Je, unawakumbuka hawa?

Je, unawakumbuka hawa?

MAFUNZO

Member
Joined
Sep 4, 2012
Posts
47
Reaction score
29
vijana.png
Baada ya wadau kuchangia changia picha hii, nitawaletea story na surprise fulani kwa wadau wa jamii forum. Sana sana kwa wale enzi za miaka ya 1980 mpaka 1990 hivi.
 
Watakuwa Vijana Jazz hao, kuna sura naziona kama Maneti na Kalala.
 
Naanza kwa Surprise. Surprise yenyewe ni wimbo. Je, wimbo huu unakukumbusha wapi? Baadaye nitamwaga story za enzi hizo. Keep in touch.

Nyimbo za wakati huo, zilikuwa na mafunzo mengi sana. Kuna wimbo mmoja ulioimbwa na vijana jazz uliitwa " ilikuwa lift" Katika wimbo huo......inaonesha jamaa alichanganyikiwa baada ya kumuona mke wake yuko na jamaa mwingine kwenye gari la mkewe........Soma mashairi ya wimbo huo ufaidi mambo ya zama hizo. Je, unakukumbusha nini?

ILIKUA NI LIFTI TU


Haikua jambo baya kwangu
Kwa yule kijana kumpatia lifti
Kama unavyohamu yapata wiki ya tatu
Gari langu lina matatizo ya kuzimikazimika ooo Mume wangu eee

Kutoka nyumbani Oyster Bay kufika Salender
Gari langu lilinizimikia eeee
Yule kijana alinisaidia kusukuma Mume wangu eee ooo ooooo oooooo

Kilichonishangaza sio lifti Mama Watoto
Ni tabasamu na vicheko mlivyokuanavyo ndani ya gari
Nilichanganyikiwa midomo ilianza kunicheza
Mithili ya mtu aliyemeza kipande cha moto Mama watoto
 
Hao ni Vijana Jazz na utunzi wa Hamza Kalala 'Commando' in 1985. Kwa kweli Tz tuna wanamuziki wazuri sana ila bahati mbaya wenye maredio na madj wanataka kutuulia muziki wetu wa asili na kutulazimisha kusikiliza karaoke (bongo fleva).
 
Back
Top Bottom