Je, wajua asili ya jina Afrika?

Je, wajua asili ya jina Afrika?

Hahahaa tulia uanduke kitu kinachoeleweka mkuu[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
AFRIKA na ukisema Afikaaa alafu tia swaga ya kipare, ikimaanisha amesha fika sehem husika hapo haileti maana?😵😵😵😵😵
 
Huwa najiuliza kwa nini kila kitu kinacho tuhusu watanzania na Waafrika kwa ujumlao utasikia kagundua mzungu mara Mwarabu mara muhindi. Hivi mnataka kusema mmakonde na mzaramo hawajagundua kitu?
 
Huwa najiuliza kwa nini kila kitu kinacho tuhusu watanzania na waafrika kwa ujumlao utasikia kagundua mzungu mara mwarabu mara muhindi...hivi mnataka kusema mmakonde na mzaramo hawajagundua kitu?????
Sasa wewe mwenyewe unajiita Dirham,

Na umeweka avatar ya "dirham" ambayo ni pesa "currency" ya United Arab Emirates!! Wewe kwanini usingejiita "Shilingi" na kuweka avatar ya Shilingi?
 
Sasa wewe mwenyewe unajiita Dirham,
Na umeweka avatar ya "dirham" ambayo ni pesa "currency" ya United Arab Emirates!! Wewe kwanini usingejiita "Shilingi" na kuweka avatar ya Shilingi?
Sababu ya wewe kujiita CleveeKing ni nini??? We jamaa anaekula Humburger hakuviona vitumbua????
 
Sababu ya wewe kujiita CleveeKing ni nini??? We jamaa anaekula Humburger hakuviona vitumbua????
Unaulizwa swali na wewe unauliza swali?! Sasa wewe si ndio umejifanya kuhoji eti kwanini kila kitu kimegunduliwa na Mzungu na Mwarabu? Kati ya mimi na wewe nani aliyehoji hilo?!! Hapo kwenye red yaani hata kucopy ni tatizo?!

Welcome to JF new member.
 
Unaulizwa swali na wewe unauliza swali?! Sasa wewe si ndio umejifanya kuhoji eti kwanini kila kitu kimegunduliwa na Mzungu na Mwarabu? Kati ya mimi na wewe nani aliyehoji hilo?!! Hapo kwenye red yaani hata kucopy ni tatizo?!
Nilivyo hoji ungejibu swali
suala la kucopy ni typing error.
 
Porojo ndeeeeeefu.

Afrika ni neno la Kiarabu linalotokana na neno "Afrit" kwa maana the hideous, iliyofichika.
Afrique. Kigiriki ni watu walioungua km mkaa!
Hkn kabila la waarabu wale wa sasa ni mchanganyiko wa watumwa na magiriki mavamizi ya Napoleon Bonaparte.walilazimisha tu na kupora haki za weusi.

Hilo jina "Arabs " walidandia tu hwn tofauti na watoto wa Remmy. Au Dr Sarungi, of course wamo na wagiriki pure ambao hawakurudi kwao.
 
Habari ya mchana waungwana, kama kichwa cha mada kilivyo ainisha. Nahitaji kujua asili ya jina AFRIKA.
 
Inasemekana kila jina lina asili yake na maana pia. Hata hilo jina lako ulipewa kwa sababu, na lina asili yake. Kama si la kutoka katika Biblia ama Quran, basi ni

download.jpg

La kimila lenye kumaanisha jambo, kama vile siku, tukio, mahali ama hata shida au raha aliyopata mama wakati wa uzazi wako.

Jiji la Dar es salaam zamani liliitwa Mzizima. Sultani Seyyid Majid wa Zanzibar ndiye aliyelipa jiji hili jina "Dar es Salaam" linalotokana na lugha ya Kiarabu (Dār as-Salām) lenye kumaanisha "nyumba ya amani." Maelezo yanayopatikana mara nyingi kuwa maana ni "bandari ya salama" yachanganya maneno mawili yanayofanana katika Kiarabu yaani "dar" (=nyumba) na "bandar" (=bandari).

Dar es Salaam ilichaguliwa na wakoloni Wajerumani kuwa mji mkuu wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa sababu ya bandari asilia yenye mdomo pana ya mto Kurasini.

Kuanzia 1891 Dar es Salaam ilichukua nafasi ya Bagamoyo kama makao makuu ya utawala. Bandari pamoja na ujenzi wa reli ya kati kwenda Kigoma tangu 1904 ziliimarisha nafasi ya mji ulioendelea kama mji mkuu baada ya Tanzania bara kuwa koloni ya Tanganyika chini ya Uingereza.

Bado kuna mabishano ya ni nini hasa asili ya jina Africa. Wengine wanadai linatokana na neno la Kigiriki la APHRIKE, lililomaanisha kusikokuwa na baridi, ama la Kilatini APRICA, lenye kumaanisha nchi yenye jua daima.

Wengine wanasema neno "Afrika" limetokana na lugha ya Kilatini ya Waroma wa Kale. Waroma kwa jina hilo hawakumaanisha bara lote bali eneo katika jimbo la Carthage ama Tunisia ya leo tu.

Asili yake ni kabila la "Afrig" lililoishi sehemu zile.Wakati huo Wagiriki wa Kale walitumia zaidi jina la Libya kwa ajili ya nchi kusini ya Bahari ya Mediteraneo. Maeneo ya ndani kuelekea kusini mara nyingi yaliitwa kwa jina la "Ethiopia" linalomaanisha nchi ya watu weusiweusi (kwa Kigiriki "aithiops": aliyechomwa na jua).

Katika ramani za kale kutoka Ulaya maneno yote matatu ya "Afrika", "Lybia" na "Ethiopia" yanapatikana yakitumika kama jina la bara. Jina la "Afrika" limekuwa kawaida kuanzia karne ya 16 BK.

Misri ya wakati huo ilikuwa inachukuliwa kama sehemu ya bara la Asia,na alikuwa Mwanajiografia aitwaye Ptolemy (85-165A AD) ambaye aliigawa Afrika na Asia na Ulaya kwa kuchora ramani inayoonesha Suez na Bahari Nyekundu kuwa ndio mpaka baina ya Asia na Afrika.
asili yake ni kinyiha huko mbozi songwe mpya kwa sasa ikiwa na maana" iliyojaaa tele".
 
Afrika ni miongoni mwa mabara saba yanayopatikana hapa ulimwenguni. Ni bara la pili kwa ukubwa likifatia baada ya bara la Asia kati ya mabara hayo saba lenye idadi ya watu wanaofikia bilioni 1.2. Kwa ufupi ni kwamba unapotaja bara la Afrika unataja nchi zaidi ya 60, zinazopatikana kwenye bara na hili na zenye kubarikiwa utajiri wa kihistoria na utamaduni. Na kwa wale wanaofatilia masuala ya tafiti za kiakiolojia, wanakili kuwa Afrika ndio sehemu ya kwanza kupata kukaliwa na mwanadamu.

Na mara baada ya kufahamu hayo machache kuhusu bara la Afrika. Ukweli ni kwamnba kumekuwa na mijadala mingi sana juu ya kuelezea asili ya neno hili Afrika. Na kumezuka fafanuzi nyingi zilizopata kutolewa na baadhi ya wanahistoria. Kwani inaaminika ya kwamba, neno hili la Afrika lina maana yake na lina historia yake inayojitegemea. Kuna baadhi wa wataalamu wanadai kuwa, neno hili la Afrika wala halichipukii hapa afrika na wala halina uhusiano na watu wanaopatikana kwenye bara hili.

Na hivyo wanafafanua ya kwamba, kabla ya bara hili kuitwa bara la Afrika lilipata kuitwa Alkebulan. Ambapo kwa miaka hiyo jamii hizo za mwanzo hawakutambua vizuri eneo hilo la Alkebulan, kwani hawakuwa na uwezo wa kutambua eneo la bara hili kama tunavyojua leo. Kwani msingi wa neno hilo ni Afrika ya kaskazini tu yaani Misri ya Zamani.

Kwa mujibu wa mwanahistoria wa masuala ya kiafrika Dr. Antah Cheikh Diop, kwenye maandiko yake ya “In Kemetic History of Afrika”, anaandika ya kwamba, jina la zamani la bara hili la Afrika ni Alkebulan. Ikiwa na maana ya Alkebu-lan yaani kwa lugha yetu ni “Mama wa Mwanadamu” na wengine wakapaita Bustani ya Eden. Na kwa maana hiyo ikafahamika kuwa neno Alkebulan ndio jina la zamani la bara hili la Afrika.

Ufafanuzi zaidi ni kwamba, watu wa mwanzo kupata kutumia neno hili la Alkebulani ni jamii za Moors, Wanubi, Wanumidi, Wakhart-Haddan pamoja na jamii za mwanzo za Waithiopia. Na kutokana na Waafrika wengi wa mwanzo kukosa kuhifadhi historia zao kwa njia ya maandishi, ikaja kufahamika ya kwamba, neno hili la Afrika lilikuja kuanzishwa na wageni kutoka Ulaya yaani Wagiriki na baadae Waroma.

Inapata kusimuliwa kuwa, wageni hao walioanzisha neno hili la Afrika, kilichowafanya wafanikiwe kusambaza neno hili, ni kutokana na uwezo wao wa kusafiri sehemu mbalimbali na kutawala sehemu hizo na kujiwekea historia yao kadri walivyoamua. Na hata wao wenyewe wanakubali kuwa, kabla ya wao kutumia jina hili Afrika, bado kulikuwa na majina mengine yaliopata kutumika na wakazi wa bara hili la Afrika, na majina hayo ni kama, Ortigia, Corphye, Libya na Ethiopia.

Kwa mujibu wa historia kutoka kwenye jamii za Kikemitiki wanasimulia kuwa, kuna mahusiano kati ya mapinduzi ya kisiasa yanayotokea kwenye nchi za Afrika upande wa magharibi, na kwamba, mapinduzi hayo ni sehemu halisi ya historia ya Kemetiki ya zamani ambayo leo hii ndio tunapata nchi kama Nigeria, Togo, Benin, Ghana, Senegal, Gambia, Guinea, Mali, South Africa, Burkina Faso, Mauritania, Sudan na nchi zingine nyngi za Afrika.

Baadhi ya wanahostoria walijaribu kufafanua ya kwamba, baadhi ya nchi za Afrika ya magharibi zilizoorodheshwa hapo hazina uhusiano na Kemetiki yaani Misri ya zamani, ambayo ilikuwa na jina lake la Alkebulan. Lakini pia kumekuwa na mkanganyiko wa historia ya Afrika magharibi. Ambapo kwa mujibu wa mwanahistoria bwana Samuel Jonson anafafanua ya kwamba kutokana na yeye kujikita kwenye kufanya tafiti juu ya kabila la Wayorubu kutoka huko nchini Nigeria kwa miaka zaidi ya 20, amegundua mikanyiko mingi sana.

Kulingana na maandiko ya bwana Samuel Jonson ambayo yamejikita kufafanua historia ya kabila la Wayorubu kuanzia kwenye utawala wa Uingereza mpaka hivi sasa, amegundua kuwa, baadhi ya tafiti za kabila hilo zinasema kuwa, asili ya kabila hili au historia ya kabila hili linaanzia huko Saudi Arabia maeneo ya Macca, badala ya huko Afrika ya kaskazini maeneo ya Misri au zamani ilivyokuwa ikiitwa Alkebulan.

Bwana Samuel Jonson alizidi kusisitiza ya kwamba, wakazi asili wa kabila la Wayoruba ni kutoka uzao wa Wakoptiki Wakristo waliokuwa wakiishi huko Misri, na ndio maana ukiangalia historia ya Wayoruba na maeneo ya misri unaweza kuona kuna uhusiano mkubwa sana. Na kuna baadhi ya mila na desturi za Wayoruba zilipata kuwepo huko Misri, kwa mfano ule utamaduni wa maisha baada ya kifo. Na hivyo kusisitiza kuwa, hakuna kabila la Afrika linalochipukia nje ya Afrika , na hivyo Afrika ndio Alkebulan na Alkebulan ndio Afrika ya leo.

Kulingana na wanahistoria mbalimbali wanasema kuwa, asili ya jina hili la Afrika, linaaanzia kutumika miaka ya 1600 sawa na karne ya 17. Na kwa wakati wote huo, neno hilo Afrika lilikuwa likimaanisha maeneo macheche sana huko Afrika ya kaskazini. Na kuna kipindi cha ukoloni ambapo kilianzia miaka ya 1800, ambapo mataifa ya Ulaya yalifanikiwa kutawala nchi za Afrika na ndio ukawa mwanzo wa kufa kwa neno hilo la Alkebulan na kutumika neno Afrika, likijumuhisha eneo lote la bara hili.

Kwa mujibu wa wanahistoria wanasema kuwa, neno hili la Afrika, lilianza kutumika na watu kutoka Ulaya ambapo kama tulivyofafanua hapo awali kuwa, watu hao kutoka Ulaya walifanikiwa kusafiri na kutawala sehemu mbalimbali. Kwa mfano Waroma walifanikiwa kupigana kwenye vita ya Punic kuanzia miaka ya 264-146KK, vita ambayo ilihusisha waroma na watu wa Carthage ambayo ndio nchi ya Tunisia ya leo.

Baadhi ya wanahistoria wanafafanua kuwa, neno hili la Afrika, lina asili ya kilatini ambapo kwa mujibu wa lugha ya kigiriki lina maana ya Phrike yaani Dhahabu. Kwa nini walipaita dhahabu, nah ii ni kiutokana na utajiri wa dhahabu walioukuta huko Misri wakati wanafika, ambapo walipata kushuhudia vitu vingi vikiwa kwenye hali ya udhahabu. Ambapo kwa lugha ya kilatini waliita Aprica ikiwa na maana ya Jua. Kwa nini waliita jua, ni kutokana na eneo walilofikia yaani Misri walifanikiwa kuliona jua kwa uzuri zaidi kuanzia kupambazuka kadi kuzama kwake.

Lakini wanahistoria wengi wameonekana kupinga historia hiyo ya bara hili la Afrika. Na wamesisitiza kwamba, neno hili la Afrika, lilipata kuwepo hata kabla ya ujio wa Waroma kufika katika ardhi hii ambayo leo hii ndio bara la Afrika. Ambapo kwa mujibu wa mwanahistoria wa kiafrika, Bwana Matosoko Pheko, amesisitiza ya kwamba, jina Afrika ambapo zamani ni Alkebulan lilifanyiwa uchambuzi na kubainika kuwa, neno hilo lina maana ya mama wa mwanadamu yaani eneo ambalo mwanadamu alipoanza kuishi. “The Mother Of Mankind” lakini pia anakiri kuwa neno Afrika ni miongoni mwa neno ambalo lilipata kuwepo tangu miaka ya zamani.

Na alizidi kusisitiza ya kwamba, yale mawazo ya kwamba, neno hili Afrika halina uhusiano wa moja kwa moja na Waafrika, na kwamba neon hili lililetwa na Waroma, madai haya ni ya uongo. Na hili kulinda hoja yake alifafanua ya kwamba, wagiriki walifika hapa afriuka miaka ya 332KK ambapo miaka ya 250KK walifuata Waroma. Na kwamba wakati wao wanafika hapa tayari neon hili afrika lilikuwa linatumika japo lilikuwa na matamshi tofautitofauti, kwa sababu Waafrika wana lugha nyingi zenye kila aina ya muundo na maumbo. Na kwamba, kwa makadilio tu, kuna lugha zaidi ya 6000 zinazopatikana hapa ulimwengini, ambapo kati ya hizo lugha 3000 zinapatikana hapa afrika. Na kwa maana hiyo ni rahisi sana watu wa Kilatini kutamka Aprica au Aphrike au Africus badala la Af-rui-ka, kama wazawa wa bara hili walivyokuwa wanalitamka neon lao.

Na kuna baadhi ya wanahistoria wanafafanua ya kwamba, kuna uwezekano hata hilo neon ALkebulani kutokuwa sehemu halsii ya historia ya Waafrika. Na kwamba neon yenyewe alkebulan lina asili ya Uarabu . na ili kulinda hoja yao walifafanua ya kwamba, neon al- ni kiambishi awali katika lugha ya kiarabu. Na kwamba asilimia kubwa ya watu wa bara hili sio waarabu na hata kwenye lugha ya kiarabu na historia yao bado neon alkebulan lina utata. Maana haiahamiki neon Al-Kebulan ambapo hapo ukitoka hiko kiambishi awali cha Al- linabaki neon Kebulan , sasa haifahamiki kuwa Kebulan lina maana ganu kwa mujibu wa lugha ya kiarabu.

Kwa kihitimisha ni kwamba, historia ya bara hili inafahamika lakini bado haijafahamika ipi ni historia ya kweli kuhusu bara hili. Na hii ikiwa na maana ya kwamba, bado kuna mkanganyiko juu ya asili ya neno afrika. Na kwamba bado kunahitajika kufanyika tafiti zadi ili kuja na majibu ambayo yatakubaliwa na watu wote

Cc. Shadow7
 
Afrique. Kigiriki ni watu walioungua km mkaa!
Hkn kabila la waarabu wale wa sasa ni mchanganyiko wa watumwa na magiriki mavamizi ya Napoleon Bonaparte.walilazimisha tu na kupora haki za weusi.

Hilo jina "Arabs " walidandia tu hwn tofauti na watoto wa Remmy. Au Dr Sarungi, of course wamo na wagiriki pure ambao hawakurudi kwao.
Hapa watoto wa Sarungi ndo sababu ya comment hii.
 
Ancient Egypt au Misri ya zamani sio Misri ya leo, Misri ya zamani kwa jina la Kemeth ilikua ya watu weusi sio waarabu.

Huwa mnaishia juu juu kutuambia Misri ilikua na watu weusi, lakini mkiombwa evidence ya vipicha hamuleti.
 
Huwa mnaishia juu juu kutuambia Misri ilikua na watu weusi, lakini mkiombwa evidence ya vipicha hamuleti.
acha uzembe wa kijijini umeipikiwa msosi bado unataka unawishwe???

Jiongeze ntakutuna bure xxxcvy!
 
Back
Top Bottom