Je unaweza kusamehe na kusahau?

Je unaweza kusamehe na kusahau?

kusahau ina tegemea na tukio lenyewe vipi ulivo lipokea ila kusameh ni swala la imani ya mtu mwenyewe,alivo lelewa na mazingira anayo ishi-
 
Kuna vitu vingine huezi kabisa kusamehe na kusahau especially ukisalitiwa na mtu ulie muamini(kuchepuka) yaan hii kila mda utakumbk then upate hasira

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kikulacho kiunguoni mwako.

Wahenga wala hawajakosea kwa msemo huo.

Siku zote yule Mtu unaemwamini na una nia nae njema ya kusaidiana nae Kimaisha ndie atakaekuangusha.

Hapa sikusudii ya kuwa hakuna kabisa Waliowaaminifu.

La Hasha, ninachokusudia hapa ni kutokana na mifano hai niliyoiona Mimi mwenyewe kwa Macho yangu.

Watu wameangushwa kimaisha na watu wao wa karibu ambao waliwaamini sana
 
Cha Muhimu ni kusahau, na kusonga mbele.

Yaani inawezekana sana
 
Na Mtu anaekuangusha ujue anakupa Ukakamavu na Ujasiri, na pia anakufundisha.

Pamoja inauma sana, ila ni kwa Muda tu.

Itafikia Wakati utasahau kabisa
 
Kusamehe hakumaanishi usahau. Ila kusamehe kweli kunakufanya usiuhisi tena uchungu na maumivu ya lile kosa ulilotendewa pale unapokumbuka!
 
Naweza kusamehe, kusahau siwezi.. aliyenikosea nikamsamehe imani yangu kwake inaporomoka kwa kiwango cha hali ya juu..
 
Ktk ile Sala ya Baba yetu uliye Mbinguni...... Kuna kuomba msamaha pake kuna "conditional " Kwamba tusamehe makosa /dhambi zetu "kama sisi nasi tunavyowasamehe waliokukosea" kwahiyo hicho ndo kipimo cha Sisi kusamehewa na Mungu Kwa kadri tunavyosamehe waliotukosea! Ndo maana wenye ufaham wa Neno husema" nimekusamehe Kwa ajili yangu mwenyewe Au Kwa faida yangu mwenyewe" ni ngumu kibinadam kusamehe lakini kuna faida ktk kusamehe! Tena ikibidi watafute ongea nao Kwa upendo wa Kristo waelewe jinsi ulivyoumia kisha watangazie msamaha!
 
Imeandikwa "jua lisichwe tungali na uchungu Moyoni " uchungu/hasira zikijikusanya na kukaa moyoni Kwa muda mrefu wengine hupelekea kuugua /kuumwa! Wengine wamelazwa mahospitalini ukifuatilia utagundua chanzo cha tatizo ni kutokusamehe! Imeandikwa " Linda sana moyo wako kuliko yote ulindayo maana huko ndiko zitokazo chemchem za uzima" pia tafuteni kuwa na amani na Watu wote na huo utakatifu ambapo hakuna atakaemwona Mungu pasipo huo"
 
Na kiukweli pasipo kujifunza na kuruhusu Pendo la Kristo kufurika ndani yako kusamehe itakuwa ni vigumu Kwa Mtu ! Nakusihi samehe kaka na utashangaa jinsi mambo yako mengi yatakavyo fungukuka Kwa wepesi wa hali ya juu!
 
Sameheni kwa kadri muwezavyo lakini msisahau kila mara.
Kuna baadhi ya vitu ni vya kukumbuka ili msije kuumizwa tena, lakini vingine havitakiwi hata kukumbukwa pia kwa maana haitosaidia.
 
Wasamehe lakini usisahau Ili iwe fundisho kwako
 
Mungu anajali Sana uhusiano kati ya Mtu na Mtu! Hata Bwana wetu Yesu Kristo alipokuwa akikua ktk mwili imeandikwa alikuwa "akimpendeza Mungu na Wanadamu" ni muhimu sana kuwa na uhusiano mwema na Watu jamani! Imeandikwa hata sadaka yako usitoe hadi ukapatane na Yule unaewiwa nae" samehe sijui Wewe ni dada Au kaka
 
Naweza kusamehe, kusahau siwezi.. aliyenikosea nikamsamehe imani yangu kwake inaporomoka kwa kiwango cha hali ya juu..
Mkuu uko kama mimi. Ni mwepesi wa kusamehe ili nisitembee na sumu yaani chuki moyoni mwangu. Baada ya kusamehe nakuwa makini sana na huyo mtu kwani nakuwa simwamini tena kwa kiwango cha awali. Kuhusu kusahau ni ngumu. Hii ni kwa sababu kutosahau siku zote kutanisaidia kuniongoza katika kuwa makini na huyo mtu.
 
Back
Top Bottom