Je, Watanzania mlio nje ni vibarua na wabeba maboksi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Watanzania mlio nje ni vibarua na wabeba maboksi?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Fareed, Feb 8, 2011.

 1. F

  Fareed JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0


  Watanzania wanaoishi nje wanapeleka wapi pesa zao


  WaKenya ambao waaishi huku Tanzania na kwingineko duniani, mwaka uliopita walirudisha nyumbani kwao zaidi ya dola za Marekani $640 million. Wauganda nao walirudisha kwao $850 million mwaka jana. Pesa hizi zinatumika kununua nyumba, kulipa ada za shule, matibabu, nk na zinachangia sana kwenye pato la kigeni la nchi hizi jirani zetu.

  Huko Kenya, pesa zinazotumwa na raia walio nje ndiyo chanzo kikubwa cha nne cha mapato ya kigeni baada ya mauzo ya nje ya chai, mauwa na utalii.

  Benki Kuu ya Tanzania wala haijishuhulishi na pesa zinazotumwa nje na Watanzania na wala haitoi takwimu zake. Kwa mujibu wa makadirio ya Benki ya Dunia, Watanzania wanaoishi nje (diaspora) wengi wenu mkiwa wachangaji wakubwa wa mada humu JF, mwaka jana walitarajiwa kurudisha nchini kwao $17 milion tu?!

  Hii ina maana mbili. Watanzania walio nje ni wachache sana au ni wengi lakini siyo skilled workers wanaoweza kupata kipato kizuri kutokana na taaluma zao. Pengine wengi wenu mnafanya kazi za kibarua, hourly shifts kubeba maboksi and flipping burgers MacDonalds na KFC hivyo hamna pesa za kutuma kwenu nyumbani kwa ajili ya maendeleo na kusaidia ndugu zenu. Si mrudi basi Bongo?

  Au maana nyingine ni kuwa pesa hizo zinatumwa kwa wingi lakini Benki Kuu haifanyi utaratibu wowote wa kuzirekodi. Au zinatumwa kienyeji kwa kufichwa kwenye barua na mizigo mingine. Ama Watanzania mnaendekeza anasa tu huko majuu wakati Wakenya na Waganda wanajenga nchi zao? Nawaza sipati jibu.   
 2. K

  Kambarage Member

  #2
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni aibu kubwa sana. Mimi najua Watanzania wengi wanaoishi nje wamekata mawasiliano kabisa na ndugu zao wa Bongo. Hawana mpango wowote kabisa wa kuisadia nchi yao na wanajiona si Watanzania tena baada ya kuchukua uraia wa huko ughaibuni.
   
 3. T

  The Informer Senior Member

  #3
  Feb 8, 2011
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi takwimu lazima zina walakin, haiwezekani Waganda warudisha nyumbani kwao $850 million halafu Tanzania iwe $17m tu. Yaani pesa wanazorudisha Waganda kwao ni mara 50 ya pesa ambazo Watanzania walio nje wanazileta Bongo.
   
 4. Lisa Rina

  Lisa Rina JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 1,770
  Likes Received: 2,041
  Trophy Points: 280
  Hahaahaa!
   
 5. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu ukweli ni kwamba most of them, kwanza hawajaenda shule hivyo kazi za profession huwezi kupata na wengi wao wanaishi kwa kubahatisha hizo hela za kutuma huko watapata wapi?? Wale professional wachache wanajifanya kama sio watanzania tena na hawataki kusikia kitu chochote kuhusu bongo!! Sio kwamba hawawakumbuki ndugu zao bali hawana cha kutuma:twitch:!!
   
 6. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Ukweli si kwasababu ya kazi!. Watanzania wengi hawategemewi kama Wakenya, Wakenya na Waganda wakienda nje wanategemewa sana na familia kuliko Watanzania hii ni kwa sababu Watanzania wengi wametokea mijini. Wanzanzibar wanategemewa zaidi na wanatuma pesa sana nyumbani. Vilevile Watanzania wanaaminiana sana hivyo pesa nyingi wanatuma kwa watu wanaosafiri. Watanzania wanafanya vizuri tu kimaisha kama watu wengine hayo mambo ya mabox ni pumba tu.
   
 7. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ni hoja nzuri lakini nakushauri ungeuliza balozi za Tanzania katika hizo nchi ambazo ndiko kuna wabongo wengi. Labda wataweza kukupatia data zenye usahihi.
  Mfano;Cheki na ubalozi wa bongo palee DC, sababu tulipokuwa tunabadilisha passport mwaka 2006 walichukua personal info zetu wabongo wote tuishio US.Naamini watakupa picha halisi ni watanzania wangapi wanaishi nje ya nchi, asilimia ngapi tunapiga boksi na wangapi wanapiga white collar schedule.
  Halafu you be the judge.Halafu kama bado unakerwa na hizo data then cheki na balozi za Kenya, uganda au hata Nigeria uliza idadi ya watu wao wanaoishi nje, na details zao nyingine halafu linganisha usahihi wa hizo takwimu.
   
 8. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  si kweli kwamba watanzania hawatumi pesa...na hata hao wakenya na waganda si kwamba hawabebi maboksi au kufanya vibarua..naomba nikueleze kuwa unapokuwa mfanyakazi na kibarua tofauti ya mshahara ni ndogo sana tofauti na kwetu..tena unaweza kushangaa kuona kibarua ni mkorofi kuliko hata boss kwa sababu haofii kupoteza kazi ,kwa sababu anajua kesho atapata kazi sehemu nyingine na utaweza kuona kibarua hanaishi maisha mazuri tu tofauti na unavyofikiri..

  Ngoja nikwambie kitu kimoja unaweza kuwa umesoma una PhD au Masters bado ukaendelea kuwa kibarua kwa sababu si rahisi kupata kazi za oficin kwa sababu hii si nchi yako kwani kuna wazawa bado Prof.lakini hana kazi..Swala la kumkuta mtu ana miaka 25 ana Ph D si swala la ajabu...

  Jaribu kufuatilia hizo takwimu zako BOT huwe na uhakika ujue Watanzania wameweza kutuma kiasi gani..

  Pia kumbuka watanzania wengi wanapojaribu kutuma pesa bongo basi jamaa zao zile pesa huwa wanazituma tofauti na malengo yanayotumwa kwa ajili ya matumizi ya hizo pesa..basi wengi wao huwa wanakata tamaa ya kutuma pesa nje..

  Watanzania si wengi walioko nje kulinganisha na Wakenya kutokana na Watanzia wengi wanabaniana nafasi za kutoka nje...wenzetu wanasaidiana sana na kunyanyuana...
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Watanzania wanatumia money on "envelop system" sababu kutuma kwa njia zinazofahamika kama Western union, Money Gram kwetu bongo bado tuko gizani. Ukisikia mshikaji anakwenda bongo basi unampatia dollar kadhaa akawape nduguzo kwenye bahasha. Envelop system huwezi ingiza kwenye hizo takwimu nina amini watanzania wanasaidia zaidi ya wakenya na waganda. Kuna jamaa fulani waliacha kufanya kazi kabisa wakitegemea mafuba toka kwa kaka yao aliyekuwa Greece.
   
 10. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,305
  Trophy Points: 280
  Kama hizo takwimu ni za ukweli au zina-reflect ukweli basi mimi nadhani tatizo lipo kwenye idadi ya Watanzania waliopo nje. Kumbukeni Watanzania wameanza "kutoka" zaidi kwenye miaka ya 90 na kuendelea. Kusema kweli kwa mtu yeyote aliyewahi kuishi nje atakuambia idadi ya Wakenya ni kubwa... wametapakaa kila mahali na walianza 'kutoka' siku nyingi.
   
 11. F

  Fahari omarsaid Member

  #11
  Feb 8, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pesa zao wanahonga ile mbaya
   
 12. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Watatuma je wakati wao sio raia wa Tanzania, si waliwaomba uraia mkawatilia zengwe na wasomi wenu wa udsm. Mkaambiwa hawa walio nje ni chazo kizuri cha mapato bado mkatia zengwe. Hao wakenya na waganda ni raia wa huko hivyo kuwekeza nchini mwao si ishu. Ishu ni wageni wenye asili ya kitanzania kuwekeza ktk nchi ya ugenini Tanzania.
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sio Kweli Mimi toka niwe huku sijawahi kubeba maboski; I'm qualified Network Engineer --
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Feb 8, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  well said mkuu

  pia tuna barter trade ya nguvu kwasababu tunaaminiana... fanya hivyo kenya uone
   
 15. F

  Fareed JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  BoT wana matatizo makubwa. Nchi zote kila quarter na kila mwaka wanatoa takwimu za remittances. Mini sijawahi kusikia Benki Kuu wakitoa takwimu hizi. Hata kama ni ndogo, lazima zitolewa hadharani hizto takwimu.

  Nadhani Rev. Masanilo yuko sahihi, huenda Watanzania wengi walio nje wanatumia mfumo wa kuweka pesa kwenye bahasha na kuwatuma watu wanaokuja Bongo waje nazo wapeleke kwa ndugu zao. Wangekuwa wanatumia official money transfer systems, eg bank tranfers, western union, money gram, etc basi takwimu zinngekuwa kubwa sana.

  Kuna hii habari ilichapwa na Xinhua mwaka 2008, inaonesha remittances Tanzania zilikuwa just $14m miaka mitatu iliyopita, hivyo pengine sasa hivi kweli ni $17m tu:


  World Bank predicts remittances to Tanzania to fall next year

  2008-11-17

  DAR ES SALAAM, Nov. 17 (Xinhua) -- Remittances from oversea Tanzanians are projected to decrease due to the ongoing financial crisis in the developed world, the World Bank has predicted.
  The World Bank said in its latest migration and development forecast that remittance income in developing countries would decline by 1 percent at least from 2008 to 2009.
  The drop could be as much as 6 percent, according to Dilip Ratha who heads the bank's migration and development research team.
  For both 2006 and 2007, remittance income for Tanzania reached 14 million U.S. dollars.
  Sub-Saharan Africa took in 19 billion dollars in remittances in 2007, or 2.5 percent of the region's gross domestic product, according to World Bank figures.
  In sub-Saharan Africa, Nigeria and Kenya net the largest and second largest yearly remittance incomes.

  World Bank predicts remittances to Tanzania to fall next year_English_Xinhua
   
 16. malkiory

  malkiory JF-Expert Member

  #16
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha mentality za kijinga wewe mtoa mada. Wenzetu Ulaya hawachagui kazi, mtu na PhD yake unamkuta anapangua snow kama kawaida, ili mradi mkono unaenda kinywani . Blue colar workers wa Ulaya huwezi kumlinganisha na Professor wa Tanzania kimapato. Hivyo issue hapa siyo aina ya kazi bali ni kipato. Hivyo nakushauri achana na inferiority complex yako, nikuhakikishie pia kuwa mawazo kama ya kwako yameshapitwa na wakati.
   
 17. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #17
  Feb 8, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Ukiwa nje siku hizi huasaidii ndugu zako, unasaidia mafisadi. Ni bora uisaidie nchi inayokupa hata kibarua cha kubeba boksi, hapa nyumbani wapi unaweza kwenda kubeba boksi? Serikali inawakatisha tamaa, kama ingekuwa na mpango mzuri watanzania pia wanaweza kufanya vizuri.
   
 18. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #18
  Feb 8, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Nikisoma hizi comments napata picha kuwa inaonekana kuna beef kubwa kati ya wabongo waliobahatika kutoka na kuendelea na shughuli zao ughaibuni V/S waliojaribu kuondoka na kugonga ukuta, walionyimwa visa, na wanaotamani kuondoka lakini inawawia vigumu, ama wanaoendelea kupigika bongo na waya mkali.
   
 19. C

  Chuma JF-Expert Member

  #19
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Njia Nyepesi ya kukusanya Takwimu ni kuwa na Njia nyepesi na rahis za Utumai wa pesa home Tanzania. Tumekuwa tunawasiliana na ndugu walionje na inaonekana njia zilizosajiliwa TZ ni ghali sana Kutuma, hadi kutumia njia za Envelope kama alivyosema mchangiaji mmoja.

  Ukiangalia wenzetu kenya na Uganga wame-officialize njia zote then Central Government zao zinazitambua.

  Sheria za Utumaji wa pesa bongo zimeruhusiwa only kwa banks na Western Union...ambazo zote ni Ghali. kwa utaratibu huu kupata takwimu Halisi ni ngumu sana. Nafikiri Serikali ingeruhusu njia za Money Exchange kutuma na kupokea pesa, then wakawa na Control na System. Wanaweza kuwa na System za Computer itakayokuwa wanatumia Money Exchange wote ktk hili..hata wakisema GOT/BOT watakuwa wanachukua shiling 10 kwa kila amount inayotumwa, hawatoweza kosa chochote ktk Pato la Taifa.

  Pia Suala la Uchache wa Watz nje ya Tanzania si suala la Kudharauliwa...Zipo sababu nyingi ambazo wachangiaji wengi wanaweza zitoa.
   
 20. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #20
  Feb 8, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Idadi ya WaTZ ni ndogo sana huku ughaibuni ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika.
  Hebu fikiria nchi kama Gambia yenye idadi ya watu 1M ndani ya Gambia lakini ina watu zaidi ya 1M nje ya Gambia??
  Wakenya walianza kuzamia hapa nchi za Ulaya na Amerika toka 60 wakati sisi tumeanza 90.
  Wenzetu watu wanao zamia ni aina zote wakati sisi wazamiaji wengi ni watoto wa viongozi wa serikali ya CCM ambao kamwe hawaoni haja ya kutuma fedha kwa wazee wao walionona fedha za wizi.

  Pengine ingewekwa Takwimu ya Madingi wa Kitanzania wanao tuma fedha kwa watoto wao Huku ghaibuni Tanzania ingeongoza.

  Hata hivyo si kweli kwamba vipato vya watanzania ni vidogo huku ughibuni. Tuko wachache.

  Wagambia waishio Marekani kwa mfano ni zaidi ya 150,000 wakati waTanzania waishio marekani wako chini ya 25,000 kwa Takwimu za miaka3 iliyopita, wengi wao wakiwa wamelelewa kwenye mazingira ya joto la THERMOS kule Oysterbay.

  Wakenya sijui idadi yao lakini nadhani wako zaidi ya 200,000, wao wanakuja huku wakiwa tayari wamejeruhiwa na maisha ya kubanwa kule Kenya wajanja kweli kweli, wakati sisi Watanzania tunakuja huku tukitarajia tumeukata tunakuja kutesa, zaidi tunawaz kununua magari furniture na kuopoa mademu wa kizungu. Siwezi kuwasemea dada zetu.

  Bado tunaipenda nchi yetu, madai yetu ya uraia wa nchi mbili ni madai ya msingi. Hebu fikiria watoto wangu wote wamezaliwa hapa wana Passport za USA.Kisheria ni Wamarekani kwa sababu wamezaliwa hapa Je nchi yangu Tanzania ipo tayari kuwakubali wawe raia wa Tanzania pia?? Je kuzaliwa kwao nje ya Tanzania ndiyo sababu ya kuwafanya wasiwe raia wa Tanzania?? Kosa lao ni nini kutokua raia wa Tanzania??

  Waganda na Wakenya wote wanaruhusiwa kuwa raia wa nchi zote mbili ya ughaibuni na ya kwao. Sisi kwa sababu bado tunatekeleza Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea hilo linaonekana ni uasi kwa nchi.

  Maoni mengi yanatoka vijiweni zaidi kuliko kureflect ukweli.
  Maisha hapa ughaibuni ni magumu sana hata ukilipwa fedha nyingi bado maisha si marahisi kwa sababu ya setup ya system nzima.
  Dar ukilipwa $4000.00 umeukata kweli kweli hapa USA inategemeana uko state gani hawa wenzetu wana Tax za kuua mtu pili system imejengwa ili kuhakikisha unarudisha fedha yote kwao mabepari.
  Wewe unaweza ishi kwa kula Bamia na ugali kila siku watoto wako waliozaliwa hapa watakugomea na mwisho wataishia kula shuleni wakirudi nyumbani hawali. Hivi unadhani kila uchao utamwekea Lunch Box ya wali na nyama au maharage mtoto wa Kitanzania aliyezaliwa Marekani??

  Kuna tatizo la kutuma fedha Tanzania ksiha ndugu zako kukugeuza mjinga , wenyewe wanaita ATM.
  Unatuma fedha ya kujenga nyumba yako au kurekebisha nyumba ya mdingi kijijini nduguzo ikiwa ni pamoja na mdingi wako wanaishia kujengea Tumboni Street na wengine kupata maradhi kwa sababu ya fedha yako.Mwisho unalaumiwa kwa kutuma fedha na kusababisha songombingo.

  "Tangu uanze kumtumia fedha baba yako hapa nyumbani halali!!"

  Wazazi au ndugu kuwa na matumaini makubwa kuopita kiasi hadi kufikia kuuliza mbona wewe hutumi fedha wakati so and so wanatuma fedha kila siku??

  Yaani kila anyezamia Ughaibuni baada ya miaka 2 ni lazima awe ameukata??
  Ukiwa abused namna hiyo na purukushani zote za First World si ndiyo hapo unaamua kula jiwe mpaka kielewke??


  Wengi wamekuja ulaya kwa Package ya Scholarship, japo wamekaa miaka 3-4 system hawaijui hata kidogo wakirudi Bongo wanapaint picha tofauti kabisa na kufanya kila mtu huku aonekane si mzalendo huku ughaibuni.

  Niliporudi Tz rafiki yangu mmoja aliniambia nirudi Bongho kwani najicheleweshea maendeleo yangu.
  Katika kunipa stori ya namna alivyopata fedha niliishia kujua kwamba kila kitu kuanzia nyumba hadi utitiri wa magari ni matokeo ya Rushwa wizi na unyang'anyi wa kutumia nafasi yake, madaraka yake na loophole ndani ya system. Sikumwonea wivu hata kidogo kwa sababu;

  Wizi niliukataa zamani nikiwa mtumishi Tanzania naukataa leo na kesho.

  Katika miaka 10 ya utumishi wangu Tanzania nilifanikiwa kubana matumizi na kujenga nyumba 2 kisha kununu gari na kuoa. Vitu hivyo vinne vilinigharimu kila kitu nilichokua nacho na hata kunipachika jina la ugumu katika pesa,Roho ya korosho. Bado najivunia nyumba zangu mbili nilizo zijenga kwa taabu kwa pesa ya mshahara kwa kipindi cha miaka 10.(Enzi hizo mfuko wa cementi Tshs 2000 Mshahara kwa mwezi Tshs 12,500.00)japo kwa kiwango cha sasa nyumba inaonekana hafifu na ndogo.

  Wengi hapa tunaishi kama ambavyo tungeishi Tanzania.
  Wengi waishio Tanzania wanakunywa Bia kila siku, wanatembea na kila mtu wamtakaye, lakini wazazi wao hawawakumbuki. Lawama za kuto tuma fedha kwa wazazi tunajaziwa sisi tulioko ughaibuni.
   
Loading...