Tamaa mbaya

Amani Dimile

JF-Expert Member
Jul 27, 2022
243
395
Unakumbuka kipindi ambapo wazazi wako walikuwa wakikukanya kuomba au kulilia chakula cha mgeni. Unakumbuka nini kipindi kile ambapo hukutakiwa kabisa kumtazama mgeni usoni kipindi anakula au anakunywa soda yake.

Au umesahau kuwa ulifinywa sana, ukapigwa vibao na kuchapwa fimbo za kutosha kipindi ambapo mgeni alipokuwa akila basi wewe ukathubutu kukaa pembeni yake kumtazama.

Vipi, kuna muda mayai kwenu hayakupikwa miezi na miezi ila mgeni akija alikuwa akikaangiwa na kuwekewa mezani. Sasa ukitaka kujua kipi kilimkuta cha Mtemakuni, basi omba au mgeni akupe upokee. Heeee!

Ok. Unakumbuka nini pale ambapo ulilazimishwa kusema "nimeshiba" hata kama una njaa kiasi gani, pindi tu jirani au ugenini ukaulizwa kuwa una njaa. Ulikuwa ukidanganya kuwa umeshiba ili tu kutii amri ya mzazi kuwa "hakuna kula ugenini"

Wazazi wetu walikuwa na akili sana. Tena sana. Walikuwa wakitufunza kuzuia kitu kinaitwa TAMAA.

Tamaa ni mbaya sana wanangu na ndio maana wazazi wetu tangu udogoni mwetu walikuwa wakitupandikiza mbegu ya kujizuia juu ya tamaa.

Mwanadamu atafanikiwa kimaisha ikiwa ataweza kuvizuia vitu vitatu katika mwili wake. 1. Mdomo 2. Tumbo na 3. Sehemu zake za siri. Ukiweza kuviongoza hivyo viungo vitatu basi utakuwa umefanikiwa kimaisha.

Katika dunia hii ya dhambi na maafa, epuka sana kuwa na hisia za tamaa juu ya vitu ambavyo huna. Kumbuka malezi yako ya utotoni. Yaani jizuie sana na tamaa, tamaa mbaya, tamaa mbaya, tamaa mbaya, tamaa mbaya narudia kwa mara ya mwisho tamaa mbaya. KUWA MAKINI.

Nyerere aliwahi kusema "tamaa na heshima havikai nyumba Moja" jifunze kuwa na kikomo. Tamaa na maagizo ya Mungu havipatani, epuka.Tamaa itakufanya upite njia za haramu bila wewe kujua, utafanya mengine nje ya maadili mema kisa tu uchu na tamaa.

Tamaa itakufanya upige magoti mbele ya wadhalimu. Jitahidi uongoze tamaa yako, jizuie. Jitahidi uwe na uwezo wa kusema hapana mbele ya mambo ambayo kiuhalisia unaweza kuyavumilia hata kama moyo wako jibu lake ni ndio.

Hapa mjini hakuna cha bure, watu wanavitolea jasho vitu vyao sasa we ukitanguliza tamaa mbele basi jua mauti ipo nyuma inakusubiri.

Wanadamu wana tabia mbaya sana, wakijua tu udhaifu wako basi wanautumia ipaswavyo. Wakijua tu una tamaa basi wanakutumikisha mpaka ukome. Epuka kuonesha udhaifu wako, jizuie tamaa ni mbaya. TAMAA MBAYA. TAMAA MBAYA

Kama hujanielewa, basi nisamehe kwa kuongea pumba ila endelea kuwa na tamaa utakuja kunielewa tayari wadau wakiwa wanapaka mafuta

Amani Dimile
IMG-20240117-WA0042.jpg
 
Uzi mzuri, Ila wanawake ndo viumbe ambao tamaa zimewashinda kabisa kuzizuia... Ukiwa na ndoano moja ukaweka chambo cha wekundu wa msimbazi unavua wanawake idadi ambayo wewe ndo utaichoka na kuamua kupumzika.
 
Wazazi wenu walikua maskini.

Mzazi mwenye pesa atamlisha mtoto hivo 'vitu vitamu', mtoto hatobabaishwa na vya watu au vya wageni.

Halafu kupamba wageni ni tabia ya kipumbavu sana.

Ila kweli tamaa mbaya.
una mtoto? rafiki yangu hata kama utampa mtoto kila kitu kuna baadhi ya vitu anatakiwa kuishi navyo, hawez mgeni aje akipeleka soda mdomon mtoto anasindikiza na macho na mzazi upo unaangalia au weye ndio baba junio? mtoto hakatazwi chochote sawia marhaba
 
Wazazi wenu walikua maskini.

Mzazi mwenye pesa atamlisha mtoto hivo 'vitu vitamu', mtoto hatobabaishwa na vya watu au vya wageni.

Halafu kupamba wageni ni tabia ya kipumbavu sana.

Ila kweli tamaa mbaya.
Unawajua watoto mkuu, ndivyo walivyo.
Mzazi hata kama una pesa ia inabidi ucontrol tamaa ndogondogo za mwanao.
Atataka kila kitu, na hii sometimes inamjengea tabia mbaya ya kutaka kila atakachotamani awe nacho hata kama hatokitumia.

Ni kweli tamaa ni mbaya.
 
Back
Top Bottom