Je wewe uko katika kundi lipi kati ya haya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je wewe uko katika kundi lipi kati ya haya?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rubi, Feb 25, 2010.

 1. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wandugu tumejadili mengi sana kuhusu suala la ufisadi mpaka ikatokea baadhi ya watu kuitwa mafisadi nyangumi, papa, na vidagaa. Nia nzuri ya mijadala hii ya kifisadi ni kutaka kukomeshwa kwa vitendo vya rushwa, kupata viongozi bora na waadilifu, wasio wabinafsi na tamaa ya madaraka na wenye uzalendo na nchi yetu, kufanya kizazi kijacho kiwe ni taifa bora lenye elimu isiyo ya kughushi taifa lenye viongozi walio na uzalendo na nchi yao, elimu bora na mazingira salama ya kuishi. Kutokomeza umimi na tamaa ya kujilimbikizia mali isiyo halali.

  Je kwa karne hii tunayoenda nayo ni kweli kunawezekana kutokomeza ufisadi au ndio itakuwa kila siku ufisadi kama hadithi za pwagu na pwaguzi. kama jibu ni hapana sioni mantiki ya kuendelea kujadili mijadala ya kifisadi ambayo hatuwezi kubadilisha kile kinachoonekana kuwa ni ufisadi.

  Na kama jibu ni ndio tufanyaje? pengine itapidi kila mtu ajiulize kuwa anaitakia nini nchi yake? kama anitakia mema na mazuri kwa vizazi vya sasa na vijavyo afanyaje? pengine inawezekana na wewe ni mmoja wapo wa anayepinga na kupambana na ufisadi je ni ufisadi upi unaupinga?

  Je kwa upande wako wewe sio fisadi?

  Inawezekana na wewe ni fisadi lakini hujijui kuwa na wewe ni fisadi lakini uko mstari wa mbele kupinga ufisadi? Hivyo toa boriti kwenye jicho lako ili uone kibanzi kwenye jicho la mwenzio.

  kama ni mmoja katika ufisadi jaribu kujirekebisha bado hujachelewa.

  FISADI WA ELIMU
  pengine ni mmoja wa unayechangia katika kulikisha mitihani ili watoto wako na wengineo wanaokupatia fedha waweze kufaulu bila kujisomea.

  pengine wewe ni fataki unayechangia kuharibu watoto wa shule na wa mwezio kwa kuwadanganya kwa lifti na vijisenti na hatimaye kuwaharibia future yao wakati huohuo hujui kuwa na wa kwako nao wataharibiwa na mafataki wengine.

  pengine wewe ni mmoja wao unayechangia kupatikana kwa vyeti bandia hivyo kuzidi kudumaza elimu bora inayohitajika kwa maendeleo ya taifa letu. hivyo kupelekea kuwa na madaktari feki, wahandisi feki, wanasheria feki wasiojua kulinda hata mkataba ya masilahi ya nchi yetu, walimu vihiyo, n.k wa kadhaa.

  au ni mmoja wao unayewanyima watoto wako haki yao ya msingi ya kusoma hata kama una uwezo wa kuwasomesha

  FISADI WA AMANI
  pengine wewe ni mmoja wao unayepandikiza chuki za kidini au kikabila katika jamii hivyo kupelekea uhasama wa kidini au kukashifiana katika dini hivyo kutokea kwa uvunjifu wa amani, au kupandikiza chuki za kikabila hivyo kupelekea baadhi ya koo kuanza kupigana na kuuana kitu ambacho hakikuwa cha kawaida katika nchi yetu.

  Au ni mmoja wapo unayetumia dini kuwahadaa wengine lakini moyoni mwako ni mbwa mwitu unayesubiri kurarua na kumeza

  au ni mmoja wao unayetumia njia zisizo halali kujipatia mali au kwa wizi wa aina zote, udhulumaji, uongo, uhujumu uchumi wa nchi n.k kuvyo kupelekea jamii kukosa imani wanapotembea au kulala majumbani mwao kwa hofu ya kuvamiwa na majambazi, au kukosekana kwa amani makazini kati ya mabosi na wafanyakazi wao wa chini kwa kuwadhulumu haki zao, au kupelekea uchumi wa taifa kuyumba au mashirika ya umma kufa kwa ajili ya kuhujumiwa na mikataba mibovu isiyo na tija kwa taifa letu.

  FISADI WA MAPENZI

  pengine wewe ni mmoja wapo usiyemwaminifu katika ndoa yako hivyo kupelekea ndoa yako kuwa na migogoro isiyokwisha au ni mmoja wapo uliyechanzo cha ndoa ya mwingine kuvunjika.

  au wewe ni yule uliyeingia katika mahusiano kwa sababu maalumu au kwa kufata mali alizo nazo mpenzi wako bila kuwa na mapenzi ya kweli?

  au wewe ni yule unayependa kujirusha na vya uswazi au wa geti kali bila kuwa na msimamo then ukiambiwa matunda ya kujirusha unachomoa na kuhama mji au ni mmoja wa wabakaji mambo ambayo pengine hupelekea kuwa na watoto wa mitaani wengi sana au kutolewa mimba/viumbe visivyo na hatia.

  FISADI WA UTU.
  utu ni hali ya kibinadamu ya kumjali, kumpenda, kumthamini mwenzio kama nafsi yako yaani unavyojipenda mwenyewe. Pengine wewe ni mmoja kati ya wale wanaoingiza madawa ya kulevya na kuharibu vijana na watoto wa wenzio bila kujua kuwa tunaharibu taifa la kesho.

  pengine wewe ni mmoja wao unayefanya au kushirikia kwa njia moja au nyingine katika vitendo vya kinyama i.e ngono kwa watoto wadogo, ndugu zako wa damu, ngono kwa wanyama, mauaji ya albino, na mengineyo yafananayo na hayo kwa imani za kishirikina ili kujipatia mali au manufaa yako binafsi.

  Au ni mmoja wao unayependa vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike ili hali ukijua madhara ya unachowafanyajia.

  Naamini ufisadi ni mwingi kwa upande mwingine lakini je wewe uko kwenye kundi lipi? je nini ufanye kwa upande wako ili pale unapopiga vita ufisadi ujue na wewe ni safi kwa manufaa ya nchi yetu, watoto wetu na vizazi vijavyo viishi katika Taifa lililo na uadilifu, lililo na na elimu bora, afya njema, usalama na uongozi bora
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  ahahahaha CKABLA ngoja niisome tena kwa makini ...
   
 3. Mgeninani

  Mgeninani Senior Member

  #3
  Feb 25, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Na wewe mkubwa tuambie kwanza upo kundi lipi?
   
 4. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  ahahahahaa ndio najichuguza ili nijue niko wapi nitoke ila nilikuwa kwenye kundi la mwoga ambao sijalitaja. sasa naona bora kuwa muwazi. ukiona kibaya kemea, ukiona kizuri sifia.
   
 5. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #5
  Feb 25, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mmh mimi sijui niko wapi.
   
 6. M

  Malila JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,478
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Mimi nadhani uko ktk kundi la waliokosa chance ya kufanyiza !!!!!!
   
 7. M

  Malila JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,478
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Mimi nadhani uko ktk kundi la waliokosa chance ya kufanyiza!!!!!!
   
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,794
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  Me too, that makr the two of us........nitarudi
   
 9. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,794
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  That make us think. Good one man!
   
 10. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #10
  Feb 25, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kabisa, tukijichunguza vizuri tutagundua kuwa sote tuna ka-element fulani ka ufisadi uwe ni wa mapenzi, amani, elimu, uchumi n.k tena kwa jinsi mambo yanavyokwenda hapa Bongo.,ile kuona watu wengine wanafaidi jasho la wengine kupita kiasi basi wengi wetu tuna li-element la ufisadi tena ule wa kiuchumi kama wa waheshimiwa sema tu hatujapata avenue ya kuuweka kwenye vitendo.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...