Je wewe upo kundi gani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je wewe upo kundi gani

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ngongo, May 17, 2011.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Wataalamu wengi wa uchumi wanakubaliana kwamba ili nchi ijikwamue/isonge mbele kiuchumi tabaka la kati "middle Class" ni muhimu likawa kubwa.Nimejaribu kujiuliza tabaka la kati linashirikisha watu wa aina gani ?.Je tabaka la kati Tanzania [Middle Class] tangu enzi za Mwl J Nyerere hadi sasa limeongezeka au limepungua ?.

  Kwa mujibu wa tafsiri ya WB/IMF tabaka la kati [middle class] ni watu wenye kipato kuanzia u$ 2 mpaka u$ 20[3,000 - 30,000] kwa siku.Tukitumia tafsiri ya WB utakuta wafanyakazi wote wa serekali wenye kupata mshahara kima cha chini wanaangukia kwenye hili kundi[Middle Class].Wafanyabiashara ndogo ndogo eg Mama lishe,wauza mitumba,mboga mboga,matunda na nk wote wanaangukia kwenye kundi la tabaka la kati.

  Je pato la tsh 3,000/= kwa siku linakidhi mahitaji muhimu eg milo mitatu kwa siku,usafiri,huduma za afya na elimu kwa watoto ?.Ukijaribu kukokotoa utakuta pato la tsh 3,000/= kwa siku halitoshelezi milo mitatu kwa mtu mmoja na kama mtu huyo atakuwa na watu tegemezi eg mke na watoto hakika hata mlo mmoja utakuwa ni mgogoro mkubwa.

  Wataalamu wa uchumi wanapaswa kuangalia upya viwango vya kupima umaskini.Pato la u$ 2 kwa siku ni kiwango kidogo sana ukweli ukiangalia kwa namna yoyote mtu mwenye kipato hiki bado ni masikini sana hana uwezo wa kukidhi mahitaji yake muhimu ya kila siku.Yafaa kiwango cha middle class kipandishwe hadi u$ 10 [tsh 15,000]kwa siku pia suala la utegemezi eg ukubwa wa familia,usafiri na inflation likizingatiwa.
   
 2. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni kweli hili linapaswa kuangaliwa upya, ukizingatia gharama zimepanda maradufu.

  na je ni kweli kuwa, kufanya Uchumi uwe na Uwiano.....Yapasa Iwe ngumu zaidi kutoka Middle Class kwenda Upper Class....Ili watu wengi zaidi wawe Middle and lower kiasi????
   
 3. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 802
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Hivi viwango viliwekwa lini? Labda vime expire!!
   
 4. 1

  123 Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hapa nawaunga mkono wadau,kwa maisha ya sasa at least kwakiwango cha chini kiwe $5(7,500)kwa mtu mmoja ila kwa family angalau $10 (15,000)hiki angalau unaweza kusema chochote.labda mimi nafakiria kuwa hizi reaserch zao huwa wanafanya kijiji where by hakuna milo mitatu kwa siku na mambo ya usafiri hakuna.
  Naunga mkono hoja.
   
Loading...