Je, unaweza kumaliza tamaa kwa kudhibiti au kuomba?

Nov 2, 2023
60
50
Kutamani ni hisia ambayo tumeumbwa nayo na haipo kimakosa miilini mwetu.

Binadamu aliyekamilika lazima atazalisha hisia yoyote ile kutokana na anachokutana nacho kama njia moja wapo ya mawasiliano na mwili wake. Na hakuna hisia yoyote kwenye mwili isiyo na maana kwako.

Kwanini hisia ya kutamani inakuwa tatizo kwetu. Tunashindwa kuielewa na inatusababishia matokeo mengi tusiyo yatarajia. Hisia ya kutamani ikikuongoza na ukishindwa kuitambua itakupelekea kufanya mamuzi mengi yatayokuletea majuto na madhara badae. Kwanini iwe hivi, ni jinsi tulivyo tamaa tumeumbiwa itutese maishani mwetu ama kunasehemu hatujaelewa kuhusu utendaji wa akili na miili yetu.

Kwa kujua madhara ya tamaa tumeishi kwa mazoea ya kuidhibiti tamaa kwa kutumia nguvu ya kifikra na kusababisha mkanganyiko wa kiakili na utumizi wa nishati isivyopaswa. Wakati unajaribu kuidhibiti tamaa kwa kufikiri kimawazo ni kama unaisajili akilini mwako na haitoisha kuja unapokutana na mazingira yanayoendana na hiyo tamaa kwa jinsi ilivyokuja.

Kuomba kama njia ya kumaliza tamaa yako haitosaidia kumaliza mzizi wa kusumbuliwa na tamaa. Kuomba kunatumika kama njia ya kukusahaulisha au kupunguza umakini kwenye hiyo tamaa yako kwamuda si kukupa ufahamu na utambuzi utaomaliza jambo hilo kabisa na kuwa si tatizo kwako.

Kama hisia si tatizo letu sasa tamaa inakujaje kuwa tatizo. Wakati tukiwa kwenye tukio linaloanzisha tamaa ufahamu wetu unapaswa uwe juu kwa kuwa na uelewa ambao ni nafasi kati ya mawazo yetu yanayotengeneza ubinafsi ambao huwa ni mafuta kwenye kuipa nguvu tamaa ya kuchanua na kuleta madhara. Unawezaje kuimaliza tamaa kabla haija chanua na kukushambulia.

Tamaa inachochewa na mawazo ya ubinafsi, ukiweza kuwa na gepu kati ya ufahamu wako na mawazo yako hutoweza kuendeleza kutengeneza picha ya kitu akilini mwako ambayo ndio huwa tatizo kubwa linalopelekea kudhurika.

Tamaa ni kama wingu linalopita akilini mwako ufahamu wakulitambua na kuliacha lipite na lipotee bila kufanya chochote hiyo nidhamu ya kujitambua ndio suluhisho la kutoa mzizi wote wa tamaa na haitokuwa tatizo tena kwako. Ukiwa kwenye hali yoyote inayokuletea tamaa usijaribu kuikubali au kuipinga kuwa makini nayo tu. Fanya kama ni kitu usichohusika na maamuzi nacho, na pale unafsi wako unapojitoa kwenye hilo na tamaa hunyauka muda huo huo na kupotea.

Nb: Tamaa yoyote ile haikumanishi wewe ndivyo jinsi ulivyo, akili yetu inafanya kazi zaidi ya matakwa yetu kwa jinsi tunavyoishi. Usijichukulie kijidharau unajihitaji tu ufungue mlango wa ufahamu ndio uwe mwongozo wako kwenye maisha na si mawazo yako pekee.
 
Back
Top Bottom