SHERRIF ARPAIO
JF-Expert Member
- Aug 25, 2010
- 9,539
- 5,903
Yaani hata 100K tulioko nje ya bongo hatufiki!! Ha ha ha ha ndio maana mawazo yetu ni mgando
Nilisahau pwenti moja. Sisi hatutumi pesa. Nyie mliioko huko kizani mmefanya nini zaidi ya kuchakachuana. I don't pay damn even if you commit suicide. Kama unaona kuishi nje ni rahisi si uje. Kama unaona ni kubeba maboksi na ukihiyo si uje ujaribu uone. Nyie mlioko huko mkiishi kama mimende hamna bao zaidi ya ulimbukeni na utegemezi. Sisi siyo ATM machines zenu kama alivyotonya jamaa mmoja hapo juu.
Wakuu kutuma hela Tanzania si lazima umtumie mtu unaweza kuwa uajitumia mwenyewe ntatoa ufafanuzi. Wengi wa watanzania walioondoka Tz kabla ya 1990 na katikati ya miaka ya 90 bado hawafahamu namna tanzania ilivyobadilika. Njia rahisi kabisa ya kutuma hela bongo ni kuwa na account Bongo in the currency that you work on abroad. Benki karibu zote hazitozi ile bank fee ya kila mwezi kama account yako ni zaidi ya USD5000.00.
Na kutuma hela za kawaida ($10,000 <) bongo kutoka ughaibuni (interbank transfer) - mara nyingi ni fixed price mfano benki yangu ni $23 na hela zako zinakaa kwenye currency ile ile. Benki nyingi bongo siku hizi zina internet banking kwa hiyo unaweza kuiona na kufanya transaction zako popote pale ulipo. Ukitaka kumtumia hela mtu the only hassle inakuja kama unahitaji exchange rate nzuri maana hiyo ni mpaka bureau de change. Otherwise you can do another interbanking tranfer kwa rates zao au una transfer kwa mtu mwenye account ya foreign curreny anatoa anakuchenjia na kutuma unakokutaka. Utaratibu huu ni mgmu kidogo kwa wale wenzangu ambao kwa sababu binafsi hawawezi kuchomoka huko waliko na kuja bongo at least say one time in 2 years. Ila ni easy and reliable.
Tukija kwenye hoja siyo siri watanzania ni wachache sana nje ya bongo hili hasa naona ndiyo sababu ya diaspora remittances kuwa kidogo namna hiyo.
Kuna njia moja ambayo ndio wengi wanaitumia. Unampa mtu huku pesa then ndugu yako anaambiwa akachukue hela dukani kwa mpemba bongo. Hiyo ndio watu wengi sana wanaitumia siku hizi tena rates ziko bomba mno kuliko sijui moneygram ama W-union
Sio kweli kwamba waTZ ni wachache sana huko Majuu na siyo kweli kwamba wengi wao sio professionals ambao kazi yao ni kubeba maboksi n.k. Shida kubwa kwa waTZ wengi (siyo wote) popote walipo wanakosa uzalendo kwa nchi yao. Wengi hawapendi kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa. Hata hao wafanyakazi waliopo bongo kama wangepewa mishahara yako ili wakalipe kodi wenyewe wengi wangefukuzwa kazi kwa kukosa uaminifu wa kulipa kodi kwa hiari. Mungu bariki kodi ya mishahahra hukatwa juu kwa juu!
Hata hivyo hata kile kinacholipwa na hawa waTZ walioko huko majuu kinapotea kupitia mianya ya rushwa iliyokita mizizi katika nchi hii.
Naomba waTZ wenzangu popote mlipo, tuangalie ni wapi tumepotea njia, turudi njia panda tuiendee njia sahihi kwa maendeleo ya Taifa letu. Sisi ndio wenye maamuzi ya mwisho kuhusu hatima ya TZ kama ni maendeleo au umaskini uliopitiliza.
Kuna njia moja ambayo ndio wengi wanaitumia. Unampa mtu huku pesa then ndugu yako anaambiwa akachukue hela dukani kwa mpemba bongo. Hiyo ndio watu wengi sana wanaitumia siku hizi tena rates ziko bomba mno kuliko sijui moneygram ama W-union
Sio kwamba wabongo hatumi pesa nyumbani, bali ni wachache sana kulinganisha na hao majirani zetu. Wengi wetu tumeanza kutoka juzijuzu hapa wakati Ujamaa ulipoporomoka na globalisation kutuamsha usingizini.
Hao wenzetu, walikimbilia nje kutokana na matatizo ya kisiasa nchini mwao; Waganda tangu enzi za Iddi Amin, na Wakenya kipindi cha Mzee Moi. Wengi wetu kila tunapoenda; popote duniani, utakuta wakenya wapo, tena wengi; Wabongo ukibahatika mnakuwa wawili au watatu, mara nyingi unakuwa peke yako, hadi kulazimisha undugu kwa wakikuyu.