Watanzania tusimdhalilishe Rais Samia

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Kwa mwezi mmoja sasa umekuwapo mjadala wa ubinafsishaji wa Bandari ya Dar es Salaam kwa kampuni ya DP World ya Dubai umevutia wachangiaji wengi kwa nia mbalimbali

Tukiusikiliza mjadala huu umebeba ujumbe ndani ya ujumbe. Hoja iliyopo mezani ni ya ubinafsishwaji wa Bandari ya Dar es Salaam kwa DP World. Tuliamini na tunatamani mjadala uendelee katika ujenzi wa hoja za ubora au upungufu wa mkataba unaojadiliwa.

Gazetiu Jamhuri limewapongeza TLS chini ya Rais wake Harold Sungiusia wamefanya uchambuzi wa kisheria wa mkataba kati ya Serikali ya Dubai na Tanzania na wakatoa msimamowa Kisheria na Mapendekezo yah atua za kuchukuliwa Serikali imesema imepokea hoja za TLS.

Mawakli Boniface Mwabukusi na Dk. Rugemeleza Nshalla nao wameshiriki mjadala huu. Wawili hawa wamejiwekea utaratibu wa angalau kwa wiki mara moja kulifikia taifa letu kupitia mitandao, mikutano na waandishi wa habari, au kujirekodi wakatuma kwenye mitandao. Wanaitumia vyema haki ya kujieleza inayopatikana. chini ya Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Walioshiriki mjadala huu si wanasheria hao pekee, bali hata wanasiasa akiwamo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeles (CHADEMA), Freeman Mbowe, ambaye naye alitumia uhuru wa kujieleza, ila akavuka mipaka kwa kuleta hisia za udini, U-Tanganyika na u-Zanzibari. Mwabukusi huyo ndiye ameamua kutumia maneno maguma kabisa.

Wakili Dk. Nshalla amekwenda mbali kidogo. Sisi tunaamini si sahihi kwa Wakili Nshalla au mtu yeyote awaye kudhalilisha mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tunalisema hili kwa uwazi kabisa kwamba iwe Rais anatokana na CCM,CHADEMA, CUF, ACT-Wazalendo, NCCR-Mageuzi, TLP, DP na chama kingine chochote cha siasa, alimradi anakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, au Serikali ya Mapinduzi ya. Zanzibar, Watanzania tuna wajibu wa kulinda heshima ya Rais wetu.

Msimamo wa Gazeti JAMHURI ni kuwa maneno aliyotamka Dk. Nshalla ya kumwita Rais Samia muasi, mhaini na kumwelekeza kwamba ampigie simu Mfalme wa Dubai kumweleza kuwa Tanzania si shwari tena na mkataba huo anauvunja, si tu ni utovu wa nidhamu binafsi au yamemdhalilisha Dk. Nshalla pekee, bali hata taaluma ya. sheria nchini. Haiwezekani kwamba Dk. Nshalla hafahamu taratibu za kuvunja, kurekebisha au kuufuta mkataba.

Hatukutarajia, tunalaani na tunashauri isitokee tena hapa nchini mtu yeyote awaye kudhalilisha mamlaka ya urais. Rais ni sura ya nchi yetu. Kwa mfano, wiki iliyopita Rais Samia aliwakillisha Tanzania achini Malawi; alikwenda kama nembo, sura na kioo cha taifa letu.

Kuwaambia watu wanaokutana naye kwamba ni muasi au mhaini, ni kudhalilisha nchi yetu. Uongozi wa Rais Samia usipimwe kwa mkataba wa DP World ambao nao haujasainiwa. Wengi wanasahau ujenzi wa vyumba 18,000 vya madarasa. Wanasahau ujenzi wa Bwawa la Nyerere alilolikuta katika asilimia 37, leo liko karibu asilimia 90. Wanasahau ujenzi wa Daraja la Magufuli alilolikuta chini ya asilimia 10, leo limevuka asilimia 70. Wanajisahaulisha ujenzi wa reli ya lisasa unacendelea na mambo mengi ambayo tukiyaorodhesha hapa tutakesha.

Sisi tunasema hata uhuru wa kusema hayo aliyoyasema Dk. Nshalla ilipaswa kuwa schemu ya shukrani kwa Rais Samia, kwani miaka mitatu iliyopita Dk. Nshalla asingeweza kufungua kinywa kuyasema hayo. Wakati tumempata Rais Samia aliye mvumilivu, anayejenga. mifumo badala ya nchi kuendeshwa na mtu mmoja, tunaamini si sahihi kumdhalilisha kutokana na wema wa kutoa uhuru wa kujieleza anaoutoa kwa Watanzania.

Tuwe na mjadala unaohusu mkataba, lakini si udini, jinsia, ukabila, U-Tanganyika, U-Zanzibari au lolote litakalotugawa kama nchi.

Tukumbuke umoja, amani na mshikamano tulionao sisi Watanzania haukungesha kama mvua. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Sheikh Abeid Amani Karume na marais waliofuata baada yao wamesuka mkeka wa sisi Watanzania kuwa wamoja.

Tusiwaige viongozi wa mataifa jirani wanaotangaza bangi hadharani na kutukuza ukabila kama ngao ya kupata madaraka. Tunahitimisha kwa kutoa rai kuwa kamwe isitokee tena hata kama tunakuwa na mjadala mgumu kiasi gani, kuanza kuchana mkeka wa umoja wetu. Fata kama wano wenve uraia wa mataifa mengine kimyakimya - wao wanapo pa kukimbilia, sisi JAMHURI tunataka tupate maendeleo na kizazi chetu tukarithishe amani.

Tanzania ndipo nyumbani kwetu pekee. Dk. Nshalla na watu wenye hamu ovu ya kumtukana Rais Samia na kudhalilisha mamlaka ya urais, tunawasihi wajiheshimu na wasirudie kumporomoshea matusi Rais Samia.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Wengi walidhani suala la bandari ni kaupepo tu katapita kumbe sivyo mara paap kuizima ishu mkaingiza udini ikabuma,mkaingiza uzenji ukabuma,jinsia ikagonga mwamba now mnaleta suala la udhalilishaji aiseee
 
Umesahau namba ya Simu ndugu
 
Wengi walidhani suala la bandari ni kaupepo tu katapita kumbe sivyo mara paap kuizima ishu mkaingiza udini ikabuma,mkaingiza uzenji ukabuma,jinsia ikagonga mwamba now mnaleta suala la udhalilishaji aiseee
La bandari limeisha, ni kelele tu mnapiga ila Shughuli imeisha siku nyiiiingii
 
yaani unatakiwa ku update ubongo wako , ufanye kazi kiufanisi . bila kusahau ku install new version ya app ya mental capacity .

mtu au kiongozi asiyependa kukosolewa huyo hafai kuwa kiongozi!!
 
Yaani kunyaland wanajitahidi ila mama yuko vizuri sana, mvumilivu, muungwana, mpole, jasiri hatetemeshwi hata na tetemeko la maadui na majirani waovu
Big up mama, Mungu akulinde sana
Ameen
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom