Je, unavijua viatu vya Oxford vinavyovaliwa dunia nzima?

uvugizi

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,235
874
Kiatu cha OXFORD (the oxford shoes) ni viatu ambavyo vimetokea kupendwa dunia nzima , vikitofautina kidogo na DERBY SHOES .

Sehemu ya kwanza kuonekana aina hii ya viatu ni Scotland na Ireland , enzi hiyo wakiita Balmoral shoe , kuipa heshima jumba la malikia wa UK na jumba lake la BALMORAL CASTLE.

Mpaka sasa hakuna mtu aliyethibitika kuleta fashion hii ya viatu , ingawa inasadikika baada ya kuwepo chuo kikuu cha oxford kilipata umaarufu mkubwa na kupewa jina hilo . vijana wengi walichoshwa na uvaaji wa strap boot wakataka half boot( the oxford).

Mabadiliko ya boot yamepelekea kupatikana kiatu cha the oxford ,, vijana walitaka ankle ionekane na kisiwe na kisigino kirefu na lacing fupi, kama strap boot ( chunguza picha za wakoloni enzi hizo ilikuwa ni strap boot shoes , tazama picha ya livingstone na burton Stanley).

Kabla ya kutoka kiatu hichi cha oxford , hapo awali kulikuwa na kiatu cha aina ya boot ( strap boot) , unafunga mikanda/ zipu mpaka juu ya ankle za miguu chini ya magoti. Strap boots ilikuwa imeletwa na mfalme wa ufaransa Louis xiv ……. Kumbuka ufaransa ndiyo ilimeza tamaduni yote ya ulaya ( cultural epicenter in Europe ).

Utajuaje au kitu gani kinatofautisha the oxford shoes na viatu vingine ni kamba (lacing) zake siyo ndefu sana na kisigino kifupi na hakijashonwa kwa juu yaani chini ya laces kama DERBY SHOES.

Tanzania hata leo watu wanaovaa oxford shoes naweza hata kusema ni 80% kwani ndiyo viatu vinavyovaliwa na wanasiasa , watu wa kada zote na hakijawahi kupitwa na wakati zaidi ya kuongeza marembo tu. Kiatu hichi kinavaliwa na nguo yeyote

Katika maandiko matakatifu biblia kuvaa viatu ni heshima , kutovaa ni kutoheshimiwa na kuaibishwa , soma isaya 20:2-5 . vaa viatu vizuri ukithibitisha heshima na kukubalika kwako na bwana, laana ikikushika nguo na viatu unatupa .

kihiga@zoho.com
 

Attachments

  • OXFORD SHOES.jpg
    OXFORD SHOES.jpg
    30.4 KB · Views: 84
Back
Top Bottom