Je, watanzania tunataka demokrasia au maendeleo?

Hayo yote yalichangiwa na Gaddafi kung'ang'ania madaraka, matokeo yake yeye kayakosa maendeleo, kaikosa demokrasia na duniani hayupo tena!
Naona hujanielewa, nauliza watu wa nchi yake walimwondoa ili wapate Demokrasia, je wameshaipata au bado?
 
Libya naona wamerudi nyuma sana ukilinganisha na enzi za Gadafi. Maendeleo hawana wala hiyo Demokrasia waliotaka bado hawajaipata. Its "complete Total Loss in the business they transacted". Walidanganywa.
Libya hawakutaka demokrasia kupitia vita vya Marekani na ulaya walitaka demokrasia kwa njia ya Aman usitake kuleta mifano ambayo haiendani na mazingira ya Tanzania
 
Naona hujanielewa, nauliza watu wa nchi yake walimwondoa ili wapate Demokrasia, je wameshaipata au bado?

Mfano wa Libya haufanani na Tanzania kwanza Libya licha ya Gadafi kuwa na kaudikteta alifanya maendeleo ingawa wananchi hawakuwa na shukrani kwake wakaalika Marekani kuja kumwangamiza na Nchi kuangamia, Kwa Tanzania ni tofauti kabsa kwanza Nchi haina maendeleo pesa zote wanatafuna CCM wajanja wachache wanatumia pesa za walipa kodi kukandamiza demokrasia kuwalipa akina cyprian Musiba kutengeneza Sinema propaganda za kijinga jinga zisizo na Tija kwa Taifa, wanatumia pesa za umma kujenga Chato Airport kienyeji pasipo idhini ya Bunge , wametafuna Trilion 1.5 huku CAG akitishwa na kunyanyaswa wanakula 10% kwenye ununuzi wa ndege miladi yote mikubwa, ni vigumu kwa Tanzania kufanana na Libya kwani mengi yanayofanyika Tanganyika ni tofauti kubwa
 
Demokrasia huleta amani na ni sehemu ya maendeleo. hata katika familia watoto hawalishwi minofu na pilau pekee bali hupaswa kusikilizwa. Kusikilizwa ndio mfano wa demokrasia. binadamumu sio ng'ombe basi ukishawatengenezea banda zuri na kuwapa lishe umemaliza! demokrasia na maendeleo havitenganishwi! Msome Nyerere kuhusu hili.
 
Vipi kuhusu kurudi kwenye chama kimoja ili hii dhana ya kutokutaka demokrasia iwe na maana?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makaburu wa Afrika ya kusini walijenga miundombinu, walifunga watu jela, waliua watu, waliwanyima watu Uhuru, kama inavyofanya serikali ya Jiwe. Walipingwa na kisha kuondelewa madarakani kwa kunyima haki za watu. Hakuna mbadala wa UHURU.
Kwani Tanzania haina demokrasia?
 
This is Africa.

Hatuna haja ya maendeleo wala demokrasia wacha tulewe tuibiane tucheze ngoma tufe.

Maendeleo ili iweje?
 
vyote vina umubimu wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maendeleo yanaweza kuwa ya kisiasa, kiuchumi, kidemokrasia, kielimu, kisayansi, kiusalama n.k
Maendeleo sio wingi wa ndege pekee na flyover.
Aidha, tafsiri ya demokrasia isipotoshwe.
Kumnyooshea dole la kati kiongozi halafu ukishtakiwa useme nchi haina demokrasia huo ni upuuzi.
 
Asante mkuu kwa kuhoji ! Naomba kukujibu kwa contexty ya ndoa ambayo kwa kila mtu nndoa ni muhimu kuliko nchi(wanasiasa hukimbiza familia kabla ya vita),je uataka mchele na nyama kutoka kwa mpemba au kutosalitiwa hata kama maskini? kwa kuwa elimu kwa kulipia mchepuko wa mke bado ni muhimu kwa watoto ,Je inajustfy kuuchuna kwa hili ?
 
Shikamoo mkuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…