Je,walichokifanya UDOM ni sahihi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je,walichokifanya UDOM ni sahihi?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by a2_future, May 1, 2011.

 1. a

  a2_future Member

  #1
  May 1, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mimi naomba kuhoji kuhusu suala ya management ya UDOM kuwarudisha nyumbani wanafunzi wa kitivo cha mawasiliano na elimu angavu (Informatics & Virtual Education), kisa walikua wanadai pesa zao za mahitaji maalum ya kitivo (special faculty requirements).

  Halafu kwenye vyombo vya habari wanasema wanafunzi wanagomea 'laptop' ili wanafunzi waonekane hawana logic, wakati hizo pesa zimeliwa na wao.

  Wadau nisaidieni kama ni haki kwa mtanzania kufukuzwa chuo kwa kudai haki yake eti amehatarisha amani ya chuo, au kuna wengine ni watanzania zaidi kuliko wenzao?
   
 2. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,060
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  Tena ndugu yangu wanafunzi hawa wamepewa kaheshima kadogo maana mafisadi hawa wakishafuja huita media na kutapika utumbo wao na kudai wanafunzi wamefukuzwa kwa sababu ,ni wahuni,walevi,wavuta bangi n.k,kwa vile wao wameshikilia mpini na wanafunzi wamekamata kwenye makali,basi mambo hubaki vivyo hvyo...nashauri hata hao waliobaki wadai kurudishwa kwa wenzao kama na wao watafukuzwa basi wafukuzwe chuo kizima kwani ajabu nini
   
 3. p

  papachu Member

  #3
  May 2, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unajua cha kushangaza uongozi wa chuo cha elimu ya mawasilano na elimu angavu kwa kusema uongo eti wanachuo hao walikuwa tanadai laptop kitu ambacho si kweli walichokuwa wanadai wanafunzi ni kupinga kupatiwa 50,000 kwani kiasi hicho cha fedha akikizi mahitaji ya special faculty requirements.kama kunauwezekana iundwe tume ije ifanye uchunguzi chuoni hapo
   
 4. Planner

  Planner JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2011
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 296
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Mi naomba nitoe angalizo kwenu wana UDOM,now days kuna baadhi ya waandishi nao ni vibaraka wa mafisadi.kwasababu hii ni vizuri mkatumia njia za kimawasiliano kutuma habari sahihi kwa vyombo makini pale linapojiri jambo linaloathiri ustawi wenu wa kitaaluma.miwaacha wanahabari wajiandikie watakavyo sometime si wote wanaoandika uhalisia.kueni na mifumo ya kutupia habari zenu kwenye vyombo makini zinapojiri ili wale wachakachuaji wa habari waumubuke na utumbo wao.lengo ni kuliita chepe kwa jina lake ili ufumbuzi upatikane..sio huku tunaambiwa mnadai laptop kumbe suala liko kivingine.
   
Loading...