikashiriki katika mashindano ya Africa na pia kuwania kushiriki kombe la dunia?kama nchi ya Tanzania Bara ipo ndani ya Tanzania,basi Kikwete ni lazima aandike barua kwa fifa kuwa nchi ya Zanzibar ipo na inajitegemea kama nchi kamili ili ishiriki mashindano kivyake vyake.
  Vinginevyo Kikwete inabidi asimamishe mashindano ya mpira yanayoendelea hivi sasa dar ambao Tanzania Bara ndio waandaaji kwa fedha za muungano,na pia uhuru wa Tanganyika usifanyike pia mwaka huu kwavile nchi hio haipo ambapo pia ni fedha za muungano ndio zinazouungua hapo na kuwaua wanzaniabar njaa.
   
 2. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Kwanza hakuna BARA linaloitwa Tanzania katika mabara yote 9 ninayoyafahamu mimi.

  Maumivu ya kichwa huanza poolepole.
   
Loading...