FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 37,898
- 43,802
Inasemekana mataifa ya kikoloni kama Uingereza,Ujerumani, Ufaransa, Ubelgiji, Uitaliano na Ureno walijikatia vitalu katika Ardhi ya Afrika mithili ya watoto wakikatiana keki mnamo mwaka 1884 katika mkutano uliopewa jina la 'Berlin confrence' huko ujerumani. Kabala ya hapo hapakuwa na mipaka katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara, sana sana ilikuwa ni mipaka ya kufikirika baina ya 'chieftains' na 'kingdoms' mbali mbali. Je, bila kumegwa huko na wakoloni, leo hii tungekuwa taifa moja?, na je, tungekuwa ni 3rd world country? Na je, tungepewa kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa? Je, tungekuwa taifa kubwa na lenye nguvu kama nchi zingine zenye eneo kubwa kijiografia,mfano Russia, China, India, USA?