Je, utaratibu unaotumika kubadilisha laini ya kawaida kuwa ya 4G kwa mitandao mingime ni sawa na huu wa Halotel?

commm

JF-Expert Member
Sep 6, 2019
1,674
1,905
Habari za wakati huu,

Leo nilienda katika duka la halotel kubadilisha laini yangu kuwa ya 4G.

Sasa kutokana na simu janja yangu ninayoitumia ilikua ni ya laini moja ikabidi hii laini ya halotel niiweke kwenye simu ya hizi ndogo wengi wanaziita kiswaswadu kutokana na wakati huo nilikua sina matumizi nayo hasa kwenye upande wa data

Sasa kufika mapokezi ,mtoa Huduma nilimueleza shida yangu na yeye akanijibu kuwa ili kubadilisha hiyo laini iwe ya 4G ni lazima iwe kwenye simu inayosapoti 4G.

Ikabidi niitoe laini kwenye ile simu ndogo ili niiweke kwenye simu janja,Mara ananiambia hiyo laini inatakiwa ikae kwenye hiyo simu kwa muda wa wiki ndio itawezekana kubadilisha na kuwa ya 4G.

Je, kama huu ndio utaratibu wa Halotel,vipi kwa mitandao mingine maana nilipanga pia nikabilishe na laini yangu ya voda,lakini baada ya kuona kama utaribu ndio huu ilibidi tu nihairishe nisije nikapoteza muda wangu bure.
 
Mi niliambiwa Laini ya simu ikae kwenye simu masaa 24 ndipo itaweza kubadilishwa, so nikaiweka kwa hayo masaa ndo nikaenda kubadilishiwa.

Mitandao Mingine Kama Airtel na Voda hawana hayo mambo mi nilibadilisha zote bila masharti yoyote.
 
Swala la ku-upgrade/kuswap laini kwa mfano za tigo, halotel,na voda ni rahisi sanana haraka labda kwa wale wenye line za airtel ndiyo kuna ugumu kidogo. Kuswap ni swala la dakika chache mnoo.. hakuna gharama yoyote. Cha msingi ni.. laini yako unakayo hitaji kuibadili iwe ni grade chini ya 4G namaanisha 3G...
Lakini pili laini iwe imesajiliwa kwa mfumo wa alama za vidole yaani NiDA.
Screenshot_20200521-175622~2.jpg

Sent by mzawa
 
Swala la ku-upgrade/kuswap laini kwa mfano za tigo, halotel,na voda ni rahisi sanana haraka labda kwa wale wenye line za airtel ndiyo kuna ugumu kidogo. Kuswap ni swala la dakika chache mnoo.. hakuna gharama yoyote. Cha msingi ni.. laini yako unakayo hitaji kuibadili iwe ni grade chini ya 4G namaanisha 3G...
Lakini pili laini iwe imesajiliwa kwa mfumo wa alama za vidole yaani NiDA.View attachment 1455886

Sent by mzawa
Mkuu unataka kusema wewe umeswap mwenyewe?
 
hapana.mimi wiki jana nilienda kwa wakala ku apgrade laini yangu ya halotel ilikuwa kama ifuatavyo.

alikuwa ni wakala wa kwenye miamvuli.wakati ameingia kwenye app yake ya kusajili ikamwambia laini aipo kwenye cm inayo sapot 4g.

basi nikaitoa laini yangu kwenye kiswaswadu nikaiweka kwa cm yangu yenye uwezo wa 4g.

akarudia tena kusajili kwa muda uo ikakubali,kuna namba za otp za uthibitisho zikaingia kwa cm yangu nikamtajia akajaza baada kama dk 3 laini yangu ya 3g ya awali ikaandika invalid sim.
akanipa chip yangu ya 4g nikaanza kukata mawimbi muda huo uo.

sasa mimi nashangaa uyo muhudumu aliekwambia eti mpaka baada ya wiki?
ajui ama kakudanganya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa nasubiri kwanza sikukuu ipite maana wana mambo ya ajabu
 
Wamekuambia ivo ili utumie hiyo line tuu, lengo hapo wawe na wateja wengi walio active.

Kwenye kubadili line iwe ya 4G haihitaji hata uwe na simu yenye 4G/LTE. Sababu unapewa chip mpya ile ya mwanzo unaitupa.
Unforgetable

Manners Maketh Man
 
Back
Top Bottom