Je, Upinzani ni dhambi?

TAIFAKWANZA

Senior Member
Apr 20, 2013
160
61
Kupinga jambo ama hali ya mambo ilivyo kiuchumi,kijamii na /ama kiutamaduni ni kutokubaliana. Ni kukataa kwa kutoa mwelekeo mbadala wa jambo/mambo.

Anayepinga au tumwite mpinzani hutumia mbinu anuwai ktk kueleza na kufafanua kile anachodhani ni sahihi kwa jamii husika. Hotuba ktk mikutano na maandiko mbalimbali kwenye makaratasi na ki elektroniki ni baadhi ya njia atumiazo mpinzani. Jamii husikiliza na uamuzi wa nani yu sahihi kati ya anayepinga na anayepingwa ni haki na uhuru wa jamii husika

Upinzani huzaa UASI(rebellion). Kwa mawazo yangu, uasi ni matokeo ya UPINZANI (opposition) uliopuuzwa.
Anayepingwa hupuuza mawazo ya wanaompinga na kulazimisha asikilizwe yeye!

Kwa kuwa anayepingwa mara nyingi huwa na "nguvu" kuliko mpinzani wake,msigano wao kimtazamo humfanya mpinzani adhoofishwe na kuumizwa kwa kila namna na ikibidi auawe.

Hapa ndipo ndipo uasi huamua kuwa na sura ya kikatili na hapa rebellion huwa armed struggle!! Hapa ni machafuko!

Upinzani ni asili ya binadamu. Na kama ilivyo, uasi ni hulka ya binadamu.Biblia takatifu inatwambia kuwa mashetani walikuwa malaika. Walifukuzwa kwa uasi.Upinzani/uasi ni matokeo ya matumizi ya akili ktk kufikiri na kutafakari! Kama kufikiri na kutafakari si kosa,je kuwa mpinzani ni DHAMBI?

Adam na Eva walimuasi muumba wao na ndo maana mimi na wewe tunachuma matokeo ya upinzani/uasi wao!!
 
Back
Top Bottom