Je, Utawala Wa Rais Magufuli Ndiyo Wengi tuliutarajia?

Ulikuwa unamuunga mkono naona sasa upo kinyume.
Nilikuwa namuunga mkono baadhi ya mambo lakini nishaona uwezo wake mdogo. Hajui na hafanyi chochote kuboresha maisha ya watu. Yeye yuko busy na mambo ya AJABU AJABU ya kina LISSU, MANJI, IPTL nk

- Anaacha watu wengine wanateseka huku wengine wanalipana MIPOSHO YA LAKI 4 PER DAY!

N.B Kumchoka Zigo wa magogoni haimaanishi nawaunga mkono MIZIGO MIZITO YA UPINZANI
 
Tunambiwa na wahenga bali hatusikii.Mpe cheo, na fedha mtu aliye maskini, utajua maana halisi ya umaskini.
 
Umewahi katika maisha yako yote kuwa na rafiki asiye na vision?

Au umewahi ukiwa shuleni mkaongozwa na kiranja kilasa?

Magufuli hana vision kabisa. Na alipata nafasi hii bila kutarajiwa. Huyu anasogeza tu muda ili kiongozi wa nchi aingie. Yeye hana hata chembe ya uongozi kwa hiyo hajui anakoelekea hajui anachokifanya yaani ni sawa na hao watu wake wasiojulikana.

Hivi tatizo kama LA Lisu rais wa nchi anatwit hiyo ni akili kweli? Yaani Mungu utusaidie.
 
Laura Bagbo naye alikuwa na wafuasi kama alivyo Magu na yeye pia alikuwa anasema nalinda rasilimali za nchi yake. Lkn yuko wapi sasa. Magu namshauri asifikiri hicho kiti ni cha hadi kufa.
 
Nimekuelewa mkuu,mimi ni mhanga wa hali iliyopo Tanzania ila sifungamani na upande wowote.
Nilikuwa namuunga mkono baadhi ya mambo lakini nishaona uwezo wake mdogo. Hajui na hafanyi chochote kuboresha maisha ya watu. Yeye yuko busy na mambo ya AJABU AJABU ya kina LISSU, MANJI, IPTL nk

- Anaacha watu wengine wanateseka huku wengine wanalipana MIPOSHO YA LAKI 4 PER DAY!

N.B Kumchoka Zigo wa magogoni haimaanishi nawaunga mkono MIZIGO MIZITO YA UPINZANI
 
Hivi kwa jinsi vitu vinavyoendelea unategemea wapi na lini ushawaunga mkono mtu??

Ni lini ulikaa mwenyewe ukasema huu utawala wa awamu zote zilizopita ukafanya mambo uliyoyategemea??

Tatizo sisi sooote tunawaza masirahi yetu wenyewe yani ya leo ukifa wewe kila kitu kiwe kimekwisha.

Mimi namuunga mkono dr. Slaa basiiiii....??

"" nchi ilipofikia tunamuhitaji kiongozi mwenye maamuzi magumu""

Sawa tuliowengi ni wahanga wa huu utawala si utani tunanyooooka tuu.

Slaaa uliko naanza kuelewa ulimanisha nini...

Utajikuta tusiounga mkono tunaangukia kwenye hadithi ya mwalimu nyerere ya kumugeuza Rais jiwe sasa tunafeli.

Mwisho kabisaa kwa namna alivoninyoosha sikutarajia na siungi mkono utawala huu kwa masirahi yangu.
 
Naomba tujadili hii, ni kweli kuwa Watanzania tulikuwa tunautaka Utawala wa Namna ya Magufu?

Ni dhahiri huyu Mh. angependa katka Dunia hii abaki na wale wanao muunga mkono tu kila anayempinga amtoweshe. Je, ndicho tulikihitaji kutoka kwako?

Push up zote zile kumbe alikuwa anafanya ili atimize Matakwa yake ya hivi kutufanya wote tukose amani ndani ya Nchi yetu huru? Kuna faida gani ya Kusema Unawapenda Wananchi na huku Vitendo havishabihiani na yele Maneno yako!

Mh, nakuhakikishia Watanzania Walio wengi kama Siyo Wote wana hasira Vifuani mwao dakika yoyote wanaweza kupasuka. Hao wengine umaowatumikisha (Mwondoe Bashite) wote wanakwenda tu kwavile hakuna namna!

Nasikiti maisha yako baada ya Utawala huu! Sikutegemea kabisa kama ungekuwa wa hivi japo ni wengi wanaumia pia!
Wengine tulishaona mapema sana kwamba hapa hamna strategy zaidi ya ujinga wa populism tupu.

Na wengi walioanza kwa kumuunga mkonowanashtuka.

Ila kuna watu mpaka leo huwaelezi kitu.
 
Miaka miwili ya utawala wake hakuna kikubwa alichofanya zaidi ya kuwagawa watanzania, ni vijembe tu kwa kwenda mbele.
Mpaka 2020 tutakuwa hatusalimiani na jirani zetu kwa ajili yake.
 
Naomba tujadili hii, ni kweli kuwa Watanzania tulikuwa tunautaka Utawala wa Namna ya Magufu?

Ni dhahiri huyu Mh. angependa katka Dunia hii abaki na wale wanao muunga mkono tu kila anayempinga amtoweshe. Je, ndicho tulikihitaji kutoka kwako?

Push up zote zile kumbe alikuwa anafanya ili atimize Matakwa yake ya hivi kutufanya wote tukose amani ndani ya Nchi yetu huru? Kuna faida gani ya Kusema Unawapenda Wananchi na huku Vitendo havishabihiani na yele Maneno yako!

Mh, nakuhakikishia Watanzania Walio wengi kama Siyo Wote wana hasira Vifuani mwao dakika yoyote wanaweza kupasuka. Hao wengine umaowatumikisha (Mwondoe Bashite) wote wanakwenda tu kwavile hakuna namna!

Nasikiti maisha yako baada ya Utawala huu! Sikutegemea kabisa kama ungekuwa wa hivi japo ni wengi wanaumia pia!
waliompigia kura ndio wa kuwauliza binafsi nilitarajia ndio mana sikumpa kura yangu!
 
Amefanya mengi na makubwa ya kuineemesha nchi nje ya matarjio hafifu ya wanyonge wa Tanzania.

Je hayo unayodhani ni makubwa ni yapi ya ajabu ambayo viongozi watangulizi wake hawakufanya mpaka yeye aone hafai kukosolewa? Je anadhani kupata urais kwa kura za walio wengi ni kwamba anaongoza watoto hivyo wote wanapaswa kukubaliana na anachokitaka yeye? Ni maisha gani yamebadilika kwa wanyonge hasa wakulima mpaka afanyie roho mbaya wale wanaotofautina naye kimitazamo?

Tukubaliane tu kwamba ana mazuri yake, lakini kwa kweli anaonyesha chuki za wazi zisizo na sababu. Mwaka wa kwanza mlimsifia sana, lakini sasa sifa mnazilazimisha kwani hazionekani kwenye maisha halisi ya wananchi. Tukio hili la kushambuliwa Lissu limewaacha wengi na hasa waliokuwa wanamuunga mkono na shaka kubwa ya uongozi wake hata kama watu hawawezi kuongea hadharani. Hili pia limekiacha chama chake katika hali ngumu kwani ni dhahiri sasa chama chake hakiwezi kujenga hoja tena zaidi ya vitisho, na hali hii ikiachwa huenda ikalivuruga taifa letu. Mchelea mwana kulia ...
 
Hakuna mtu Tanzania au Africa ya leo angetegemea Magufuli kufanya mambo anayoyafanya kila ninapokua nje ya nchi na kusema natokea Tanzania tofauti na zamani kitu wanachojua Tanzania ni "that country of Magufuli?"

Magufuli kaiweka Tanzania and Africa kwenye ramani ya dunia that's true that's it.

Hata Nyerere aliiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia kuliko Magu lakini tuliishia kuvaa viraka. Kuiweka nchi kwenye ramani ya dunia sio lazima iwe kwa mafanikio kwani hata Hitler aliiweka Germany kwenye ramani ya dunia. Je maisha ya watanzania walio wengi hasa wakulima wamefaidika toka aingie madarakani? Je kuiweka nchi kwenye ramani ya dunia ni lazima aeneze chuki ya wazi kwa wale wenye mitazamo tofauti na yeye au wasiomsifia. Kimsingi ana mazuri yake, ila ukumbuke hata viongozi wengine wa awamu zilizopita walikuwa na mazuri yao lakini hatukuona wakihubiri chuki ya wazi kwa wanaotofautiana nao kwani kutofautiana ni hali ya kibinadamu.
 
Binafsi nilitarajia kila kitu kwenda km hv vinavyokwenda maana nilikuwa nmemfatilia muda mrefu utendaji wake bwana yule toka waziri ndio maana baada ya kuapishwa tu mie na familia yngu nikahama nchi na bado nina hakika mpk nchi hiyo iwe km Zimbabwe ndio roho yke itatulia bwana huyo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa namuunga mkono baadhi ya mambo lakini nishaona uwezo wake mdogo. Hajui na hafanyi chochote kuboresha maisha ya watu. Yeye yuko busy na mambo ya AJABU AJABU ya kina LISSU, MANJI, IPTL nk

- Anaacha watu wengine wanateseka huku wengine wanalipana MIPOSHO YA LAKI 4 PER DAY!

N.B Kumchoka Zigo wa magogoni haimaanishi nawaunga mkono MIZIGO MIZITO YA UPINZANI
He is busy dealing with People and not Issues!
 
Back
Top Bottom