Mr George Francis
JF-Expert Member
- Jun 27, 2022
- 274
- 486
UCHAWI ni matumizi ya nguvu zisizo za kawaida zinazotumika kuwadhuru wengine kwa namna isiyo ya kawaida.
Uchawi unajumuisha mazingaombwe, kuloga, matumizi ya vifaa vya uchawi, matendo ya nguvu za giza au umiliki wa maarifa ya siri yasiyo ya kawaida.
Uchawi sio dhana mpya katika jamii zetu bali ni imani ambazo zipo tangu zamani hata kabla ya ujio wa Yesu au Nabii Issa kama anavyotambulika kwa waumini wa dini tofauti.
Mfano: KUTOKA 7:11 neno linasema
"Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na WACHAWI; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao."
YOSHUA 13: 22 Neno linasema
"Balaamu naye, huyo mwana wa Beori, huyo MCHAWI, wana wa Israeli walimwua kwa upanga kati ya hao wengine waliowaua."
Lakini pia hata baada ya ujio wa Yesu wachawi walikuwepo pia.
Mfano: Simoni aliyekuwa akifanya uchawi katika kanisa la Wasamaria.
MATENDO YA MITUME 8:9-11 neno linasema
"Na mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa.
Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu.
Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake."
Mchawi mwingine aliitwa Bar_Yesu ambaye tunamuona katika
MATENDO YA MITUME 13:6-8
Neno linasema
"Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu;
Mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu.
Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani."
Maandiko haya yanadhihilisha kuwa uchawi upo tangu na tangu enzi hizo mpaka sasa katika kizazi hiki lakini Uchawi ni chukizo kwa Mwenyezi MUNGU na hata sheria za nchi zinakataza watu kujihusisha na vitendo vya uchawi.
Kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha Sheria ya Uchawi, Sura ya 18, Kama ilivyofanyiwa maboresho mwaka 2023 Uchawi ni kosa kisheria.
Kifungu hicho kinasema kwamba
(a). Mtu yoyote ambaye kwa kauli zake au matendo yake anajionesha kuwa ana nguvu za kichwani,
(b). Mtu yoyote anayetengeneza, anayetumia, anayemikiki au anayejionesha kuwa anamiliki zana za kichawi,
(c). Mtu yeyote anayempa mtu mwingine zana yoyote ya kichawi,
(d). Mtu yeyote anayemshauri mtu mwingine kutumia uchawi au zana ya kichawi,
(e). Mtu yeyote anayetishia kutumia uchawi au zana ya kichawi dhidi ya mtu yeyote au mali yeyote
basi mtu huyo anatenda kosa chini ya Sheria Ya Uchawi.
Kifungu cha 5 cha Sheria Ya Uchawi yaani The Witchcraft Act, [Cap 18 R.E. 2023] kinasema kwamba
• Mtu yeyote anayetenda kosa chini ya Sheria hii kwa lengo la kutaka kusababisha kifo, ugonjwa, jeraha au balaa kwa jamii fulani, kundi fulani la watu, mtu fulani au mnyama au kusababisha uharibifu wa mali yoyote adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka (7) saba.
•Mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria ya Uchawi bila kuwa na lengo la kusababisha madhara yaliyoelezwa kwenye kifungu cha 5(1) anapaswa kuadhibiwa kulipa faini isiyopungua shilingi laki moja za kitanzania au kifungo kisichopungua miaka (5) mitano.
Kwa mujibu wa sheria za nchi yetu uchawi ni kosa linalotambulika kisheria. Hivyo mtu yeyote anayetenda vitendo vya uchawi anaweza kushitakiwa na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria.
Kama una uthibitisho wa dhahiri kuhusiana na kutendewa vitendo uchawi usiogope kupeleka kesi Mahakamani eti kwakuwa umewahi kusikia kwamba selikari haiamini uchawi.
Endelea kunifollow ili tuendelee kujifunza hapa kuhusu mambo mbalimbali ya kisheria na maisha mengine kwa ujumla.
#No_learnig_No_earning
So We Have To Learn.
Content By Mr George Francis