DOKEZO Je, Wanafunzi kuchoma mkaa ni sahihi? Waziri wa Elimu na Mkuu wa Mkoa Kigoma fuatilieni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Don Moen

JF-Expert Member
Nov 12, 2020
1,566
2,944
Ni jambo la kushangaza wanafunzi kufanyishwa kazi za kubeba magogo na kuchoma mkaa kwa ajili ya waalimu wao.

Lugufu girls high school iko Wilaya Uvinza na kabla ya shule hii kuanzishwa ilikuwa ni makambi ya wakimbizi.

Shule hii iko porini sana na ili ufike ukitokea Uvinza mjini kielekea Kigoma mjini utashuka Lugufu polisi na ndipo uchukue boda boda ya sh 5000 hadi 7000 kuelekea Lugufu high schools ambazo kuna ya wasichana pekee na wavulana pekee zikiwa jirani kabisa.

Shule hii mkuu wake ni mwanamke katili na asiyemuelewa kabisa.

Jambo baya ni aina mkuu wa shule mpenda pesa kupindukia, huwafanyia wanafunzi biashara ya chakula na maziwa. Huangalia wazazi wenye uwezo na kuanza kukisha watoto wao kwa kulipia bills kwa mwezi.

Mwanafunzi akishindwa kulipa bills zake hatoruhusiwa kwenda likizo hadi wazazi watume pesa, hii sijui imekaaje.

Jambo la pili hupewa kiasi kidogo na waalimu na kuwaruhusu wasichana wadogo wa f5 na 6 kwenda kubeba magogo porini kwa ajili ya kuchoma mkaa wa waalimu. Kutokana na tabia hii watoto hufeli sana mitihani yao ya terms.

Kwa tabia hii wazazi wengi wamehamisha watoto wao sana.
Mfano watoto wa tahasusi ilikuwa na wanafunzi zaidi ya 73 wamehama na kubaki 11 tu.

Kwa hali hii hawatendei haki watoto, wazazi na taifa. Mimi nilikuwa na binti yangu pale na alikuwa na matokeo mabovu mno kila mtihali alipata div. 4, nimemhamidha shule nyingine kwasasa anapata div one kuanzia ya 4 hadi 6.

Waziri wa elimu tumia wakaguzi wa elimu kunisuru shule hii.
 
Hii taarifa isipokuwa jungu sijui, umeandika kinafiki Sana. Ila sawa mamalaka zitafanyia kazi. Ila just tu, mwanao umemlea kimayai Sana, ndo maana anakuletea taarifa
 
Hii taarifa isipokuwa jungu sijui, umeandika kinafiki Sana. Ila sawa mamalaka zitafanyia kazi. Ila just tu, mwanao umemlea kimayai Sana, ndo maana anakuletea taarifa za kipuuzi
Mbona kama umeguswa sana mkuu wewe ni mwalimu? Miongozo ya wlimu inaruhusa haya?

Si ameomba mamlaka ifuatilie na ukweli utajulikana?. Ikiwa jamaa kalea mtoyo kimayai mbona na wengine wamehamisha watoto toka 73 hadi 11?
Japa pia ametoa ushuhuda wa mwanae kupata matokeo chanya huoni kuwa ana hoja?

Au umesoma shule za kata ndanindani wanakong?'oa visiki unataka watoto wote wapitie huko?
 
Kama hauku pitia jambo hili jua wazi kabisa wewe niwale wa bus la njano
20220825_095143.jpg


Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mbona kama umeguswa sana mkuu wewe ni mwalimu?
Miongozo ya wlimu inaruhusa haya?
Si ameomba mamlaka ifuatilie na ukweli utajulikana?.
Ikiwa jamaa kalea mtoyo kimayai mbona na wengine wamehamisha watoto toka 73 hadi 11?
Japa pia ametoa ushuhuda wa mwanae kupata matokeo chanya huoni kuwa ana hoja?
Au umesoma shule za kata ndanindani wanakong?'oa visiki unataka watoto wote wapitie huko?
Umemjibu vyema
 
Nikwambie kitu? Wewe ni mwalimu, umegombana na mkuu wako umeamua kuja kumchafua huku.

Hao watoto hawachomi mkaa ila huwa wanasogeza kuni za kuchomea mkaa.

Sisi pale Ifunda tulikuwa tunapalilia shamba LA shule mwisho huoni, bonge LA shamba. Ndio maana Leo hatuna ajira ila hatufi na njaa.
 
Back
Top Bottom