Je, vidonge vya ku "cream" ngozi ni salama?

Je, vidonge vya ku "cream" ngozi ni salama?

Si kweli ishu ya kuoza huyo alikua na matatizo mengine, angesema labda kuharisha, kuumwa kichwa nk sawa ila kuoza hizo stori tu za mitaani hazina ukweli wowote
Wee tumbili nini? Amekueleza madhara yanayoweza kutokea ama yaliyowahi kuwakuta watu- sasa unapinga nini? Umeuliza ili usikie sifa nzuri ee? Sasa kwa nini unasumbua watu si uyatumie tu kama taarifa mbaya huzitaki.
 
Nime ulizwa hili swali, kutokana na taaluma yangu, na huyu dada nikakimbia kuangalia ingredient, naona vitamin c, glutathione ila bado Nina mashaka sana nikaona nilete Kwa wataalamu husika watupe elimu Kwa manufaa ya wote, pliz wazee wa kutukana tafdhali hapa ni ulingo wa elimu si kubezana

Kwa nini awe mweupe?
 
Unasema umeulizwa kutokana na taaluma yako; nikajua wewe ni Dermatologist?
Kwa kifupi dawa yoyote inayobadili ngozi, ina adhiri Melanin inayotengenezwa na melanocytes kwa ajili ya kulinda ngozi na UV nk
Sasa ukiondoa mlinzi jua chochote kinaweza kuingia...inabidi uanze kuweka walinzi artificial ambayo ndio unaona watu kucha kutwa wanakimbizana na mavipodozi yenye sumu za kila aina ni kwa kuwa, kwa namna moja au nyingine wali ondoa walinzi wa ngozi kwa kujua au kutokujua.
KWA KIFUPI SIO NZURI, NA UKITOA MLINZI WA ASILI (Melanin), TEGEMEA KUTUMIA GHARAMA KUBWA KUAJIRI MLINZI WA KUMLIPA (kutumia vipodozi dawa muda wote).
 
Si kweli ishu ya kuoza huyo alikua na matatizo mengine, angesema labda kuharisha, kuumwa kichwa nk sawa ila kuoza hizo stori tu za mitaani hazina ukweli wowote
Yaani wewe unatafuta ushauri ila unatamani kusikia positivity tuu bila madhara, hakuna cha rafiki wala nini hapo naona ni kama umeanza kuleft group unatafuta changes za haraka
 
Nime ulizwa hili swali, kutokana na taaluma yangu, na huyu dada nikakimbia kuangalia ingredient, naona vitamin c, glutathione ila bado Nina mashaka sana nikaona nilete Kwa wataalamu husika watupe elimu Kwa manufaa ya wote, pliz wazee wa kutukana tafdhali hapa ni ulingo wa elimu si kubezana

Nilishangaa kuona hadi wagombea urais wanajichubua.

Wanawake wana mambo ya kijasiri sana.
 
Yaani wewe unatafuta ushauri ila unatamani kusikia positivity tuu bila madhara, hakuna cha rafiki wala nini hapo naona ni kama umeanza kuleft group unatafuta changes za haraka
Kaka hii ni biashara nayotaka kifanya, kusema kuoza ngozi sijawahi sikia hicho kitu tunaharibiana biashara
 
Naona mtoa mada ye moya ndjo anatafuta kuwa mweupe, anajifunga anasema kutokana na taaluma yake, taaluma gani inayouliza afu anasikilizia majibu ya positive effects tu hataki mtu awe na negativity juu ya hayo makitu? Atoke pale ye moya anatafuta kuleft group
Mi ni clinical medicine kaka punguza ka mdomo ume kia asha boko wewe, asha ngedere acha pigo za kike hapa hatuchambani tunapeana elimu
 
Mafuta yoyote yanayobadili rangi ya ngozi og sio mazuri kwa ngozi! Japo mimi huwa naangalia kama hakuna hydroquinone ndio natumia maana unakuta lotion kali kama caro white ina asilimia 4.4-4,5% na mtu anaungua kama kaungua na moto! Hydroquinone inazuia melanin kutoka na hivyo husababisha kansa ya ngozi!

Vitamin c kazi yake ni kufanya ngozi ionekane bright na glutathione ni antioxidant ina kazi ya kufanya ngozi ku enlight! Na hizi huwa wanaweka kidogo tu ili product ionekane safe na sio safe! Acids kama AHA/BHA, hydroquinone, tretinoin, au steroids ndio zinazofichwa humo!
Kwahivyo mchanganyiko ni mwingi mwanetu!
NI mwendo wa kupaka sumu tuu
 
Nasikia Kuna mtu alimeza akaamza kuoza huku anajiona..

Kila utachoingiza tumboni mwako kinaenda kwenye mfumo wako wa damu.kinagusa Kila organ yako mwilini.tumbo,utumbo,kibofu,Figo,ini,kongosho,nyingi,moyo,mapafu nk.
Kabla hujameza uwe unafikiri kwanza.
Mitandao ya kijamii nayo inawaharibu sana wenye vichwa vibovu. Unakuta ukiingia Instagram kila mdada unayemuona ana glow basi hapo mtu tamaa inamuingia na yeye anataka ku glow na rangi yake ya cocoa.
 
Nashukiru sana, mi ni mfanya biashara huyu dada kanizindua, kuhusu vidonge nimshauri, nikaona hii ni fursa, let me use it nivichukue nisambaze, but nikataka nipate experience, come-on hata paracetamol unayo kunywa ina madhara kwani usimywe dawa za kienyeji ambazo nazo huleta kidney failure

Sasa unauza vitu na hauna ujuzi navyo kielimu?
 
Back
Top Bottom