Je wanadamu tuna FREE WILL??

Free will tunazo ila hakuna kiumbe kisicho na fomula ,kwamba ukistep nje ya fomula utapata madhara.
Ila pia tuko controled kwa kiasi fulani tangu kuzaliwa kwetu..
Ndio maana kila kitu kina negative na positive.. kila kitu kina kinyume

Ila yale matukio ya zama huwaga yameshaandaliwa katika mfumo huo huo wa + -
Kwahiyo kila litokealo kama sio matokeo hasi basi matokeo chanya.

kwa mfano yuda asingemsaliti angetokea mwingine kwasababu yupo mtu wa aina ya yuda siku zote ,na yeye angali ametumia free will kujitoa katika dhambi.. lakini lile tukio la usaliti liko pale pale... ndio maana katika bible wanasema "ili litimie neno lililonenwa na manabii" kwamba matukio tayari yapo controlled kama Unavyoona Ratiba ya harusi nk ila je nani atayakamilisha ndio inapokuja hio "FREE WILL"
 
Reactions: Cyb
Free will tunazo ila hakuna kiumbe kisicho na fomula ,kwamba ukistep nje ya fomula utapata madhara.
Ila pia tuko controled kwa kiasi fulani tangu kuzaliwa kwetu..

So nikawaida kabisa
Tuko controlled na nani mkuu?
 
Hakuna kitu inaitwa freewill,always kuna causality somewhere!

Hii Freewill ya kwenye bible ni pure lie na myth tu.

Mwanangu Sam Harris ka-debunk it left and right!

See him here:

Kama hatuna free will basi huu uzi umeujibu kwa kushurutishwa?
 
Reactions: Cyb
Kama hatuna free will basi huu uzi umeujibu kwa kushurutishwa?

Mkuu

Umemsikiliza Sam Harris hapo mkuu?

Ni kwamba mpaka nimeingia humu kujibu hii post yako inajumlisha countless of causers ambazo ni seen and unseen internal and external...mpaka ubongo wangu unakubali kuchapa keyboard yangu hapa kukujibu ni baada ya minyukano ya causes chungu nzima,zilizokua powerful zimeshinda ndio maana nikachapa keyboard hapa..

Msikilize Sam Harris hapo,Free Will imekua debunked kushoto kulia!
 
Huu ndio ukweli.

Hata wanaotengeneza vyombo vya kutumia kama mashine au magari, kuna menu za vyombo hivyo, jinsi ya kuvitumia na kuvitunza.
Binadamu pia ana menu yake inayomwelekeza jinsi ya kujitumia na kuishi.
Mungu kupitia maandiko matakatifu ameeleza kila kitu kuhusu Binadamu aliye muumba, aishi vipi na jirani, ale nini, avae nini, afanye nini, asifanye nini ili aishi vizuri na kujitunza afya yake imavyopasika.
Mambo hayo yako wazi kabisa kwa mfano imeandikwa, usiue, usizini, mpende jirani yako, usiibe, NK.
Sasa wewe unazini na mke wa mtu, au unaiba au unaua, watu wanakukamata wanakuua kwa kukuchinja au kukuchoma moto au kwa kipigo, halafu unaanza kumlaumu Mungu eti haja kulinda.
Unaanza kimsingizia Mungu eti ameumba dunia yenye machafuko ya vita na kadhalika kadhalika.
Umeambiwa kabisa usipotii Neno la Mungu hakika utakufa, sasa kwanini lawama.
Neno la Mungu ndio afya na ulinzi wenyewe.
Amri ambazo Mungu ameziweka ili tuzifuate, zimewekwa kwa manufaa yetu wenyewe ili tustawi hapa duniani na kufurahia maisha.
Tusipo zifuata basi tukubali madhara yatakayotupata, chanzo ni sisi wenyewe.
Ndio maana mtu akipigwa kwa kufumaniwa haendi kushtaki popote, anajua amestahili adhabu hiyo.
Wajibu wa kufanya Wema au Ubaya upo mikononi mwetu.
 
Binadamu ana Free will ya kutenda mema tu.
Kwenye kutenda mabaya Binadamu hana Free will.
Tupo huru kufanya mambo mazuri kama kufanya kazi, kuabudu, kujiburudisha, kusaidia wengine, kula chakula nk.
Katika kufanya uovu Binadamu hana uhuru.
Ukimtukana mtu utashtakiwa na kufungwa jela. Ukibaka utauawa na watu wenye hasira, ndio maana watu wanaogopa kufanya maovu.
Hatupo huru kufanya uovu.
Tupo huru kufanya mambo mema tu.
 
Free wil ni contradiction kwani Mungu mwenye uwezo wote haiwezekani binadam akawa free! Kila anachofanya mtu Mungu anajua ! Hiyo free wil imetoka wapi ?
 
katika amri za mungu ya pili anasema "nami nawaptiliza wana na maovu ya Baba zao,hata kizazi cha tatu na cha nne wanichukiao...so kama mzee Wako alikosa,,utahukumiwa hadi wewe..
BASI huyo mungu ni balaa
 
kama tunayo basi itakuwa ni freewill ya mwendokasi 😱😱 maana hiyo freewill haiwezekani niikute wakati nishafika duniani 😳😳 ilitakiwa niipate kabla ya kuja duniani hiyo sio freewill hiyo ni lazima case closed
 
Good summary!!
Mazingira, makuzi, elimu, mila na desturi, n.k zimemuathiri mwanadamu katika free will yake sana.
Safari ya kiroho ni ya upekee kwa maana ya kuwa kila mmoja ameumbwa tofauti kuufikia u yeye wake....spiritual path

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliwahi kuandika thread hapa hapa jukwaani kuhusu usaliti wa yuda kwa yesu kuwa ni tulio/kitendo kklichopangwa kabla ila yuda alikuja kukamilisha script iliyotayali lakini kwa maksudi mods waliufuta ule uzi.Katika suala la free will binadamu na viumbe wengine hicho kitu hatuna bali limewekwa kiimani ili kuhalalisha adhabu ambazo mungu anasema atazitoa kwa wakosefu.Kama mungu kweli ametupa uhuru wa kuchagua mema na mabaya kwanini achikizwe na machaguo yetu,kama alikuwa hataki mabaya yafanyike aliyaumba kwa sababu gani,kwanini alimuumba binadamu ambaye anaweza kutenda mabaya ambayo yeye hayapendi.Hii dhana ya free will naipinga sana sababu ni illogic kabisa hivi kwanini mungu alimuumba shetani kama yeye anachukizwa na vitendo vyake?maswali ni mengi kuliko majibu.......Vitabu vinasema mungu anajuwa yaliyopita yaliyopo na yajayo,kama mwakani wewe au mimi nitafanya zinaa mungu anajuwa kabla hata ya kufanyika kitendo hicho,na kwa kuwa mungu anajuwa ni lazima hilo tendo nilifanye ili kuleta maana ya god is perfection tofauti na hapo mungu hatakuwa na sifa hii.Je kama nitafanya hili tendo huo mwwaka huoni kuwa sikuwa na uhuru wa kuchagua sababu my fate ilikuwa tayari existed.Binadamu hatuna freewill mungu anatuonea kwa kutupa adhabu ambazo yeye ambaye ni perfection angeweza kuziondoa since day one of creation


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu upo sahihi. Hata utatuzi wa jambo utegemea kuelewa kwanza kipi ni chanzo kwa asili.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bro free will tunayo that why tunajua lipi ni jema na lipi ni baya na tuuwezo wa kuchagua na kwa upande wa Yuda alitumia free will kumuuza Yesu na mpango wa Mungu ulikuwa kumkomboa binadamu kwa njia kifo na mateso lakini si mpango wa Mungu kwa Yuda kumsaliti Yesu kilichotokea kwa Yuda ni misuse of our freedom ( free will) ikampelekea Yuda kumuuza Yesu ukitaka ku prove hii Yesu alimlaumu Yuda kwa kitendo chake kwani alimwambia kwa kitendo anachodhamilia kukifanya ni heri asingezaliwa hivyo free will ipo


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwa upande wangu naweza kusema kuwa free will anayo Mungu sisi tunapewa kama gifts after birth ila sio kwamba u can do each and everything bila sir God kujua kinachoendelea

Sent using Infinix hot 4
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…