Je, wajua hili kuhusu mainjinia wa meli ya Titanic?

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Inawezekana ukawa unajua ila si mbaya tukumbushane kidogo. Katika maisha wenzetu wazungu wana kitu wanaita Dedication na Commitment. Wanaheshimu sana mambo hayo.

Nadhani umesoma,umesikia habari nyingu kuhusiana na meli kubwa kabisa iliyopata kuzama miaka hiyo al maarufu kwa jina la Titanic. Tamka /Taitanik/ good.

Basi wakati meli hiyo inazama taratibu huko katika kina cha bahari. Mainjia wa meli hiyo hawakuwa wakihangaika kugombea maboya au kukimbilia kwenye mitumbwi ya uokozi.

Wao walikuwa busy kuhakikisha umeme upo/ taa zinawaka ili abiria waweze kujiokoa.na hatimaye wao walifariki wakiwa katika tukio hilo la kishujaa la kuhakikisha abiria wao wanaokoka.

Hii ndiyo aina ya uongozi tunayotaka tuwe nayo. Dedication na commitment kwa kazi na watu wako. Hawa walikuwa mashujaa wa aina yake. Hakuna hata Injia mmoja aliyejiokoa katika meli ile. Walijitolea kufa kwa ajili ya watu wengine.

Haya nawe sema unalolijua kuongezea matukio haya ya mashujaa wenzetu huko Ulimwenguni.

Screenshot_20191004-163359~2.png
 
Kuna yule padre aliyegoma kuondoka, kuna mzee alibadilishana boya kwa jacket ili afe kama gentleman. Kuna group la waimbaji waliendelea kuimba mpaka mwisho. Wakati mafataki yanafyatuliwa meli iliyokuwa karibu ikadhani Titanic walikuwa wanafanya party. Wakati huo mfumo wa mawasiliano ulikuwa haufanyi kazi usiku baada ya ajali tribunal ikaamua meli ziweze kuwasiliana na usiku. Mengine waongeze
 
Titanic bhana kuzama kwake kuna maajabu na mambo mengi yaliyoshangaza likiwemo hilo...pia kuna waimbaji waliokuwa wanapiga violin na kuimba hawa hata hawakujali hekaheka zote zile waliendelea kutoa burudani kama kawaida,pia captain mkuu nae aligoma kuondoka ingawa opportunity ilikuwepo alikaza kukaa kwenye chumba chake cha kuongozea meli mpaka mauti ilipomkuta
 
Meli hiyo ya Uingereza ilizama mwaka 1912 baadaya kugonga iceberg wakati wa safari yake ya kwanza kutoka Uingereza kwenda Marekani. Ilikuwa na watu zaidi ya 2,200 - kati yao zaidi ya 1,500 walifariki. Ilikuwa meli kubwa kuliko zote wakati huo.
 
nazani kizazi cha zamani nitofauti sana na cha leo. siku hizi ni ngumu kijakazi kufa kwa ajili ya Mkuu wake hata mume hayupo tayari kufa kwa ajili ya mke wake. watu wa sasa hawana ujasiri wa kujiua kujichoma moto kuonesha msimamo wao dhidi ya jambo fulani. utandawazi umeharibu uhalisia wa Utu
 
Pengine kwa habari za chini ya kapeti na vitabu kadhaa visivyopatikana mtaani ni kwamba ile issue ilikuwa planned from early.
White Srar Line ndo waliotengeneza meli. Kati ya vitu nilivowahi fatilia sana ni Titanic na Freemason mpaka nilipumzika kusoma stories zake. Mwaka wa pili sasa miaka mingine miwili ntarudia
 
Yule mwalimu anaitwa Rwakahere aliyekuwa anaokoa wanafunzi wake watatu hadi nchi kavu akaamua kumrudia wanne nguvu zikamuishia wakafa naye bado anakumbukwa?
Ilianzishwa nishani yake iliishia wapi?
Kastory kazuli ako
 
GuDume Mkuu umechokoza halafu ukakimbia maana hukumalizia km ni ile Filamu ya James Cameron au ni kile kitabu cha A NIght to Remember kilichoelezea kuzama kwa Meli kubwa Titanic cha mwaka 1955 kilichoakusanya True story ya watu 63 waliopona ajalini
tukiachana na filamu ya James Cameroun mambo halisi ni kuwa
  1. chnzo cha ajali ni mtu mmoja kulazimisha Captain Smith kuongeza mwendo wa Meli isivyo kawaida wakati huo ikikmbia kilomita 39 kwa lisaa moja
    Who is to blame for the sinking of the Titanic?
    It was Bruce Ismay's fault
    To meet this schedule the Titanic could not afford to slow down. It is believed that Ismay put pressure on Captain Smith to maintain the speed of the ship.Speed‎: ‎Cruising: 21 kn (39 km/h; 24 mph). Max:
  2. Ilizama chini ya Bahari km kilomita 4 How far down is the Titanic?
    he wreck of the RMS Titanic lies at a depth of about 12,500 feet (3.8 km; 2.37 mi), about 370 miles (600 km) south-southeast off the coast of Newfoundland.
  3. Mengine yapo kwenye vitabu na search eng.[/QUOTE]
 
Elezea hii kwa mapana ni story yenye mafundisho muhimu.
Yule mwalimu anaitwa Rwakahere aliyekuwa anaokoa wanafunzi wake watatu hadi nchi kavu akaamua kumrudia wanne nguvu zikamuishia wakafa naye bado anakumbukwa?
Ilianzishwa nishani yake iliishia wapi?
 
Elezea hii kwa mapana ni story yenye mafundisho muhimu.
Ni hapo Kigamboni Dar either ilikuwa pantoon au Boat ilikuwa inazama.Ikiwa na watu na baadhi ya wanafunzi.
Kulikuwa na mwalimu mmoja mkerewe.
kwa jina la Rwakahere alikuwa na wanafunzi wake.
Wakerewe ni wataalamu wa kuogelea aliokoa watatu alivyokwenda kuokoa wanne wakati anamleta nchi kavu akaishiwa nguvu wakafa naye.
Ikaonekana kuwe na nishani ya Rwakahere yaani mwalim aliyefanya jambo la ujasiri sijui iliishia wapi?
Wakati huo nilikuwa mdogo ila nakumbuka ila nimeona niweke wazi kama kuna wahenga watuambie ukweli.
Nimejaribu ku-goggle sijaona kitu wakati ule hakukuwa na goggle miaka ya middle 80's
 
Back
Top Bottom