Je, walikiamini walichokihubiri ?

Fred Mpendazoe

Verified Member
Aug 21, 2016
33
900
Ninaona maandiko mengi yakieleza kwamba hatua nyingi zinazochukuliwa na Serikali ya CCM chini ya uongozi mahiri wa JPM, yalisemwa na Chadema kupitia Tundu Lissu au Mnyika au Mbowe. Hii siyo hoja imara.

Hapa duniani wapo watu ambao wanaweza kusema jambo ukadhani wanasema jambo hilo kwa dhati kumbe wanaamini tofauti kabisa. Mfano Chadema walimsema sana Lowassa kama fisadi kwa zaidi ya miaka 10, lakini hawakuyaamini waliyoyahubiri. Ndiyo maana mwaka 2015 wakampokea Lowassa kuwa mgombea urais. Watanzania wakaihukumu Chadema kwenye uchaguzi Mkuu.

Wabunge wa Chadema wamehubiri sana demokrasia na kufanya maandamano kudai demokrasia pana. Wabunge hao walifunga midomo kuonyesha hisia hizo wakiwa bungeni. Lakini uteuzi wa wagombea ubunge wa bunge la Afrika Mashariki ikadhihirisha kwamba wanachokisema si kile wanachokiamini. Ndani ya Chadema demokrasia ni kwa masilahi mapana ya kikundi cha watu.

Kwahiyo madai ya Chadema na viongozi wa Chadema kudai kwamba yanayotekelezwa kwa sasa wao waliyasema siku nyingi ni hoja isiyo na mashiko.
Jambo lililo mhimu na la msingi ni mwenendo chanya wa viongozi na wanachama wa chama cha siasa kwa jamii. Pili chama cha siasa kinatakiwa kusimamia kinachokiamini. Siyo kuhubiri tu.

Kingine, lugha zinazotumika na baadhi ya viongozi wa Chadema mara nyingi huonyesha upungufu wa maadili na inawafanya watanzania wajiulize, je watu hawa wakipewa madaraka watakuwaje ? Ukosoaji wa Chadema umekuwa wa matusi. Na ukiwa mtukanaji wa Serikali utapewa sifa nyingi sana na hata kuitwa jiniasi- genius. Ni ujinga. Hitler alikuwa genius lakini alikuwa mharibifu pia. Unaweza ukawa genius na unajua sana sheria lakini bila moyo wa uzalendo hautakuwa na faida kwa jamii.

Rais JPM anafanya kazi njema, watanzania tumuunge mkono.
 
Laface77

JF-Expert Member
Jul 9, 2008
2,116
2,000
Moja ya maandiko bora kabisa ya mmoja wa ng'ombe waliokatwa mkia! Ulianzisha CCJ ikafa kabla haijaanza, ukaja CHADEMA ukitegemea cheo/ubunge ukapigwa kotekote sasa hivi umerudi kundini lakini umeshakatwa mkia!Pole sana mzee naona unaendelea kuweweseka tuu.
 
funza

JF-Expert Member
Sep 5, 2013
7,481
2,000
Ninaona maandiko mengi yakieleza kwamba hatua nyingi zinazochukuliwa na Serikali ya CCM chini ya uongozi mahiri wa JPM, yalisemwa na Chadema kupitia Tundu Lissu au Mnyika au Mbowe. Hii siyo hoja imara.
Hapa duniani wapo watu ambao wanaweza kusema jambo ukadhani wanasema jambo hilo kwa dhati kumbe wanaamini tofauti kabisa. Mfano Chadema walimsema sana Lowassa kama fisadi kwa zaidi ya miaka 10, lakini hawakuyaamini waliyoyahubiri. Ndiyo maana mwaka 2015 wakampokea Lowassa kuwa mgombea urais. Watanzania wakaihukumu Chadema kwenye uchaguzi Mkuu.

Wabunge wa Chadema wamehubiri sana demokrasia na kufanya maandamano kudai demokrasia pana. Wabunge hao walifunga midomo kuonyesha hisia hizo wakiwa bungeni. Lakini uteuzi wa wagombea ubunge wa bunge la Afrika Mashariki ikadhihirisha kwamba wanachokisema si kile wanachokiamini. Ndani ya Chadema demokrasia ni kwa masilahi mapana ya kikundi cha watu.

Kwahiyo madai ya Chadema na viongozi wa Chadema kudai kwamba yanayotekelezwa kwa sasa wao waliyasema siku nyingi ni hoja isiyo na mashiko.
Jambo lililo mhimu na la msingi ni mwenendo chanya wa viongozi na wanachama wa chama cha siasa kwa jamii. Pili chama cha siasa kinatakiwa kusimamia kinachokiamini. Siyo kuhubiri tu.

Kingine, lugha zinazotumika na baadhi ya viongozi wa Chadema mara nyingi huonyesha upungufu wa maadili na inawafanya watanzania wajiulize, je watu hawa wakipewa madaraka watakuwaje ? Ukosoaji wa Chadema umekuwa wa matusi. Na ukiwa mtukanaji wa Serikali utapewa sifa nyingi sana na hata kuitwa jiniasi- genius. Ni ujinga. Hitler alikuwa genius lakini alikuwa mharibifu pia. Unaweza ukawa genius na unajua sana sheria lakini bila moyo wa uzalendo hautakuwa na faida kwa jamii.

Rais JPM anafanya kazi njema, watanzania tumuunge mkono.

Wewe acha uongo wako propaganda za kumchafua Lowasa zilikuwa zikitoka CCM na kuwapelekea Wapinzani lakini Lowasa alipokwenda chadema alianika A-Z Ukweli wote kwa kuwambia kuwa Richmond ni ya kikwete, watanzania hawakumhukumu Lowasa kwenye kura walimchagua vizuri alipata kura nyingi lakini CCM walifanya uchakachuaji mkubwa,

JPM hajafanya kazi njema kwani amecopy vilio vya Wapinzani tokea zamani na kujidai yy ndiyo kaanzisha kulia juu ya wizi huo watanzania sio wajinga hawapo nyuma ya magufuli upo peke yako na wajinga wachache,

watanzania wengi wanataka mkapa na kikwete wafikishwe mahakamani kwani wao na wabunge wa CCM ndiyo waliosababisha yote haya na kama si wabunge wa CCM kwa sema ndiyooooo.. leo hii tusingekuwa tunaijadili hii.
 
The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
15,588
2,000
Lakini kumbuka hata mkubwa nae anatumia lugha hizohizo kwa wapinzani. Siafiki lugha zisizo na staha hata kama tunakosoa jambo. Unaweza kuongea kiungwana tu ukaeleweka, upinzani haimaanishi kupinga kila jambo, kutumia lugha tata na wakati mwingine matusi.

Huu ni wakati wa kuweka tofauti, ubabe na ushabiki pembeni kwa manufaa ya nchi yetu.

Akija rais mwingine akasema barabara mbovu, ndege kuna ufisadi, sgr kuna ufisadi tutamshangilia na kusahau tulimsifu hivyohivyo aliyekuwepo madarakani wakati yanatokea.

Serikali/JPM ajikite kutekeleza wajibu wake na kuendeleza kazi ya kujenga nchi, hiyo ni njia bora zaidi kuliko zote za kupambana na upinzani.

Unaongeleaje kauli ya maagizo kwa spika kuwabana wabunge wa upinzani?
 
Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,056
2,000
Ninaona maandiko mengi yakieleza kwamba hatua nyingi zinazochukuliwa na Serikali ya CCM chini ya uongozi mahiri wa JPM, yalisemwa na Chadema kupitia Tundu Lissu au Mnyika au Mbowe. Hii siyo hoja imara.
Hapa duniani wapo watu ambao wanaweza kusema jambo ukadhani wanasema jambo hilo kwa dhati kumbe wanaamini tofauti kabisa. Mfano Chadema walimsema sana Lowassa kama fisadi kwa zaidi ya miaka 10, lakini hawakuyaamini waliyoyahubiri. Ndiyo maana mwaka 2015 wakampokea Lowassa kuwa mgombea urais. Watanzania wakaihukumu Chadema kwenye uchaguzi Mkuu.

Wabunge wa Chadema wamehubiri sana demokrasia na kufanya maandamano kudai demokrasia pana. Wabunge hao walifunga midomo kuonyesha hisia hizo wakiwa bungeni. Lakini uteuzi wa wagombea ubunge wa bunge la Afrika Mashariki ikadhihirisha kwamba wanachokisema si kile wanachokiamini. Ndani ya Chadema demokrasia ni kwa masilahi mapana ya kikundi cha watu.

Kwahiyo madai ya Chadema na viongozi wa Chadema kudai kwamba yanayotekelezwa kwa sasa wao waliyasema siku nyingi ni hoja isiyo na mashiko.
Jambo lililo mhimu na la msingi ni mwenendo chanya wa viongozi na wanachama wa chama cha siasa kwa jamii. Pili chama cha siasa kinatakiwa kusimamia kinachokiamini. Siyo kuhubiri tu.

Kingine, lugha zinazotumika na baadhi ya viongozi wa Chadema mara nyingi huonyesha upungufu wa maadili na inawafanya watanzania wajiulize, je watu hawa wakipewa madaraka watakuwaje ? Ukosoaji wa Chadema umekuwa wa matusi. Na ukiwa mtukanaji wa Serikali utapewa sifa nyingi sana na hata kuitwa jiniasi- genius. Ni ujinga. Hitler alikuwa genius lakini alikuwa mharibifu pia. Unaweza ukawa genius na unajua sana sheria lakini bila moyo wa uzalendo hautakuwa na faida kwa jamii.

Rais JPM anafanya kazi njema, watanzania tumuunge mkono.

Huu si wakati wa kuzodoana. CCM wakubali tu walitufikisha hapa tulipo na wewe huna tifauti kabisa na kina Lissu maana unawasema CHADEMA wote as if Lissu ni CHADEMA yote. Mbowe kama mwenyekiti ahajasema neon lolote kuhusu mchanga hata katibu mkuu sijamsikia kabisa.

Kina Lowasa na Sumaye najua kabisa hawana ubavu hata kusifia ama kukosoa hizi harakati za Magufuli. Usipende kutuambia serikali ya CCM ndiyo inafanya haya mageuzi huo ni uongo maana hao wabunge wa CCM ni vilaza wa kura za ndiyo ni Bashe peke yake ana uwezo wa kusema chochote kila maana ni mzalendo.

Hizi jitihada ni za Magufuli na serikali yake, bahati mbaya tu kuwa Magufuli ni mwanachama wa CCM lakini najua kabisa CCM mlio wengi hampendi haya yanayoendelea hata huko CDM pia hawayapendi.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
38,634
2,000
Ninaona maandiko mengi yakieleza kwamba hatua nyingi zinazochukuliwa na Serikali ya CCM chini ya uongozi mahiri wa JPM, yalisemwa na Chadema kupitia Tundu Lissu au Mnyika au Mbowe. Hii siyo hoja imara.

Hapa duniani wapo watu ambao wanaweza kusema jambo ukadhani wanasema jambo hilo kwa dhati kumbe wanaamini tofauti kabisa. Mfano Chadema walimsema sana Lowassa kama fisadi kwa zaidi ya miaka 10, lakini hawakuyaamini waliyoyahubiri. Ndiyo maana mwaka 2015 wakampokea Lowassa kuwa mgombea urais. Watanzania wakaihukumu Chadema kwenye uchaguzi Mkuu.

Wabunge wa Chadema wamehubiri sana demokrasia na kufanya maandamano kudai demokrasia pana. Wabunge hao walifunga midomo kuonyesha hisia hizo wakiwa bungeni. Lakini uteuzi wa wagombea ubunge wa bunge la Afrika Mashariki ikadhihirisha kwamba wanachokisema si kile wanachokiamini. Ndani ya Chadema demokrasia ni kwa masilahi mapana ya kikundi cha watu.

Kwahiyo madai ya Chadema na viongozi wa Chadema kudai kwamba yanayotekelezwa kwa sasa wao waliyasema siku nyingi ni hoja isiyo na mashiko.
Jambo lililo mhimu na la msingi ni mwenendo chanya wa viongozi na wanachama wa chama cha siasa kwa jamii. Pili chama cha siasa kinatakiwa kusimamia kinachokiamini. Siyo kuhubiri tu.

Kingine, lugha zinazotumika na baadhi ya viongozi wa Chadema mara nyingi huonyesha upungufu wa maadili na inawafanya watanzania wajiulize, je watu hawa wakipewa madaraka watakuwaje ? Ukosoaji wa Chadema umekuwa wa matusi. Na ukiwa mtukanaji wa Serikali utapewa sifa nyingi sana na hata kuitwa jiniasi- genius. Ni ujinga. Hitler alikuwa genius lakini alikuwa mharibifu pia. Unaweza ukawa genius na unajua sana sheria lakini bila moyo wa uzalendo hautakuwa na faida kwa jamii.

Rais JPM anafanya kazi njema, watanzania tumuunge mkono.
Mkuu Fred Mpendazoe, naunga mkono hoja ya practicing what you preach

P.
 
funza

JF-Expert Member
Sep 5, 2013
7,481
2,000
Mleta mada ni mshamba sana anadhani watanzania hawana kumbukumbu yaani kasahau kuwa vilio juu ya mikataba vipo tokea miaka ya 90 wananchi wanajua Ukweli wote wanafahamu kuwa mkulu ka-copy kilio cha Wapinzani kwa shinikizo la Daud Bashite ambaye yupo na Acacia kwa mbinu zile za blackmail kama kawaida yake, ni mwendo wa kufa kufaana sasa kaamua kula pesa zao akiwaaminisha kuwa atawasaidia kukaa pamoja na kuandaa mikataba mipya wapo Wajanja wengi huko CCM wananufaika na hii pressure ya Acacia ni aina ya Sinema za ajabu zinazotengenezwa Tanzania ambapo mwisho wake ni Aibu kwani wenye nia njema ni wachache sana.
 
zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
13,169
2,000
Mkuu mpendazoe hivi kweli unadiriki kuuliza kma wanaamini walichohubiri???? Hivi wangekuwa hawakiamini wangeendelea kukilalamikia kitu hicho kwa miaka zaidi ya 18 sasa???? Yaani kila hotuba ya KUB kwa wizara ya nishati na madini haikosi kelele juu ya mikataba nyonyaji aaaah we unaona hawaamini????? Wafanyeje uwaamini???

Kipindi wanapitisha muswada mbovu wa gesi na mafuta ni wapinzani pekee ndo walitoka nje huku ccm wakibaki kuupitisha na jana wameumbuka baada ya mwenyekiti wao kuwaambia wakarekebishe walichopitisha maana kina udhaifu ule ule uliolalamikiwa na upinzani sawa hapo nani haishi anachokiamini je ni ccm ama chadema????

2. Bunge la katiba. Kwenye rasimu ya warioba kulikuwa na kipengele kinacholazimu serikali kuleta mikataba bungeni ili iwe wazi kwa mijadala ya kitaifa kabla haijaanza kutumika hawa hawa wapinzani waliopiga kelele kwa miongo miwili kabla ya bunge la katiba walisupport kipengele hili ila hiko chama ulipo walikifuta sasa ni nani hapo ameishi alichohubiri......chadema ama chama chako.

Unanishangaza sana mkuu..... hiko chama chako je kinaamini kilichohubiri kuwa ni cha kizalendo je kimeweza kuishi maneno yake na wakati kimetufikisha hapa??? Na swali langu je miaka yote chadema imepigia kelele masuala haya ya mikataba chama chalo walikuwa wanajibu nini?????

Anyway umeongelea swala la lowasa kinachochekesha wwe ni mmojawao waliomsafisha lowasa kwa kuandika makala kwenye raia mwena isemayo UTUSAMEHE LOWASA..... sasa iweje ulimsafisha na ukaomba akusamehe kwa kumsingiza na ukaandika hoja nzito sana eti leo unakana andiko lako ??? Ssa tukueleweje?? Ukiwa ccm ooh lowasa fisadi chadema ooh lowasa msafi sahvi tena ooh lowasa fisadi ssa 2020 ukirudi tena upinzani utasemaje???

Mkuu mambo mengine ni heri ukae kimya tu lakini kuhoji nani aliamini alichohubiri naona chama chako kina kesi nyingi za kujibu
 
Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
14,029
2,000
Jambo lolote likipigiwa kelele na upinzani ukitaka upinzani walikane, serikali ilitekeleze, likitekelezwa tu upinzani wanalikana.. Kikubwa JPM aendeshe kwa mujibu wa ILANI ya CCM.. Na yote yapo wazi katika ilani yetu
 
The Businessman

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
7,412
2,000
Kama wewe mwenyewe hujielewi kamwe huwezi kumuelewa Tundu Lisu alichoandika!

Halafu si lazima wote tumuunge mkono Rais.

Kuwa mwanaccm ni nusu ya uchizi na ndio maana TL anapenda Kuwait's "maccm".
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,663
2,000
Ni kikumbuka Mpendazoe alivyokuwa na uwezo wakati akiwa Mbunge wa CCM kabla ya kuuacha na kujiunga Chadema sipati picha ya huyu Mpendazoe wa kizazi hiki.

Hivi kumbe njaa iko hivi? madhara yake kumbe yanaweza utafuna ubongo kuliko hata saratani ya kichwa?

Mzee mwenzangu Mpendazoe, hebu tunza heshima yako na ya family yako kwa kutoendekeza njaa kwa kiasi hicho.
 
MeinKempf

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
11,107
2,000
Upinzani wengi hapa Tanzania ni "wasaka tone wa nguru wa paona" tu
matumbo yao yanaongoza ufikili waon, sasa yakipewa utamu kidogo baasi
kwisha kazi.
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
9,216
2,000
Ninaona maandiko mengi yakieleza kwamba hatua nyingi zinazochukuliwa na Serikali ya CCM chini ya uongozi mahiri wa JPM, yalisemwa na Chadema kupitia Tundu Lissu au Mnyika au Mbowe. Hii siyo hoja imara.

Hapa duniani wapo watu ambao wanaweza kusema jambo ukadhani wanasema jambo hilo kwa dhati kumbe wanaamini tofauti kabisa. Mfano Chadema walimsema sana Lowassa kama fisadi kwa zaidi ya miaka 10, lakini hawakuyaamini waliyoyahubiri. Ndiyo maana mwaka 2015 wakampokea Lowassa kuwa mgombea urais. Watanzania wakaihukumu Chadema kwenye uchaguzi Mkuu.

Wabunge wa Chadema wamehubiri sana demokrasia na kufanya maandamano kudai demokrasia pana. Wabunge hao walifunga midomo kuonyesha hisia hizo wakiwa bungeni. Lakini uteuzi wa wagombea ubunge wa bunge la Afrika Mashariki ikadhihirisha kwamba wanachokisema si kile wanachokiamini. Ndani ya Chadema demokrasia ni kwa masilahi mapana ya kikundi cha watu.

Kwahiyo madai ya Chadema na viongozi wa Chadema kudai kwamba yanayotekelezwa kwa sasa wao waliyasema siku nyingi ni hoja isiyo na mashiko.
Jambo lililo mhimu na la msingi ni mwenendo chanya wa viongozi na wanachama wa chama cha siasa kwa jamii. Pili chama cha siasa kinatakiwa kusimamia kinachokiamini. Siyo kuhubiri tu.

Kingine, lugha zinazotumika na baadhi ya viongozi wa Chadema mara nyingi huonyesha upungufu wa maadili na inawafanya watanzania wajiulize, je watu hawa wakipewa madaraka watakuwaje ? Ukosoaji wa Chadema umekuwa wa matusi. Na ukiwa mtukanaji wa Serikali utapewa sifa nyingi sana na hata kuitwa jiniasi- genius. Ni ujinga. Hitler alikuwa genius lakini alikuwa mharibifu pia. Unaweza ukawa genius na unajua sana sheria lakini bila moyo wa uzalendo hautakuwa na faida kwa jamii.

Rais JPM anafanya kazi njema, watanzania tumuunge mkono.
Neno uzalendo ni wimbo tu ambao ccm imekuwa ikiuimba kwa sauti na matendo tofauti. Hata Ben na Kikwete walipokuwa wanauza madini yetu kwa bei ya kutupwa waliimba uzalendo.

Zimwi baya la nchi hii ni ccm
 
tamuuuuu

JF-Expert Member
Mar 10, 2014
14,553
2,000
Tume huru idaiwe mapema ccm itoke vinginevyo watanzania mtapata tabu sana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom