Je, Utawala Wa Rais Magufuli Ndiyo Wengi tuliutarajia?

Ndikwega

R I P
Feb 1, 2012
5,979
5,524
Naomba tujadili hii, ni kweli kuwa Watanzania tulikuwa tunautaka Utawala wa Namna ya Magufu?

Ni dhahiri huyu Mh. angependa katka Dunia hii abaki na wale wanao muunga mkono tu kila anayempinga amtoweshe. Je, ndicho tulikihitaji kutoka kwako?

Push up zote zile kumbe alikuwa anafanya ili atimize Matakwa yake ya hivi kutufanya wote tukose amani ndani ya Nchi yetu huru? Kuna faida gani ya Kusema Unawapenda Wananchi na huku Vitendo havishabihiani na yele Maneno yako!

Mh, nakuhakikishia Watanzania Walio wengi kama Siyo Wote wana hasira Vifuani mwao dakika yoyote wanaweza kupasuka. Hao wengine umaowatumikisha (Mwondoe Bashite) wote wanakwenda tu kwavile hakuna namna!

Nasikiti maisha yako baada ya Utawala huu! Sikutegemea kabisa kama ungekuwa wa hivi japo ni wengi wanaumia pia!
 
Amefanya mengi na makubwa ya kuineemesha nchi nje ya matarjio hafifu ya wanyonge wa Tanzania.
 
Mimi ndio hata hua siangalii taarifa ya habari kabisa hasa nikihisi atatokea ktk habari siku hiyo.
 
Mimi kwenye maamuzi ya kijinga nilitegemea afanye ujinga zaidi ya huu. Ila naona anajitahidi ujinga hayo maamuzi siyo mengi sana
 
Kwa kweli kavuka matarajio yangu kiasi kwamba natamani hata nijiunge na CCM,
 
Hakuna mtu Tanzania au Africa ya leo angetegemea Magufuli kufanya mambo anayoyafanya kila ninapokua nje ya nchi na kusema natokea Tanzania tofauti na zamani kitu wanachojua Tanzania ni "that country of Magufuli?"

Magufuli kaiweka Tanzania and Africa kwenye ramani ya dunia that's true that's it.
 
Back
Top Bottom