Je upepo ume geuka?

Je upepo ume geuka?

Killing machine

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2022
Posts
2,374
Reaction score
3,392
Sio kawaida kwani sio wanawake,sio wanaume,sio mabinti,Wala sio vijana wa kiume Wana sema hawataki

Mitaani Kuna minong'ono mizito na ubaya ukisogea karibu ili uiskilize vizuri Minong'ono hiyo hukoma na watu Wana tawanyika sjui kwanini?

Mitaa inazungumza kwa usiri na kujificha jificha Tena huzungumza kwa kujuana juana Kama utafika wasiye kujua mazungumzo ya mwanzo hukoma ghafra na kuanza kuzungumzia habari ya uchimbaji na uchomaji wa Dhahabu

Hii ni dalili kwamba sikuhizi watanzania Hawa aminiani wao kwa wao huenda wanajua Kuna kuuzana

Kuna Kila dalili kwamba watu Wana mengi ya kuongea Ila hawana pa kupumulia sijui wahusika Wana wasaidiaje ?

Kwakifupi watanzania Wana hasira Ila wamekosa ujasiri wa kuzitoa hasira zao kwani hawaijui hatima ya kesho zao kwao na kwa familia zao

Binafsi naiomba serikali yetu isiji kite kwenye kuwadhibiti watanzania wasiongee

badara yake ijikite kwenye kutatua Yale yanayo ongelewa na watanzania hii itasaidia Sana

Nguvu kubwa inayo tumika kuwa zuia watu wasiongee nguvu hiyo hiyo itumike kwenye kutatua magumu ambayo watu wanaya pitia na kuya zungumzia

Gharama kubwa ambazo Zina tumika kwenye kuzuia maandamo kutawanya watu nk

Gharama hizohizo zitumike kwenye Mambo ya msingi yanayo wagusa watanzania moja kwa moja Kama maji kwenye mini yetu,dawa kwenye hospital zetu,kukamata mafisadi na Wala lushwa ,usawa kwenye vyombo vya Dora na Sheria nk

Kuna wakati staki kuamini kwamba serikali yetu Haina watu wenye busara wa kulimaliza hili Bila virungu,mapanga,au risasi na mabomu

Mpaka najiuliza hivi je! niupepo tu umebadilika?

Ukaidi huu na kuto kuskia huku kwa viongozi wetu kunani kumbusha nyakati za biblia nyakati ambazo farao alifanywa kuwa mgumu kwa makusudi na mungu ili kusudi la mungu litimie

Je mungu kaifanya serikali yetu iwe kiziwi/kipofu kiasi kwamba haioni what is next ili kusudi lake litimie?

Kwa maana ukimya huu na kiburi hiki cha serikali yetu juu ya maswali ya watanzania kwa serikali yao sio bule

Kuna kila dalili kwamba ng'ombe wanampango mbaya juu ya mfugaji wao atakapo enda kuwa chunga machungoni kesho hasuhi

Hekima imlinde na busara imuongoze mfugaji yule🙏🙏🙏
 
shutterstock_61229197-1024x682.jpg
 
Back
Top Bottom