Je ungekuwa wewe ungefanyaje ???

Je ungekuwa wewe ungefanyaje ???

NITIKE NDOSI

Senior Member
Joined
Jan 15, 2013
Posts
153
Reaction score
86
Mambo niaje wana MMU
Mwenye majibu na hii kitu naomba anisaidie.
Nina jamaa yangu ambaye ni marafiki wa muda mrefu sana,tangia tunakua na mpaka sasa na midevu yetu.
Ni mara nyingi ananitaarifu kuwa girl friend wake ananisifia sana
eti utasikia;
''yule jamaa yako ni mpole!!!''
''hivi amewahi kugombana na watu kweli!!!''
''mimi mnapokuwa wote najisikia raha na story zake''
''atapata raha mke wake''
Sasa kitu kilichonifanya ni shituke ni pale tunapokuwa wote watatu naona concetration zake kubwa huwa kwangu
kuliko boyfriend wake.

USHAURI WENU TAFADHALI.........
 
Shtuka,ebu imagine we ndo rafiki yako afu demu wako ndo anakuwa na such attitude kwa best friend wako utahisi nini?ukishajua utahisi nini utajua hatua ya kuchukua.
 
Unataka ushauri gani? Tukwambie umgegede?
 
Angalia huyo msichana asije akawa chanzo cha kuvunjika kwa urafiki wenu!
 
Huyo msichana ni kahaba hana lolote atawagombanisha, usimpe nafasi!
 
mgegede bwana sii anakutaka mwenuewe lol

I concur!
kwani hata wa kwake akileta tabia hizo unafikiri ataachwa kugegedwa!
Huyo amemzimia yeye kama vile yule wa kwake atakavyomzimia mshikaji wake. GEGEDA!
Dunia imeshakuwa tambara bovu bana:target:
 
Sidhani kama ni jambo baya kama girlfriend wa rafiki yako akikusifia! Kama kweli sifa hizo unazo yeyote tu angekusifia ILA....

Kama unahisi(ukweli unaujua mwenyewe) kama kuna zaidi ya hizo sifa(anakutaka), na pia wewe na rafiki yako ni 'best' friends nakushauri yafuatayo;

1. Mwambie mshkaji wako kuwa girl friend wake anavyokusifia(ukijua anakutaka) haufurahii
2. Mwambie girlfriend wa mshkaji wako kuwa(kama anakutaka) haitawezekana na haujisikii vyema anavyokusifia.

Kama kweli msichana anakutaka na ukaamua kukaa kimya yafuatayo yanaweza kutokea;

1. Mshkaji ataona mienendo mibaya na atakuwa na udadisi na atahisi unamtaka girlfriend wake, mtagombana
2. Utaingia 'KING' siku moja na kufanya kitu utakachojuta maisha yako yote.

Kama msichana anakusifia kawaida tu(unaujua ukweli) mueleze kiupole kuwa si jambo zuri kukusifia sana wewe maana hata yeye angekuwa na rafiki wa kike halafu boyfriend wake(mshkaji) anamsifia sana angejisikiaje?

NAtumai nimesaidia
 
Usitutake tukueleze cha kufanya. Kama we mtoto ulifikaje humu?
Kesho mkeo akifanya kama unavyofikiria unaanza kulalama. Kumbuka mtenda hutendwa na anapotendwa hujihisi kaonewa.
 
usitutake tukueleze cha kufanya. Kama we mtoto ulifikaje humu?
Kesho mkeo akifanya kama unavyofikiria unaanza kulalama. Kumbuka mtenda hutendwa na anapotendwa hujihisi kaonewa.
hapo hujashauri kitu mkuu!!!!
 
Mambo niaje wana MMU
Mwenye majibu na hii kitu naomba anisaidie.
Nina jamaa yangu ambaye ni marafiki wa muda mrefu sana,tangia tunakua na mpaka sasa na midevu yetu.
Ni mara nyingi ananitaarifu kuwa girl friend wake ananisifia sana
eti utasikia;
''yule jamaa yako ni mpole!!!''
''hivi amewahi kugombana na watu kweli!!!''
''mimi mnapokuwa wote najisikia raha na story zake''
''atapata raha mke wake''
Sasa kitu kilichonifanya ni shituke ni pale tunapokuwa wote watatu naona concetration zake kubwa huwa kwangu
kuliko boyfriend wake.

USHAURI WENU TAFADHALI.........


Kwa sababu ameshonesha dalili. Mtongoze.
 
Anakutaka huyo! sasa bro akili kumkichwa, kuvunja urafiki umgegede huyo manzi au kuwa mbali kabisa na manzi kulinda urafiki wenu.
 
Huwa navunja ukimya namwambia! Nakutaka straight, then nimskie akakataa ndo basi akikubali pia the same, kiufupi hafai huyo! watu tunalingana na kila leo mbora zaidi atatokea, so lazimaawe na mapenzi ya kweli kwa mmoja na si kujishebeduashebedua
 
Kwani ukisifiwa unakua umependwa? Ndugu endelea kumuheshimu shem wako na rafiki yako.
 
mpe mtu sifa zake alizonazo ni haki yake. Inawezekana anakusifia kawaida tu ila wewe ukawaza mbali zaidi. Wewe kwa kuwa umehisi kitu na hutaki itokee ishu mbaya yoyote, basi kuwa nae makini na usimzoee saaaana maana itakugharimu utaishia kusema shetani alinptia.
Unaweza kumwambia kuwa asikusifie sana, af akakugeuzia kibao unamtaka ikawa noma zaid. We ni mwanaume nenda nae kwa akili tu.
 
Back
Top Bottom