Je ungekuwa wewe ungefanyaje ???

Je ungekuwa wewe ungefanyaje ???

Kwa akili ya kawaida, anavutiwa sana na wewe labda hata kuliko huyo aliyenaye anaogopa tu kukutamkia moja kwa moja lakini picha iko wazi.

Pili, Huyo dada hajui nini cha kusema na wapi pa kukisemea.

Tatu, Usiwe karibu saaaana nae shemejio, Mpe heshima sana. cause ikitokea rumour kuwa watembea naye, itakuweka kwenye nafasi ngumu kukanusha kwa jamaa yako.

Nne. Sitisha huo mpango wako, maana hiyo background uliotoa ya urafiki wenu ni kana kwamba unataka kumuwahi lakini urafiki wenu upo at stake. hata wakiachana, jiweke pembeni na huyo binti.

Sidhani kama ni jambo baya kama girlfriend wa rafiki yako akikusifia! Kama kweli sifa hizo unazo yeyote tu angekusifia ILA....

Kama unahisi(ukweli unaujua mwenyewe) kama kuna zaidi ya hizo sifa(anakutaka), na pia wewe na rafiki yako ni 'best' friends nakushauri yafuatayo;

1. Mwambie mshkaji wako kuwa girl friend wake anavyokusifia(ukijua anakutaka) haufurahii
2. Mwambie girlfriend wa mshkaji wako kuwa(kama anakutaka) haitawezekana na haujisikii vyema anavyokusifia.

Kama kweli msichana anakutaka na ukaamua kukaa kimya yafuatayo yanaweza kutokea;

1. Mshkaji ataona mienendo mibaya na atakuwa na udadisi na atahisi unamtaka girlfriend wake, mtagombana
2. Utaingia 'KING' siku moja na kufanya kitu utakachojuta maisha yako yote.

Kama msichana anakusifia kawaida tu(unaujua ukweli) mueleze kiupole kuwa si jambo zuri kukusifia sana wewe maana hata yeye angekuwa na rafiki wa kike halafu boyfriend wake(mshkaji) anamsifia sana angejisikiaje?

NAtumai nimesaidia
 
Mambo niaje wana MMU
Mwenye majibu na hii kitu naomba anisaidie.
Nina jamaa yangu ambaye ni marafiki wa muda mrefu sana,tangia tunakua na mpaka sasa na midevu yetu.
Ni mara nyingi ananitaarifu kuwa girl friend wake ananisifia sana
eti utasikia;
''yule jamaa yako ni mpole!!!''
''hivi amewahi kugombana na watu kweli!!!''
''mimi mnapokuwa wote najisikia raha na story zake''
''atapata raha mke wake''
Sasa kitu kilichonifanya ni shituke ni pale tunapokuwa wote watatu naona concetration zake kubwa huwa kwangu
kuliko boyfriend wake.

USHAURI WENU TAFADHALI.........

Amependezwa na wewe zaidi ya mchumba wake, Linda mahusiano ya watu maana kuna wengine wanaamua kutumia chance kama hizo kuwapata wanawake wa marafiki zao, Ila kwa mtu mwenye busara atamzoea tu kama shemeji na hataendeleza mahusiano. Kinachohitajika ni respect. Also may be huyo rafiki yako alivyo hajamridhisha huyo mwanamke may be katika tabia (upole), n.k Just be good.
 
hamna swali hapo kaka majibu unayo........ili kulinda heshima yako punguza muda wa kuwa na rafiki yako anapokuwa na gf wake,....
 
Jamani mtanzania ni mtanzania tu kusifiwa kidogo tu imeshakua topic, si ajabu mwenzio wala hana time hua anakusifia kama shemeji tu sasa kwa vile na wewe unamtaka basi unaenda mbaaalii..khaaa!
 
2 options.

1. Mkule

2. Mwambie ajiheshimu, wewe no shemeji yake aache kukumezea mate, alaaaaaa

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom