Je, wewe umewahi bahatika kukutana na kiongozi yeyote wa Taifa hili na umepata kuongea naye kuhusu nini na mtazamo wake uliuonaje?

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Ni wanasiasa gani umewai kutana nao Live na Mliongea nini Mkashauriana nini.

Mwaka 2003 nilikutana na Mzee Hassan Mwinyi kabla sijaanza kufanya kazi na serikali kwa Ukaribu, tuliongea Mengi na nikamkumbusha mambo Mengi ya Nyuma ya History yake binafsi ambayo Wengi hawajui kwakuwa niliipata kutoka kwa Mlinzi wake wa Karibu, alifurahi sana.

Mwaka 2005 kabla ya kupita kugombea Jakaya Kikwete tulikuwa tunakutana naye kwenye Kamati fulani ambayo alizoea kutuambia perform better than yesterday but less than tomorrow.

Mwaka 2011 Nimekutana na Mzee Mkapa Rwanda alikwenda kwenye Masuala ya ishu za kushauri huko Rwanda, Huyu mzee alikuwa na mawazo safi Sana na alikuwa na maono ya Mbele kuhusu AFRIKA na TANZANIA Ila nilichogundua aliogopa sana CCM kutoka madarakani.

Mwaka 2013 na 2014 nilipokuwa naenda TANZANIA Mzee hayati Magufuli tumekutana Sana na mawazo mengine Mengi ni chanya, Ila hayo machache ambayo ni hasi yalikuwa na Madhara makubwa mno.

Mzee Sarungi, ni rafiki yangu sana, ukimsikiliza Sarungi alafu ukamsikiliza Maria utashangaa ,wote ni wazalendo ila Approach ziko against each other.

Mzee Pinda Tokea akiwa ofisi ya rais he was very Humble na mtu mnyenyekevu, anapenda utani Kama alivyokuwa Samweli Sitta ila...

Kiongozi ambaye sijabahatika kukutana naye ni Rais Samia Suluhu Hassan.


Lukuvi, Masilingi hawa wote nimekaa nao sana pale Bukoba Lukuvi akiwa Mkuu wa Wilaya, akili anayo sana na Maono japo walisema shule kaunga unga.

Je, wewe umewai bahatika kukutana na kiongozi yeyote wa Taifa Hili na wapi na umepata kuongea naye kuhusu nini na mtizamo wake uliuonaje?
 
Mimi nimekutana na Sumaye analalamika Pembeni Ila kwenye vikao VYA CCM anakaa kimya.

Pia yule alokufa kwenye helcopter Deo Filikunjombe.

January Makamba ni moja ya hazina ya vijana wa kuja kuongoza Taifa hili hapo Mbele.

Nimefanya naye kwenye program ya Wakimbizi Kigoma, pia tumekutana USA akisoma kwakweli huyu kijana smart.
 
Nimekutana na Baba wa Taifa Nyerere nakumbuka nilijigonga ukutani maeneo ya Offisi fulan nikaona mtu yuko nyuma yangu wakati nayapoza machungu akanijulia hali akanisihi niende zahanati nisipuuzie.

Kilichonishangaza wakati huo nilidhani ana pesa kumbe maskini hana kitu alichukua kalamu toka kwenye shati akaandika kimemo fulani akaniagiza sehem nikapata huduma.

Huyo ndo nilikuwa impressed kukutana naye, Wengine tunakutana Ila Moments zao so rahisi kunigusa.
 
Back
Top Bottom