Je, Viongozi wa Idara ambao ni Wachagga waachie ngazi!??

Status
Not open for further replies.
Natangaza kuwachukia Wachaga..nina sababu na ni watu wenye Chuki na wabinafsi...Yes i said na nitaandika kuhusu hili

Adui wa Wachagga "Gembe"; unaonaje ukafanya mbinu zote ili uwe Rais wa Tanzania (hata kwa mapinduzi); Kama alivyofanya Adolf Hitla, ili hatimae uwaelimineti Wachagga kama Hitla alivyo waelimineti Wayahudi?
Pulu apu yua sox man.
 
Mwanakijiji, naomba unisaidie kujibu hili swali...! Je tukishawaondoa wachaga kwenye maradaka/uongozi tuweke kabila gani? Wamasai? Wagogo? Wanyaturu? Wakurya? Wabondei? Wahazabe? Wafipa? Wahehe? Wahaya? Wanyakyusa? Wapare? Wakara? Wangoni?

Sidhani kama hilo litakuwa tatizo kwani na wenyewe wakishajikita kwenye madaraka sana tunaanza kampeni ya kuwaondoa na wao na tuendelee kupokezana hivyo hadi makabila yote 120 yaishe...
 
Sidhani kama hilo litakuwa tatizo kwani na wenyewe wakishajikita kwenye madaraka sana tunaanza kampeni ya kuwaondoa na wao na tuendelee kupokezana hivyo hadi makabila yote 120 yaishe...

Asante kwa jibu zuri, sasa makabila yote yakishaisha? Nani atafuata? Huoni kitakachofuata kitakua ni kuanza kuhoji udini? Au uzanzibari na Utanganyika? Umri? na vitu kama hivyo?

Je huoni kwa mtazamo huo kama wako unapanda mbegu za chuki na mgawanyo kati ya tanzania? kama nilivyosema hapo awali, kweli mimi sikufahamu, lakini naona kuna agenda ya siri unataka kuianzisha hapa. na tusipokua makini na watu wa aina yako, naona tutaishia kuwa kama majirani zetu, Rwanda na Burundi
 
Ndiyo M/Kijiji,

Itasaidia sana. Ni njia nzuri ya kuleta maendeleo kwa watu wote.

Kwamba aliye mbele akamatwe, azuiwe aliye mbele asubiri, ili wengine nao waje taratiiiibu kumfikia. Ili waanze pamoja tena. Usijali kwamba huyo alieyebaki nyuma atakuwa ametumia muda gani kumfikia yule anayesubirishwa.

Kwa kuwa suala hapa ni kuwepo kwa usawa, haitaruhusiwa tena mtu yeyote kukimbia kimaendeleo na kuwaacha wengine nyuma. Kila tukiona dalili kama hiyo inajitiokeza tunazuia tena. Njia ziko nyingi .. walipe kodi zaidi, nafasi za elimu zisitolewe kwa wengineo, biashara za upendeleo, kazi kwa upendeleo ...

Wale watakaokuwa wakubwa serikalini waruhusiwe kujilimbikizia mali kifisadi, hasa kama wanatoka makabila nje ya wachagga.

Mpaka wote tuwe SAWA!

SAWA KABISA.

Inawezekana.....

AU? .......
 
This thread has negative connotations, nakumbuka hadithi ya Mwalimu ,ile ya wachawi.Ukila nyama ya mtu mmoja utaendelea kula tu nyama ya mtu!!!!
 
Asante kwa jibu zuri, sasa makabila yote yakishaisha? Nani atafuata? Huoni kitakachofuata kitakua ni kuanza kuhoji udini? Au uzanzibari na Utanganyika? Umri? na vitu kama hivyo?

Je huoni kwa mtazamo huo kama wako unapanda mbegu za chuki na mgawanyo kati ya tanzania? kama nilivyosema hapo awali, kweli mimi sikufahamu, lakini naona kuna agenda ya siri unataka kuianzisha hapa. na tusipokua makini na watu wa aina yako, naona tutaishia kuwa kama majirani zetu, Rwanda na Burundi

Mkjj, hajabagua wala hawezi kuwa mmbaguzi. Nachoamini ni kuwa kuna ujumbe ataka ufikisha hapa (I hope i did not get him wrong)!!!!

Mhafidhina, hujasikia tuhuma kuwa wachagga wanapendeleana na kupeana ajira kiasi cha kujazana maofisini??? Mfano ilishazungumzwa sana kuwa TRA wamejazana wachagga!!!!

Sio siri kuwa kama ambavyo baadhi ya binadamu wa makabila mengine wanavyopendeleana, wapo wachaga wanaofanya hivyo pia. lakini hiyo haimaanishi kuwepo kwao wengi maofisini ni kutokana na sababu ya upendeleo tu!!! Ni mapungufu ya kibinadamu tu

HAPANA bwana, hao jamaa wameenda shule na wana usongo wa maisha. Take note kuwa, Kujazana kwao, si maofisini tu bali hata kwenye biashara. Pitia vioski, maduka, mabaa, mahoteli, magesti, shoe shinner, mafundi saa, by proportion utaona wachaga ni wengi!!!!

Watu wamezuia uwezo wao wa kufikiri na kuishia kudhani kuwa wachagga wanapendeleana bila hata kuangalia historia ya wachagga kielimu/taaluma. Nadhani ni kutokana na hali ya kuficha udhaifu wetu au kukubali kuwa tuna mapungufu ndio maana hawa jamaa wanatuzidi. Au kwa lugha ya mitaani TUNATAFUTA MCHAWI, WAKATI WACHAWI NI SISI WENYEWE!!!!

Ndio maana imetolewa RAI, wachaga waondolewe, kisha lije kabila jengine ambalo nalo tukiona wamejaa twaliondoa. Tunazunguka weeee mpaka tunamalizana!! NADHANI HOJA HII INALENGA ZAIDI MAMBUMBUMBU WA KUFIKIRI na wala si fikra za kibaguzi!!!!!
 
Mzee Mwanakijiji, you are not serious my dear, are you?
kama hoja ni wachaga kuwa wengi kwenye idara fulani, ni bora taratibu za ajira za idara hiyo zichunguzwe, huenda zina matobo yanayopelekea watendaji kujiamulia kwa interest zao. Then matobo hayo yazibwe. Laikini kusema waachie ngazi wote, simply because they are chaggas ni upotofu. Jamii ya Kitanzania isiyoamini katika ukabila itapotoka sana endapo kwa mara ya kwanza itaamua on tribal basis.

Alternatively, the Government (if need be) should put an effective Performance Management mechanism in place to track and measure performance of its employees be they Chaggas or Kweres. Atakayebainika kutofikia malengo yaliyowekwa aondolewe bila kujali ni Mmasai, msukuma,mjaluo etc then nafasi hizo wapewe wenye uwezo.....hata kama watakuwa wachagga tena!
Mzee Mwanakijiji nimekuwa nikisoma mada na hoja zako ndani ya JF. mara nyingi nimekuwa nikiziona nzuri na hoja za nguvu, hivi imekuwaje leo umeibuka na hoja hii? Ndiyo maana nikaanza kuuliza your seriousness on this.
 
Mwanakijiji unaleta mambo ya Wahutu na Watutsi. Acha hiyo sumu kabisa. Tujifunze yaliotokea kwa nchi hiyo na madhara yaliyoletwa na uchafu kama huo.
 
Naanza kupata hofu kuwa kwa post kama hizi baadaye zinaweza kusababisha wakapatikana watu kama akina THEONESTE BAGOSORA, ANOTOLE NSEGIYUMVA, ALLOYS NTABAKUZE na wengineo ambao wamebainika kuwa walianza mipango ya kuwafuta wenzao wa kabila la Kitusi kwenye uso wa dunia kwa takribani miaka minne na zaidi, kabla ya kuanza utekelezaji. Much care is needed, vinginevyo kuna watu ambao ni wepesi mno kupandikizwa mbegu ya chuki mioyoni mwao na baadaye kuwa vigumu sana kuwarekebisha kisaikolojia.
 
Hivi tunaweza kukaa chini na kuzungumzia ukabila kwa mtiriko kama huu wa M/Kijiji? Hebu chungulia nje zaidi, k.m Kenya, au hata South Africa, au UK, hauoni trend ni ile ile kwamba kuna watu wa sehemu fulani wanaonekana zaidi katika nyazifa fulani, kwa wenzetu watasema watu wa kusini au kaskazini lakini pengine sio kwa makabila. Nyerere alisema, INATUPASA TUKIMBIE ILHALI WAO WANATEMBEA. Kama kweli shida ni wengi kuhisi wameachwa basi hao wanapaswa wachukue jitihada zaidi ili wawahi hao walio mbele yao.

Lakini ni nani anasema watu hujipanga kama kabila. Mimi ni Mchagga, nilikwenda shule, sikupita darasa la saba, ikabidi nirudie mara kadhaa, na wazazi walitaka nifanye kazi niachane na shule, lakini kumbe baadae nimefika Chuo Kikuu na nimetembea nchi nyingi, lakini sikumbuki hata mara moja kusaidiwa na mchagga au kwa namna hio na mtu yeyote mwingine, ni jitihada zangu na ninajisifia. Sasa wewe kalia unatafuta kwa nini wewe si CEO ukidhani nafasi hiyo umenyenganywa na wachaga, wakati unalalalama wenzio wanachimba vitabu. Mkijiji wacha tabia mbaya hio
 
If they are recriuted based on merits hamna taabu issue ni pale mtu akiajiliwa kisa ni binamu,au uncle au jirani kijijini.
Mara nyingi wanaoajiliwa kwa namna hiyo wanakuwaga wasumbufu maofisini alafu vimeo kwa kwenda mbele
 
Mimi sikubaliani kabisa na kauli hii. Ndugu zangu wachagga wamewajibika sana katika kuuendeleza uchumi wa taifa hili. Kila kabila halikosi watu wenye tabia mbaya lakini kuwaweka wachagga wote kwenye kapu moja, hilo halikubaliki. Lazima uchochezi aina hii uwekewe kikomo. Hili haliwezekani kabisa.
 
Ni muhimu kwa mleta maada hii angefanya utafiti japo kidogo ili kuweka uzito wa hoja yake,sijawahi kuona tangazo la kazi lenye sifa ya mtu atakiwe awe ni MCHAGGA. ni kwa utafiti japo mdogo ungetufungua macho au kuonyesha udhaifu wa hoja yenyewe,Mfano angeenda kwenye idara husika na kukagua taratibu za ajiri, pamoja na kuona matangazo ya ajira na sifa za waombaji na namna walivyochaguliwa.( Usikute nafasi tano za ajira,jumla ya waombaji wenye sifa'200' wachagga 110 wengineo tisini,namna hiyo hata awakichaguliwa wachagga watatu,na wengine mmoja mmoja kwa mantiki hiyo tutegemee ofisi iwe na wachagga weingi. Nafikiri hoja ingekuwa na maana kama ingeeleza wengi wa wachagga wasio na sifa... hakika ni upuuzi na ni kama hoja iliyovuma hapo mbeleni ya wakiristo na waislam katika ajira ...
 
Wachaga ni Wahindi wa Kitanzania...mababiani haswaaa..kwenye kila kitu.Wanajituma na wanastahili kuwa mbele.
Chuki na fitina hazina maana.Makabila mengine inabidi tujitutumue ili kujaribu kuwa kama Wachaga.Mimi nwa admire kwa kuwa wachapa kazi na wasomi.
 
Kama kwa hiari haiwezekani, Rais anaweza kutoa agizo (executive order) na kutaka wachagga waachie ngazi na wakae pembeni kwa angalau miaka mitano ili watu wa makabila mengine wapate nafasi. Hili linaweza kuwahusu Wanyakyusa na Wahaya vile vile. Kama hawatafanya kwa hiari tunaweza kufanya kwa nguvu hata kwa kutunga sheria maalum ya kuwalazimisha.

Mzee Mwanakijiji et all,

Mie naona kuna haja sasa ya viongozi wote ambo ni wachaga wachie Ngazi sababu utumbo mwingi umefantywa na wachaga...umekuwa ni wizi mtupu kila siku...

 
Takwimu za elimu za miaka ya 60 zinaonesha kuwa Wachaga walikuwa juu sana kwa kuwa na wahitimu wa shule za msingi na sekondari. Walijenga sana shule za wazazi enzi za ukosefu wa nafasi za sekondari. Hata sensa ya 88 inaonesha wachaga, wake kwa waume, walivyokuwa mbali sana katika suala la kuwa elimu na taaluma.

Hapa kuna uhusiano wa kitakwimu kati ya mafanikio hayo ya kielimu/kitaaluma na uwepo wao katika takribani kila nyanja ya taaluma na biashara Tanzania. Hili ni suala la kihistoria. Inabidi liangaliwe kihistoria.

Pamoja na haya yote nchi yetu haijatoa Rais Mchaga - imetoa Mzanaki, Mkwere, Mzaramo na Mmakonde! Hii yote inaonesha jinsi gani tumepiga hatua katika kusawazisha tofauti za kihistoria. Hekima Umoja Hizi ni Ngao Zetu!
 
Hii thread imenishtua sana. Hata hivyo, kwa kuwa tunaheshimu uhuru wa kujieleza, basi mambo ya ukabila yajadiliwe kwa staha, umahiri, ukweli na kwa malengo ya kujenga. Tukitumia uhuru wetu kubomoa, basi tutakuwa tunafanya ufisadi wa uhuru huu. Tukifika hapo, hatutakuwa na tofauti sana na mafisadi wanaopigiwa mayowe wajameni...chonde chonde tuwe waangalifu.

Naomba mtafute best quotes za mwalimu kwenye ile thread ya ukabila, bahati mbaya sina muda sasa, ila nakumbuka kama alisema mtu anayeanza kujadili kabila la mtu yeye ndiye mwenye ukabila? Naomba tusaidiane, ipo humu, nilisoma mwaka jana tafadhali. Itatusaidia kupanua mawazo yetu, hata kama inaweza kuwa si sahihi.
 
Tujiangalie sana tunapojadili jambo hili kuhusu ukabila. Lawama kutoka kwa wananchi fulani wanaosema Wachagga, au Wachaga, wanatunyonya kama kupe haina msingi wowote.

Hawa ni ndugu zetu. Wamefanya kila jitihada kujiendeleza kwa miaka mingi sana hata kabla ya uhuru wa nchi yetu iliyokuwa inaitwa Tanganyika.

Nani walimpiga mrija na kumfyonza damu walipofanikiwa kupata elimu kabla ya Watanzania wengi kutimiza lengo hilo?

Ni makabila gani waliyoyanyonya na kuyakandamiza walipofanikiwa kuwa na maendeleo kule Kilimanjaro kabla ya mikoa mingine nchini Tanzania?

Nani aliwazuia watu wa makabila mengine kujenga shule kama Wachaga walivyojijengea shule katika mkoa wao?

Nani aliwazuia watu wa makabila mengine kwenda shuleni?

Kwanini Wachaga wameweza kupata elimu ya juu kuliko makabila mengi nchini Tanzania?

Kwanini wamefanikiwa kibiashara na kuchuma fedha sehemu zote za taifa letu kuliko watu wengi wa makabila mengine?

Mnataka Wachaga waache kusoma shule ili wasifanikiwe maishani?

Mnataka Wachaga waache kufanya biashara ili raia wote tuwe sawa katika umaskini?

Mnataka Wachaga waangamie?

Wamefanya nini, hawa ndugu zetu Wachaga, kustahili chuki ya aina hii?

Tangu lini katiba yetu imesema ili kuwa na taifa moja, ni lazima makabila yetu yaishi sehemu zao, yatengane, na kwamba Wachaga, Wanyakyusa, Wahaya na watu wa makabila mengine hawana haki kuhamia na kuishi na kufanya biashara sehemu mbali mbali za Tanzania?

Tumesahau Mwalimu alipotuonya kwamba tukiendelea na ubaguzi huu na kuwalaumu Wachaga, Wahaya na Wanyakyusa, taifa letu litakwisha na tutaanza kupigana na kuuana. Alivyosisitiza, ni upuzi na ukabila wa aina hiyo "which led to the establishment of Biafra," a point he underscored in his radio broadcast to the nation in September 1968 a few months after Tanzania recognised Biafra as an independent nation in April that year, the first country to do so; the late Chediel Mgonja, who was then minister of state for foreign affairs, made the official announcement.

Kama kuna Watanzania wengi wanaowachukia Wachaga, mnataka wajitenge? Watakuwa na haki kufanya hivyo na kuwa na nchi yao.

And if they do so, please, please, don't do anything to impede their progress by denying them access to the sea or by trying to choke off their landlocked nation. Leave them alone so that they can continue to thrive in their homeland - the Republic of Kilimanjaro or Chaggaland or whatever they want to call it.

Ndiyo maana ni muhimu katiba yetu pamoja na katiba zote katika bara letu ziwe na provisions ambazo zinawaruhusu watu wanaobaguliwa kuwa na nchi yao - the right to self-determination. Let them go. The same applies to Zanzibar. Kama the majority of Zanzibaris - for whatever reason - hawataki kubaki katika muungano and have demonstrated their wish in a referendum or plebiscite to pull out of the union, fine, - let them go!

Thank God, the vast majority of Tanzanians don't feel that way: that discrimination is right, and that tribalism should be institutionalised as a national virtue as it has been in Kenya since - and even before - independence despite claims to the contrary by some Kenyans.

We are the only country in Africa with a reputation of having virtually conquered tribalism in spite of the fact that we have one of the largest numbers of tribes or ethnic groups on the continent and are also one of only four countries with more than 100 - the others being Nigeria, the Democratic Republic of Congo (DRC), and Cameroon.

I hardly post anything here. I am just an interested observer. But my conscience won't let me rest and I have decided to write something in response to what I consider - as many people do - to be a vicious campaign against the Chagga on this forum and elsewhere. And it's nothing new in Tanzania and among Tanzanians elsewhere concerning the Chagga.

There seems to be a concerted effort by a number of unscrupulous individuals to whip up sentiments against the Chagga in an attempt to mobilise forces against them, portraying them as villains who have been able to forge ahead at the expense of their fellow countrymen - and women.

The Nyakyusa and the Haya have been hammered the same way, although in varying degrees. More often than not, the primary target seems to be the Chagga.

The sledgehammer that's being wielded and used against the Chagga - and to a somewhat smaller degree against the Haya and the Nyakyusa but sometimes just as viciously by a few individuals - is the same lethal weapon Hitler used in his diabolical campaign to exterminate six million Jews.

It's also the same weapon the Hausa-Fulani used against the Igbo in Northern Nigeria, leading to pogroms in which more than 50,000 Igbos were massacred in different parts of Northern Nigeria within three months in 1966 alone - between July and September - and eventually to the death of about 2 million of them by the time the Nigerian civil war ended on 12 January 1970 - officially on January 15th when the seccesionist forces of Biafra were forced to surrender to federal might after they were viciously pounded into submission by Nigerian federal troops of an army division led by Olusegun Obasanjo, a Yoruba from the Western Region, who later became the military head of state and then civilian president of Nigeria.

It's also the same weapon, stoking embers of hatred against a targeted group, which led to genocide involving the extermination of about 1 million Tutsis in neighbouring Rwanda in 1994 at the hands of the Hutu, and to the massacre of about 500,000 Hutus in Burundi by the Tutsi since 1993, without even counting the 100,000 Hutus who were wiped out by the Tutsi in Burundi in 1972 and 1973.

It's also the same weapon members of different ethnic groups have used against each other with unconstrained fury in neighbouring Kenya with tragic consequences; also the same weapon the Zulu used against the Xhosa and vice versa in South Africa in the early 1990s when more than 10,000 people were killed just before the diabolical institution of apartheid came tumbling down.

And it can happen right here in Tanzania if we are not careful about that.

Kuna watu wanaosema kusudi la mjadala huu wa swala hili kuhusu Wachaga ni kusisitiza kwamba kila Mtanzania ana haki zote kama wananchi wenzake.

I'm skeptical of that. It's just a clever way of trying to hide one's ulterior motives which include fostering and fuelling tribal sentiments against the Chagga and members of other tribes who are accused of thriving at the expese of their fellow countrymen.

But having said all that, haimanishi kwamba hatuna ukabila - kabisa au hata kidogo - nchini Tanzania. Kuna ukabila, but not of the virulent kind that's prevalent in Kenya. And we should admit that there are tribalists in every tribe.

Tukiendelea kukaa kimya ingawa tunajua ukweli kuhusu ukabila wa wenzetu katika makabila yetu, taifa letu halitakwenda popote. Huo ni ukabila, na tutajiangamiza wenyewe na ukabila wetu.

Hakuna Mchagga anayesema ukweli ambaye atakana ukimwambia kwamba kuna Wachagga ambao wana ukabila sana. Hakuna Mnyakyusa, Mhaya, Mgoni, Mhehe ambaye atakana hilo - kwamba kuna watu katika kabila lake ambao wana ukabila sana. Kuna ukabila katika makabila yote. Tatizo ni kuwalaumu watu kutoka makabila machache - hasa Wachagga, Wahaya na Wanyakyusa - kwamba ndiyo hao tu wenye ukabila nchini hapa Tanzania au kwamba ndiyo hao ambao wanawanyonya na wanawakandamiza wananchi wenzao.

Kitu ambacho nasisitiza hapa ni kwamba tupambane na ukabila wa kila aina kama tulivyopambana na ukoloni na kama tulivyowasaidia ndugu zetu nchi za Afrika kusini katika vita vyao vya ukombozi ambavyo pia vilikuwa ni vita vyetu kama Wafrika - kwani sisi sote Wafrika ni "ndugu moja" - (si Kiswahili cha Wahindi tu!)

Kama TANU creed ilivyosisitiza tulipoanza kugombea uhuru, Afrika ni moja na Wafrika wote ni ndugu zangu.

And practise what you preach.

Tumeishi kwa amani bila kuchapana mapanga, kupigana virungu na kuchomana visu tangu tulipopata uhuru. Hata kabla ya uhuru, watu wa makabila mbali mbali katika nchi yetu waliishi pamoja bila kumwaga damu. Lakini ikiwa hatujitahadhari, that's exactly where we are headed.

God forbid!

Ukabila ni balaa. Na tunaposema Mungu ibariki Tanzania, we should mean it. Hatuwezi kufanya hivyo ikiwa tumejaa chuki ya ukabila. Wachagga ni ndugu zetu. Sisi sote ni ndugu moja.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom