Je wajua jumuiya ya africa mashariki ni mpango kabambe wa kenya kunyonya rasilimali za tanzania!?

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,810
18,543
Wengi wetu hatujui kilichopo nyuma ya pazia la Jumuiya ya Africa Mashariki. Laiti tungejua tusingeridhia kuuza nchi yetu kwa wageni.

Huu ni mpango mahsusi wa wakenya ambao ndio nchi yenye uchumi mkubwa zaidi Africa Mashariki. Wakenya walishapiga mahesabu na kuona faida kubwa watakazozipata katika Jumuiya hii. Hii inatokana na ukweli kwamba mnyonge anaposhindana na mwenye nguvu mwenye nguvu atashinda, labda jambo lisilo la kawaida litokee.

Wakenya katika mahesabu yao wanaona haya mambo yafuatayo:
1.Ardhi; unaona tayari wanapora ardhi vibaya huko Arusha. Ardhi kule Kenya imemilikiwa na walowezi wachache kutoka UK, nk watu wengi ni manamba tu. Nimewaona wengi tu kule Kilombero na Matombo tayari wanapita na magari yenye namba za Kenya
2.Utalii; wameanza mpango wa kujenga kiwanja cha ndege cha kimataifa kilometa 50 tu kutoka KIA kwa ajili ya kukamua Kilimanjaro na kanda ya kaskazini na walisema waziwazi jambo hili na kuna zaidi ya kusema hapa.
3.Soko la bidhaa zao, kumbuka wana viwanda vingi kuliko nchi zilizobaki kwa pamoja
4.Malighafi kwa ajili ya viwanda vyao: Tanzania tutapoteza thamani ya mazao yetu kwa kuuza mazao ghafi kwa bei rahisi
5.Usafiri wa anga: tayari bao lishapigwa hapa na wameshilikia hisa hata katika Precision Air na mpango ni kuua Aviation industry ya Tz
6.Soko la ajira, na hapa tayari walishafanikiwa sana mapema tu angalia jinsi UDOM palivyojaa wahadhiri wakenya! Mtanzania si rahisi hata kidogo kuajiriwa Kenya. kumbuka hata Mkalenjini wa huko Kenya inahitaji bahati kubwa kupata ajira ya kufagia ofisi ndio m-tz!
7.Madini: una habari wakenya walishanunua vinu vya kuyeyusha dhahabu wakati hawachimbi dhahabu?!
8.Umoja wa sarafu: hii ndiyo njia nzuri ya kutengeneza syphon na uchumi kumwagikia kwao kiulaini

Bila kujidanganya na kwa uhakika hebu tutaje kama wanavyotaja wakenya faida za hii jumuiya kwetu:
1.
2.
3.

Kumbuka! kwa sababu ni kweli wengi wa wakenya wanaoshiriki katika kujenga mikataba na muundo wa EAC wanaujuzi wa kiuchumi zaidi ya nchii zilizobakia, basi si ajabu wala uongo kwamba wanahakikisha kwamba kila wanaloiingiza kwenye Jumuiya linawafaidisha wao kwanza!

Tilia maanani kwamba: viongozi wa Kitanzania walivyo carefree na wazembe wakubwa wasiojali kama wanayoyafanya yanawafaidisha wananchi ama laa. Na pia usisahau kwamba Wa-tz wengi wanaugonjwa wa kuwapaparikia wageni na kukubaliana na kila kitu wanachosema.

Na Wakenya wanalijua hili vizuri sana!

Sasa sisi Watanzania tujaribu kwa dhati bila kujisemea tu kwa ushabiki ni kwa vipi tunaona moja kwa moja faida za hii jumuiya kwetu. Tuache ujinga wa kusema tukiingia kwenye jumuiya ndio tutapata akili, kwani tumepata akili kwa kunyonywa na wakoloni mamboleo zaidi ya miaka 50 tokea kabla ya uhuru hadi leo?

Nimeishi na wakenya Tz na kule kwao. Wanaona Tz kama shamba la kuvuna na wanaomba Mungu ni lini nchi hizi zitaunganishwa tu, ni lini sarafu itakuwa 1

Kati ya yanayowavutia wakenya ni upole na ustaarabu wa Watz(pengine kwa sababu ya ujinga na umaskini wa wa-tz?).

Utakuta Mkenya anakuja leo Tz na kuanza kuwatukana watu na kuwaambia nyie hamna lolote, lakini la ajabu watu wanawaangalia tu. MImi binafsi wananijua na wanasema wewe ni Mtz tofauti.

Tafadhali Watz wenzangu tuishi kama tupo Tanzania. Hii ni nchi yetu. We must feel proud of it la sivyo tutauzwa kama bidhaa!
 
I call it "EAST African Commotion aka Confusion"; it is not only about money thirsty Kenya, what about power thirsty Uganda, blood avengers Rwanda and its sister country Burundi and then Southern Sudan? Think about it TANZANIANS, where do we fit; what shall we gain but loose a lot? We can hardly manage our own countries and then we start some FEDERATION of five states, I am sure DRC is in too? Or it will be in. Hebu angalia Kenya na Uganda wanatoana macho sababu ya migingo...kisiwa kidogo na wanataka EAC to help solve such a minor border issue? How will we manage all these countries with different backgrounds? We are so naive
 
Kulikuwa na kura ya maoni au something similar to that, na kama nakumbuka vizuri wabongo wa mipakani waliikataa.. Sasa kwa watu wenye akili ile ilikuwa ishara kubwa sana kuwa hiyo kitu haifai, lkn kwa watawala hawa wasiojali tunalo. Mi huwa nauliza tutaungana na malawi, zambia na msumbiji pia? Au wao siyo 'majirani zetu wazuri?!'
 
Back
Top Bottom