GE2025 Je, wanaharakati wana haki ya kuzuia wengine wasipige kura?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Je, wanaharakati wana haki ya kuzuia wengine kupiga kura?

  • Wana haki kuzuia wengine kupiga kura

  • Hawana haki kuzuia wengine kupiga kura

  • Sijui

  • Sijali

Results are only viewable after voting.

Kiranga

Platinum Member
Joined
Jan 29, 2009
Posts
85,695
Reaction score
145,396
Je, wanaharakati wana haki ya kuzuia wengine wasipige kura?

Tuna siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025. Uchaguzi huu umegubikwa lindi la kukosa uhalali pengine kuliko uchaguzi mwingine wowote Tanzania.

Hata mgombea wa CCM ameshutumiwa na mpaka kufunguliwa kesi kuwa kajipitisha bila kufuata utaratibu.

CHADEMA imesusia uchaguzi. Mgombea wa ACT Wazalendo kazuiwa kushiriki, ingawa kuna wanaosema kafanya makosa mwenyewe. Wagombea wengi, hata ndani ya CCM wamekatwa bila sababu za kueleweka.

Kuna watu wengi wanalalamika kuwa uchaguzi hauna uhalali, tume ya uchaguzi inachaguliwa mwenyekiti na rais anayegombea urais pia katika uchaguzi, na matatizo mengine mengi ya kikatiba na kiuendeshaji.

Hivyo, wanaharakati wengi wanataka kuandamana siku ya uchaguzi tarehe 29 October. Hiyo ni haki yao ya kikatiba.

Lakini, wengine wanakwenda mbali zaidi, wanataka kufanya civil disobedience kuzuia wengine wasifanye uchaguzi. Hawa si tu wanataka kuandamana, bali pia wanataka kuzuia uchaguzi hata kwa kutumia fujo na nguvu.

Wanasema huu si uchaguzi, ni uchafuzi, ni maigizo, ni figisu tupu. Hivyo, wana haki ya kuuvuruga usifanyike.

Lakini, kuna watu wameamua kushiriki kwenye uchaguzi huu. Kwa kujua na kukubali huu si uchaguzi ni uchafuzi, au kwa kutokujua na hata kukataa habari hiyo inayopinga uhalali wa uchaguzi.

Na wao wanasema wana haki yao kushiriki uchaguzi huo, na wana haki ya kufanya uamuzi binafsi kwamba uchaguzi huu ni halali au si halali, waachwe waitumie haki yao. Demokrasia si kulazimishana, ni watu wote kupata uhuru wa kufanya maamuzi wanayoona ni sahihi.

Hili ni swali muhimu na gumu kifalsafa.

Kuna wanaharakati wanasema wana haki ya kuvuruga uchaguzi usio halali.

Kuna wapiga kura wanasema haki yao ya kuamua kupiga kura iheshimiwe.

Haki hizi mbili zinaonekana kugongana.

Tunapitaje hapa kwa usalama bila kuvunjia kundi moja la wanaharakati haki yao ya civil disobedience kuvuruga uchaguzi, lakini pia tusiwavunjie watu walioamua kupiga kura?

Na kama hatuwezi ku maintain haki zote, haki ipi inaipiku nyingine? Kwa sababu gani?

Naomba mazungumzo ya kidhahania zaidi, yajikite kwenye sababu za kifalsafa Zaidi, kimantiki, kuliko kuwa na mjadala wa kisasa wenye hisia zaidi.
 
Cha kwanza watakao zuia watu wasipige kura siyo wanaharakati bali ni sisi wananchi na tarehe 29 tunakiwasha

Tumeshaandaa mipango yote ya kuchoma kituo cha kura kilichopo hapa mtaani na hata mwenyekiti wa mtaan anajua
 
Uchaguzi huu watakaoenda kupiga kura ni
1. Maskini wa kutupwa wasiojielewa
2. Wanachama wa CCM kindakindaki
3. Walionunuliwa Ili wakawapigie kura watu wapate kula.

Tofauti na makundi hayo hapo juu hakuna mtu wa kupiga kura mwaka huu.

Na wanaotaka kuzuia ni Kwa sababu wananchi wengi wanaangukia kundi namba moja.

Uchaguzi wa mwaka huu hauna uhalali hata mbinguni.
 
Uchaguzi utafanyika katika mazingira yoyote yale, yawepo au yasiwepo maandamano.
Kwa sheria za nchi yetu, serikali kutokujali maoni ya walio wengi na pia kukosa uungwana hata watu wawili wakipiga kura uchaguzi utahesibaka umefanyika na mshindi atatangazwa kushinda kwa 50% au 100% kama kura zote mbili hazitaharibika kwa hiyo hakuna namna maandamano kama yatakuwepo yanaweza kuzuia uchaguzi kufanyika hata yakiwa makubwa kiasi gani, suala litakalobaki kama wingu kichwani mwao ni uhalali(legitimacy) wa hiyo serikali itakayokuwa madarakani.
 
Je, wanaharakati wana haki ya kuzuia wengine wasipige kura?

Tuna siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025. Uchaguzi huu umegubikwa lindi la kukosa uhalali pengine kuliko uchaguzi mwingine wowote Tanzania.

Hata mgombea wa CCM ameshutumiwa na mpaka kufunguliwa kesi kuwa kajipitisha bila kufuata utaratibu.

CHADEMA imesusia uchaguzi. Mgombea wa ACT Wazalendo kazuiwa kushiriki, ingawa kuna wanaosema kafanya makosa mwenyewe. Wagombea wengi, hata ndani ya CCM wamekatwa bila sababu za kueleweka.

Kuna watu wengi wanalalamika kuwa uchaguzi hauna uhalali, tume ya uchaguzi inachaguliwa mwenyekiti na rais anayegombea urais pia katika uchaguzi, na matatizo mengine mengi ya kikatiba na kiuendeshaji.

Hivyo, wanaharakati wengi wanataka kuandamana siku ya uchaguzi tarehe 29 October. Hiyo ni haki yao ya kikatiba.

Lakini, wengine wanakwenda mbali zaidi, wanataka kufanya civil disobedience kuzuia wengine wasifanye uchaguzi. Hawa si tu wanataka kuandamana, bali pia wanataka kuzuia uchaguzi hata kwa kutumia fujo na nguvu.

Wanasema huu si uchaguzi, ni uchafuzi, ni maigizo, ni figisu tupu. Hivyo, wana haki ya kuuvuruga usifanyike.

Lakini, kuna watu wameamua kushiriki kwenye uchaguzi huu. Kwa kujua na kukubali huu si uchaguzi ni uchafuzi, au kwa kutokujua na hata kukataa habari hiyo inayopinga uhalali wa uchaguzi.

Na wao wanasema wana haki yao kushiriki uchaguzi huo, na wana haki ya kufanya uamuzi binafsi kwamba uchaguzi huu ni halali au si halali, waachwe waitumie haki yao. Demokrasia si kulazimishana, ni watu wote kupata uhuru wa kufanya maamuzi wanayoona ni sahihi.

Hili ni swali muhimu na gumu kifalsafa.

Kuna wanaharakati wanasema wana haki ya kuvuruga uchaguzi usio halali.

Kuna wapiga kura wanasema haki yao ya kuamua kupiga kura iheshimiwe.

Haki hizi mbili zinaonekana kugongana.

Tunapitaje hapa kwa usalama bila kuvunjia kundi moja la wanaharakati haki yao ya civil disobedience kuvuruga uchaguzi, lakini pia tusiwavunjie watu walioamua kupiga kura?

Na kama hatuwezi ku maintain haki zote, haki ipi inaipiku nyingine? Kwa sababu gani?

Naomba mazungumzo ya kidhahania zaidi, yajikite kwenye sababu za kifalsafa Zaidi, kimantiki, kuliko kuwa na mjadala wa kisasa wenye hisia zaidi.
Yote yanawezekana kufanyika siku Moja maandamano na kupiga kura, watawala wasiwe waoga si wanakubalika na wananchi.
 
KUMEKUWA na porojo za muda mrefu sana kuwa kuna wanaharakati uchwara wanaweza kuzuia uchaguzi usifanyike na wanadanganyika na kauli za watu kama akina heche kuwa wanazuia uchaguzi na hakuna uchaguzi utafanyika..

Kwa mara nyingine tena tunawaambia kuwa uchaguzi ni suala ziti sana la kikatiba na linafanywa kwa kuwa lazima katiba iheshimiwe na jaribio lolote la kuzuia katiba kutekelezwa maana yake nikuzuia demokrasia na kupelekea kuwa na uongozi usio madarakani kiuhalali kwa kuwa haukuchaguzliwa kwa mujibu na matakwa ya kikatiba.

Jana kwenye mahojiano fulani padre wenu wa TEC mwanaharakati Padri Kitima amesema kwa ufasaha sana kuwa uchaguzi lazima ufanyika na wao kama TEC wako tayari kufanya kazi na uongozi wowote utakaochaguliwa baada ya uchaguzi huo.
 
Kuna wanaharakati wanasema wana haki ya kuvuruga uchaguzi usio halali.
Mkuu hili neno wanaharakati nashindwa kufahamu huwa unamaanisha kina nani. Juzi ulikuja na habari kutoka kwa page ambayo hakuna anayejua ni ya nani lakini ukaipa jina la mwanaharakati.

Naomba unijuze hao wanaharakati wanaosema wana haki ya kuvuruga uchaguzi. Ikiplendeza uweke na rejea za hao wanaharakati waliosema hivyo
 
Back
Top Bottom