Je! Viongozi wa dini na wao wanaapa baada ya kuchaguliwa?

nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
1,012
843
Naomba kuuliza? hivi Viongozi wa dini baada ya wao kufanya uchaguzi ndani ya taasisi zao na wao huwa wanaapa kwa kutumia vitabu Vitakatifu Kama ilivyokwa Viongozi wa Serikali ?
 
Viapo vya kutumia vitabu vya dini havina uzito wowote , jitu lina apa kuwa mwadilifu lina enda kinyume chake na hakuna chochote kinachompa .

Vile viapo vya asili vingekua vinatumika watu wangenyooka hasa hawa viongozi uchwara.
 
Sijajua kwa upande wa Dini nyingine na madhehebu mengine ya kikristu

lakini angalau kidogo ninafahamu kwa Roman

katika makanisa ya Roman Katoliki, viongozi wa dini, kama vile mapadre, maaskofu, na kadinali, wanaapa kwa kutumia vitabu vitakatifu. Hasa, Biblia Takatifu inatumika wakati wa kutoa viapo muhimu. Hii inaweza kuwa wakati wa kuwekwa wakfu, kupewa madaraka maalum, au kuahidi utiifu na uaminifu kwa Kanisa na mafundisho yake. Viapo hivi vinatolewa kama ishara ya kujitolea kwao kwa imani na kwa huduma ya Mungu na Kanisa.
 
Back
Top Bottom