Je viongoz wetu wametusaliti kwa kusisitiza kiswahili while watoto wao english medium

Mporipori

Member
Nov 22, 2010
44
0
Salaam wana JF.,

Imekuwa ikisisitizwa mara nyingi hasa na viongozi wetu kwamba kiswahili ndio lugha ya taifa tuienzi. Na sababu kubwa ya kuiweka kuwa lugha ya kufundishia ni kwa sababu ni lugha ya taifa. Lakini wajumbe mtakubaliana na mimi kuwa lugha hii haina tija kwa sasa.. Kama ni compulsory kama lugha ya taifa, kwa nini sasa kuna English medium schools ambazo zinaheshimika sana na ndiko viongozi wetu na watu wengine wenye uwezo wanasomesha watoto wao huku wakiwaacha walala hoi wahangaike kwenye shule za kiswahili kuidumisha 'lugha ya taifa' halafu baadae secondary wanafundishwa kwa kutumia kiingereza wakati ubongo umeshaanza kuchoka. matokeo yake tunapata product dhaifu na wasomi ambao hawawezi kucompete kwenye market.

Hivi ni sababu gani ya msingi inayofanya tuendelee kukumbatia kiswahili na kukitumia kama medium of instructions in primary schools (ambapo wote tunajua ndio muda muafaka ambapo mtoto ni rahisi kudevelop communication skills)

Je viongozi wetu wanasubiri nini..?
 

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
1,195
Viongozi wetu ni wabinafsi. Kama viongozi wetu wana nia ya kukikuza, mbona hata katika dhifa za taifa, Rais wetu haongei Kiswahili? Tukumbuke pia mwaka 1995, Mh.Mrema alipogombea urais, CCM walikuwa wakijinadi kuwa Mkapa ni bora zaidi kwa kuwa amebobea katika lugha ya Kiingereza na kuwa itakuwa ni aibu kwa taifa kupata rais asiyemudu Kiingereza vizuri.

Kiswahili kiendelee kuwa lugha ya Taifa lakini Kiingereza iwe lugha ya kufundishia.
 

SUWI

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
548
195
Kwanza itabidi hao waalimu wa Primary warudishwe shule kwa kujifunza english la sivyo itakuwa balaa!!!!!!!!!
 

Mporipori

Member
Nov 22, 2010
44
0
Ni tatizo kubwa kutumia kiswahili kufundishia while tunajua hakitusaidii chochote zaidi ya kuturudisha nyuma.. chukua mfano wa vitabu hata vya story tu, ni ngumu kumkuta mbongo amekaa anajisomea sababu ya lugha (vingi vipo kiingereza) how tutaweza kujenga wasomi na jamii yenye uwezo wa kujieleza na kuchambua mambo katika ulimwengu huu wa utandawazi..?

Ndio maana tunaogopa kuingia shirikisho la Africa mashariki coz wasomi ni wachache na wachache hao bado hawajiwezi.. Kwa nini hawataki kuukubali ukweli..? au wanataka wawe wachache..?

Mwanafunzi wa Tanzania siku zote ana kazi mbili anaposoma 1. Kutafsiri lugha 2.Kuelewa concepts za somo husika. dats elimu yetu inaonekana ngumu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom