Je Yanga ndio wamiliki wa uwanja wa Jangwani?

kilimbamula

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
1,792
851
Habari wanajf, nimekuwa nikifuatilia sakata la kushindwa kwa Yanga kuendeleza uwanja unaodaiwa kuwa wao maeneo ya Jangwani unaopakana na jengo lao.

Katika siku za hivi karibuni, mwenyekiti wa Yanga aliahidi kujenga uwanja huo utakaochukua watu 40 elfu.

Tukaonyeshwa na ramani na wajenzi kutoka china ambao inasadikiwa walikuwa tayari kuujenga.

Hata hivyo kuna habari zinadai kuwa timu hiyo imekatazwa kufanya hivyo kwa sababu kuu mbili
1. Hilo ni eneo la wazi na Yanga siyo wamiliki bali wamepakana nalo na wanalitumia kama watumiaji wengine wa eneo la Jangwani wanavyofanya hivi sasa.
2. Hata kama watataka kununua haitowezekana kwa sababu eneo hilo ni mapumulio ya bahari na kinyume na taratibu za mazingira kujenga maeneo hayo.

Kama ni kweli, kwanini Yanga inawadanganya wapenzi wake miaka yote kuwa wanamiliki uwanja na kutumika kama chambo ya kuwazuga wapenzi na wanachama kuwachagua viongozi?

Wajuvi wa suala hili tafadhali jitokezeni kuweka sawa jambo hili ili liwe wazi kwa wanachama wote.

Watani zao sasa wanamiliki kihalali eneo kubwa huko Bunju, wanamipango bora ya baadae kujenga kiwanja kikubwa cha kisasa. Je Yanga wao watakuwa wanatumia open space hadi lini?

Karibuni wataalamu kwa mjadala.
 
Wamegoma kuja? Hapa hawaji ila ukiandika Yanga kuendelea kupanda ndege watakuja weng kusema teaah sisi ni wa kimataifa.
 
Uwanja wa Kaunda ni wa Yanga,ili waujenge vizuri ni kwamba lile eneo halitoshi so inabidi waongeze eneo kwa kununua maeneo jirani ili wapate eneo la kutosha
 
Back
Top Bottom