Je, wako wapi wakongwe hawa?

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
Miongoni mwa sintofahamu inayoendelea ni kutojulikana alipo aliyekuwa staa wa Bongo Movies, Mikalla aliyeng’ara kwenye Filamu ya The Lost Twins akitumia jina la Anita; filamu iliyoandaliwa na aliyekuwa kinara wa tasnia hiyo, marehemu Steven Kanumba chini ya Kampuni ya Mtitu First Game Quality.

Sintofahamu hiyo imesababisha hofu kutanda miongoni mwa mashabiki juu ya ni wapi walipo baadhi ya mastaa wao ambao waling’ara mno, lakini sasa hawajulikani walipo huku wengine wakidaiwa hali zao ni mbaya kimaisha.

Hata hivyo, kama ilivyo desturi ya Gazeti la IJUMAA kudili na mastaa ndani na nje ya Bongo linakuletea ripoti nzito ya nani yupo wapi na anafanya nini?

MIKALLA
Ni kweli Mikalla alikuwa ni mwigizaji mkali kuanzia kipaji hadi uzuri ambapo wengi waliomshuhudia katikati ya miaka ya 2010 walikiri kwamba atakuja kuwa staa mkubwa wa Bongo Movies, lakini mambo yakawa kinyume.

Mbali na Filamu ya The Lost Twins, Mikalla alifanya vizuri mno kwenye Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu chini ya Kampuni ya Tuesday Kihangala ambayo mkurugenzi wake ni Jumanne Kihangala almaarufu Mr Chuzi, akitumia jina la Lucky likiwa ni jina la Kingereza la jina lake halisi la Bahati.

Kuna madai mazito kwenye mitandao ambayo yanadai kwamba, Mikalla alifariki dunia mwaka 2015 huko jijini London nchini Uingereza kwa ajali ya gari, lakini hakuna mwenye uthibitisho huku baadhi ya watu wakisema si kweli, bali yupo na anaishi maeneo ya Mbezi ya Kimara jijini Dar, jambo ambalo haku aliyejitokeza na kulithibitisha hivyo kama kuna mtu anajua lolote awasiliane na gazeti hili.

JINI KABULA
Huyu alikuwa staa wa Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu chini ya Mr Chuzi na mbali ya hapo alikuwa Miss Kurasini jijini Dar kabla ya kujikita kwenye muziki wa Bongo Fleva chini ya Kundi la Scorpions likiwa na memba wenzake, Baby Madaha na Isabella Mpanda.

Mwaka 2017, Jini Kabula alipitia changamoto ya kiafya ambapo alikumbana na janga kubwa la kuugua ugonjwa uliotajwa kama ‘kichaa’ ambapo baada ya kupona aliliambia IJUMAA kwamba, mapito aliyopitia anaona ni kama alikuwa kuzimu kisha kurejea duniani.

Baada ya hapo Jini Kabula alikwenda jijini Mwanza kupumzika kwa kaka yake kisha atarejea tena kwenye sanaa.

ANITA WA MATONYA
Anita wa Matonya anatajwa kuwa miongoni mwa ma-video vixen wakali wa kitambo hicho akitumika vyema kwenye Video ya Anita ya msanii Matonya kisha video ya msanii MB Dogy.

Wengi walimtabiria Anita kwamba angekuwa bonge la staa kwenye sanaa Bongo, lakini mwenyewe anasema yupo, lakini kuna mambo yalimuweka kando ya sanaa ikiwemo familia yake iliyoshika Dini ya Kiislam kisha alijikita kwenye biashara na kuachana na mambo ya kuuza sura.

Mwenyewe anasema kwa sasa yupo tayari kurudi kwenye sanaa na mashabiki wake wakae tayari kumuona tena na sasa amekua mkubwa, lakini bado familia inamuwekea ngumu.

DUDU BAYA
Miongoni mwa wakongwe waliowahi kufanya vizuri kunako Bongo Fleva yupo pia Dudu Baya. Mkali wa Wimbo wa Mpenzi Bubu na Mwanangu Huna Nidhamu.

Dudu Baya amekuwa akiibua sitofahamu kama ilivyo kwa sasa ambapo mashabiki wake wengi wanajiuliza yupo wapi na kuzua hofu kwa kuwa anatajwa kuwa mmoja wa wasanii wenye bifu nyingi Bongo?

Mwaka 2020 alipotea kwa takriban siku 15 kiasi cha binti yake kuibuka kwenye vyombo vya habari akiomba msaada wa kupatikana kwa baba yake kabla ya kupatikana mkoani Geita na sasa taarifa zinasema yupo nyumbani kwao jijini Mwanza, lakini hali ya kimaisha si shwari.

VENGU
Vengu alikuwa mmoja wa mastaa wakubwa wa komedi akitumikia Kundi la Orijono Komedi ambalo kwa sasa limerudi hewani, lakini bado haonekana yapata miaka zaidi ya kumi sasa.

Vengu alianza kuugua mwaka 2009. Mwaka 2011 alizidiwa ambapo alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar. Rais wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Mrisho Kikwete alikwenda kumjulia hali akiwa hospitalini hapo.

Baada ya hali yake kutotengemaa, alipelekwa kwenye Hospitali ya Apollo nchini India ambako alipatiwa matibabu na kurejeshwa nchini akiendelea kuuguzwa na familia ambapo familia huwa haipendim kueleza anaendeleaje zaidi ya uwepo wa taarifa kwamba yupo nyumbani kwao Ifakara mkoani Morogoro.

MR CHUZI
Mr Chuz anatajwa kuwa mmoja wa waigizaji walioleta mapinduzi ya tamthilia za Kibongo baada ya kuanzisha Jumba la Dhahabu akiwa mkurugenzi wake.

Mbali na kuwa mwigizaji mkali, pia alikuwa dairekta aliyeshiriki kutengeneza vipaji vingi vya waigizaji kama Jini Kabula, Joan Matovolwa, Jack wa Chuzi na wengine wengi.

Hata hivyo, umepita muda mrefu hajasikika, lakini taarifa za Gazeti la IJUMAA zinaeleza kwamba anaendelea na sanaa akiwa ameweka makazi nyumbani kwake, Makongo jijini Dar na mkoani Maorogoro.

MZEE MAGARI
Alikuwa mzee mmoja aliyepamba mno Bongo Movies akiigiza vizuri kwenye uhusika wa baba mkorofi asiyependa uzembe ndani ya familia.

Hata hivyo, baada ya kung’ara kwenye filamu nyingi alitimkia nchini Marekani na huku anaendeleza sanaa yake, japokuwa haivumi Bongo kama zamani.

FRANK MWIKONGI

Utampenda Frank Mwikongi pale alipoigiza kwenye tamthiliya na marehemu Kanumba, Ray na wengine, lakini ghafla akapotea.

Frank yupo nchini Marekani, ana mishe nyingi za kimaisha hivyo haifahamiki kama atarejea kwenye sanaa.

Mara ya Mwisho ilikuwa mwaka 2015 ambapo Frank alitinga Bongo na kuchukua fomu ya kugombea ubunge kwenye Jimbo la Segerea jijini Dar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, lakini hakufanikiwa.

SYLVIA SHALLY
Mwanzoni mwa miaka ya 2010, ukimuacha Wema Sepetu, Irene Uwoya, Jokate Mwegelo, Lisa Jensen, Aunt Ezekiel na wengine, mrembo Slvia Shally alikuwa ni moto wa kuotea mbali.

Umaarufu wa Shally ulitokana na kushirikishi Miss Tanzania 2010 na kuibuka kwenye tano bora AKIWA Mshindi wa Miss Ilala kisha akatumbukia kwenye tasnia ya filamu akiwa mikononi mwa Kanumba.

Baadaye alikuwa maarufu zaidi baada ya kubainika kwamba yupo kwenye penzi matata na Kanumba.

Hata hivyo, kuondoka kwa Kanumba aliyetangulia mbele ya haki siku ile ya Aprili 7, 2012 kuliwapoteza wengi na miongoni mwao ni Shally.

Taarifa mpya ni kwamba, kwa sasa amejikita kwenye biashara akiwa ameolewa na ni mama wa familia.

LISA JENSEN
Alifanya vizuri kwenye Miss Tanzania 2006 akiingia tano bora kisha alijikita kwenye filamu na kina Jokate na kuwa mto wa kuotea mbali.

Mara ya mwisho aliuza sura kwenye video ya Mawazo ya Diamond na baada ya hapo akapotea huku kukiwa na taarifa kuwa aliolewa nje ya nchi na sasa ni mama wa familia.

MIRIAM GERALD
Miriam alikuwa Miss Tanzania 2009 na Miss Redds ambapo alipata umaarufu mkubwa baada ya ushindi na kujikita kwenye filamu za Kibongo.

Kipo kisa kimoja maarufu cha Miriam ambapo mwaka 2009 alishipandishwa kizimbani pamoja na mtu mwingine wa kiume anayesadikiwa kuwa boy friend wake kwa tuhuma za kupiga na kujeruhi ambapo wote walishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kutupwa lupango.

Baada ya hapo, Miriam alirejea nyumbani kwao Mwanza na hakusikika tena.

JACK WA CHUZI
Jina lake halisi ni Jacqueline Pentzel, lakini alipewa jina la Jack wa Chuzi kwa sababu Mr Chuzi ndiye aliyemtoa kiugizaji baada ya kuanzia kwenye u-misi ambako hakufurukuta.

Unakumbuka lile Kundi la Jarowe? Yaani Jack, Rose Ndauka na Wema? Basi hizo ndizo nyakati bora za Jack wa Chuzi kabla ya kuolewa na sasa ni mama wa familia.

JESCA CHARLES
Jesca alikuwa mmoja wa waimbaji matata muziki wa Dansi akifanya vizuri alipokuwa Twanga pepeta. Alishiriki utunzi, uimbaji kwenye safu ya mbele na kucheza, lakini ghafla akapotea.

Kama ulikuwa unajiuliza yupo wapi, basi Musa Mateja ni Mwandishi na Mtangazaji wa Global Redio ambaye anasema kwa sasa, Jesca ameolewa na mzungu na anaishi Uingereza, muziki alishaupiga teke.

LILIAN INTERNET/JANETH ISINIKA
Kama ilivyo kwa Jesca Charles, wanamuziki wengine wa Twanga Pepeta, Lilian Internet na Janeth Isinika, nao wameolewa na kuweka mambo ya muziki kando.

Kuna wakati Lilian Internet alitaka kurejea ulingoni, lakini mambo ya kifamilia yakambana, akashindwa.

NAKAAYA SUMARI
Ni dada wa Miss Tanzania 2005, Nancy Sumari ambaye alitikisa kwenye Bongo Fleva na Ngoma ya Mr Politician. Nakaaya ambaye alikuwa akiwakilisha Arusha kwenye gemu, alikuwa miongoni mwa marapa wa kike wenye kujiamini hasa baada ya kuachia ngoma hiyo ambayo ilikuwa ikiegemea kwenye siasa.

Kama ilivyo kwa wanawake wengine naye mambo ya familia yalimbana na sasa anatunza familia yake jijini Arusha.

REHEMA/VAI/SABRINA/BABY CANDY/NATASHA
Mbali na Anita wa Matonya, Binti Kiziwi na wengine, miongoni mwa ma-video vixen waliotisha na kutabiriwa kuja kuwa mastaa wakubwa Bongo ni Rehema Fabian (video ya Pasha), Vai wa Ukweli, Sabrina Hakunaga (Video ya Hakunaga ya Suma Lee), Baby Candy (Video ya Dully Sykes) na Natasha (Moyo Wangu ya Diamond).

Wengi wao kama Rehema na Sabrina wamekimbilia China na wengine wanajihusisha na michongo mingine jijini Dar.

WASANII KIBAO BONGO FLEVA
Wapo wasanii kibao wa Bongo Fleva ambao wanaumiza vichwa mashabiki wao kama, Joslini (Niite Basi Mpenzi), Bob Junior (Oyoyo), Rado (Usiulize), Rah P (Hayakuhusu), Dataz (Tunatawala), Besta (Kati Yetu) Mandojo na Domokaya (Wanoknok), Enika (Baridi Kama Hii), Ray C (Na Wewe Milele), PNC (Mbona), Mr Nice (Kikulacho), Hawa (Nitarejea), Kali P (Imekaa Vibaya), Noorah (Ice Cream), Caz T (Nakuhitaji), Maunda Zorro (Nataka Niwe Wako), Bob Rudala (Nimekuchagua Wewe), Hafsa Kazinja (Pressure) na wengine wengi; baadhi yao muziki umewashinda wapo choka mbaya huko mikoani na wengine wanajikongoja kurudi kwenye gemu.
 
Sijamona Mike T(Mnyalu)-
"Kamaa Mike T ningekuwa staa,"
Pia Mad Ice
 
Back
Top Bottom