Naomba Hotuba ya Rais Samia isomwe Makanisani na misikitini kwa mwaka mzima

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,293
9,723
Ndugu zangu Watanzania,

Leo Rais Samia, mama wa shoka, jasiri muongoza njia, shujaa wa Afrika, chuma cha reli, nuru ya wanyonge, na sauti ya Afrika na wa Afrika, ameongea kwa uchungu na hisia kali sana mbele ya Watanzania na dunia nzima kwa ujumla. Mpaka kufikia hatua watu kuomba hotuba yake kusomwa makanisani na misikitini kwa mwaka mzima ili kuwafikia wengi zaidi na kukaa katika mioyo yao. Amegusa mioyo ya Watanzania, ameonyesha kwa ujasiri na uimara kuwa yeye ni zaidi ya Rais, ni zaidi ya mama, ni zaidi ya mlezi wa Taifa, na ni zaidi ya kiongozi. Leo Rais Samia ameonyesha ni mchanganyiko wa hayo yote, na vyote hivyo vipo ndani yake. Kwa hakika, ni kipawa cha kipekee na uwezo wa kipekee wa uongozi aliojaliwa na Mwenyezi Mungu. Ni uwezo na kipawa au karama ambayo huwezi ukaikuta kwa kila mtu. Ni mbegu ambayo haioti kwa kila mtu na kuchipuka kila mahali.

Kwa uchungu na hisia kali sana zilizojaa uzalendo na upendo kwa Taifa letu na Watanzania, amezungumzia juu ya kufanya siasa za hoja, kiungwana, kistaarabu, na zenye kuzingatia sheria, kanuni, taratibu, mila, desturi, na utamaduni wetu kwa ujumla. Ameonya na kutuasa kujiepusha na matumizi mabaya ya lugha, hasa lugha chafu za ubaguzi kwa misingi ya udini. Ametuasa Watanzania kutumia uhuru uliopo hapa nchini kwa shabaha ya kujenga na kuibua fikra chanya na mawazo mbadala katika kujenga na kuchochea maendeleo ya Taifa letu.

Ameonyesha kusikitishwa sana na watu ambao wamekuwa wakipanda majukwaani na kutumia uhuru huo vibaya kwa kuanza kufungua midomo yao na kutapika maneno ya kuudhi, kudhalilisha, kutukana, na kushusha heshima za watu wengine kwa chuki binafsi pasipo hoja za msingi. Ametuasa Watanzania kuweza kuvumiliana na kukosoana kwa lugha za heshima, staha, na adabu, na siyo kuongea utafikiri mtu aliyekosa malezi bora ya wazazi wake au ambaye hakupata kabisa malezi ya wazazi wake na kujikulia tu pasipo maadili bora wala muongozo wa aina yoyote ile.

Amezungumzia juu ya maadili na wajibu wa wazazi katika kuwalea watoto wao ili wasije kusombwa na matamaduni ya kigeni ambayo hayakubaliki kabisa katika jamii yetu na Taifa letu. Amesikitika sana juu ya mmomonyoko wa maadili kwa baadhi ya vijana kwa kuiga tu na kunakotoa picha mbaya na kuonyesha wazazi kujisahau katika wajibu wa malezi ya watoto wao. Kwa uchungu mkubwa sana kama mama mzazi, mlezi wa Taifa letu, ameonyesha kusikitishwa sana na ukosefu wa adabu kwa baadhi ya vijana ndani ya Taifa letu. Ameongea kwa maumivu makali sana Rais wetu mpendwa, kipenzi cha Watanzania, mpaka wasikilizaji wengine wakawa ni kama wanataka kutokwa machozi juu ya baadhi ya vijana kukosa adabu kabisa kana kwamba waliokotwa mahali walikokuwa wanaishi wenyewe tu bila muongozo wa aina yoyote ile wala malezi bora.

Hotuba hiyo iliyosambaa kwa haraka sana mitaani na mitandaoni kama maji ya mafuriko imepelekea Watanzania kupendekeza hotuba hiyo kusomwa makanisani na misikitini kwa muda wa mwaka mmoja ili kuendelea kuwafikia Watanzania wengi zaidi kwa kuwa ni hotuba yenye ujumbe mzito sana kwa Taifa letu na yenye uwezo wa kurekebisha baadhi ya vijana na kuwakumbusha wazazi juu ya wajibu wao wa malezi kwa watoto wao.

Rai yangu kwa Watanzania, hasa vijana, tujitahidi kuwa watulivu tuzungumzapo mbele ya hadhira, tutumie lugha za heshima, staha, na adabu ya hali ya juu sana. Tuzungumze kama watu tuliolelewa vyema na kufundwa vyema, tuache mihemuko, jazba, kukurupuka, na kuropoka tuwapo mbele ya watu au maiki. Tujifunze kuchuja kauli zetu na kuchunga ndimi zetu, tuwe wasikilizaji wazuri pale tusipoelewa na kuwa wenye busara pale tupewapo nafasi ya kuzungumza. Tumtangulize Mungu na kumuomba hekima zake kabla ya kuzungumza, tumuombe aongoze ndimi zetu kabla ya kufungua vinywa vyetu. Tuache na kujizuia kabisa mihemuko, utafikiri mtu aliyewehuka au kuzidiwa na mibangi kichwani.

Kwa wazazi, ni jukumu la kila mzazi kushiriki vyema katika malezi ya mtoto au watoto wake. Taifa bora na lenye maadili bora

linaanzia na kujengwa katika ngazi ya familia. Watoto walelewe katika maadili bora yenye hofu ya Mungu na kumpendeza Mungu, wawe ni wenye staha, busara, subira, vifua, hekima, na upendo kwa wengine. Wasiwe watu wa visasi au chuki pasipo sababu. Wafundishwe nidhamu ya hali ya juu na tabia njema watakayotembea nayo popote pale walipo na kuwa mfano wa kuigwa kwa watu wote na kupendwa na jamii nzima kwa tabia yao njema.

Wana jamii forums, tuanze kubadilika humuhumu kwa kuacha kutumia lugha ya matusi na udhalilishaji kwa watu wengine. Tubishane kwa hoja na kukosoana kwa hoja na tukubaliane kutokukubaliana, ambayo ni sehemu ya demokrasia inayokubalika. Hoja ipingwe kwa hoja na siyo matusi na kudhalilishana. Tuwe wa mfano na tutunze heshima ya jukwaa letu, na siyo kuligeuza kama jukwaa la wahuni na watoto watukutu na walioshindikana ndani ya jamii. Pasiwe kama mahali pa walevi walioshindikana au kuzibika au kuharibika akili.

Kazi iendelee, mama amefikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Mmeona Waraka unabamba sana. Si ndiyo nyie mliokua mnaimba nyimbo za kuchanganya dini na siasa? Au mmeshaona Waraka umeuza sana , hivyo na nyie mnatafuta soko na jukwaa hilohilo muweze kuuza?

Ama kweli wanasiasa hamuaminiki wala hamjui mtakalo wala mkataalo.

Hao wananchi umekutana nao lini na wapi?
 
Kwi Kwi Kwi , na bado ataanza kunena kwa lugha muda si mrefu
Rais Samia ni Chaguo la Mungu aliyeinuliwa na Mwenyezi Mungu kuwatumikia watanzania.Ni zaidi ya mama ,ni zaidi ya mlezi ni zaidi ya kiongozi kwa Taifa letu. Watanzania tunapata vyote kutoka kwa Mama yetu aliyejaliwa Karama na kipawa cha uongozi .
 
Mmeona Waraka unaidi sana. Si ndiyo nyie mliokua mnaimba nyimbo za kuchanganya dini na siasa? Au mmeshaona Waraka umeuza sana , hivyo na nyie mnatafuta soko na jukwaa hilohilo muweze kuuza...
Mimi nimewasilisha maoni na maombi ya watanzania ambao ndio wenye nchi yao. Wameguswa sana na hotuba ya Rais samia.
 
Ndugu Zangu Watanzania,

Leo Rais Samia mama wa shoka ,jasiri muongoza,Shujaa wa Afrika,Chuma cha Reli ,Nuru ya wanyonge Na Sauti ya Afrika na Wa Afrika Ameongea kwa uchungu na hisia kali Sana Mbele ya watanzania...
Wewe wa kike au wa kiume? Una mambo ya kigasho! Miongoni mwa watu wanatakiwa kupumzishwa ni pamoja na wewe! Wewe ni mzigo na ni hasara kubwa kwa taifa hili! Ufe tu!
 
Acha uvuvi mkuu mimi nipo humu mda mrefu nikipigania Taifa langu na kumuunga mkono mzalendo wa kweli na aliyelibeba Taifa letu katika mabega yake mh Dr Mama Samia Suluhu Hasssan.
.....
Mimi sina chuki na wewe mkuu...

Maana uandishi ni kipaji kikubwa sana ambacho nahisi mimi sina.
 
Rais Samia Ni Chaguo la Mungu aliyeinuliwa na Mwenyezi Mungu kuwatumikia watanzania.Ni zaidi ya mama ,ni zaidi ya mlezi,ni zaidi ya kiongozi kwa Taifa letu. Watanzania tunapata vyote kutoka kwa Mama yetu aliyejaliwa Karama na kipawa cha uongozi .
Umenukuu andiko lipi lililosema Rais auze Bandari ?

FB_IMG_1686074170313.jpg
 
Hao Watanzania wa Uarabun au Hapa hapa
Watanzania wazalendo na wanaojitambua na wenye uchungu na mapenzi mema na Taifa letu ndio wanahitaji jambo hilo ili kulisaidia Taifa letu hasa vijaja, ambao baadhi yao kama akina Mdude wanaonyesha kuzibuka akili na kukosa malezi bora ya wazazi wake na hivyo kupelekea kuwa kama kituko katika jamii.
 
Back
Top Bottom