Kampuni ya Nike yafungua kesi kwa madai ya kuibiwa chapa ya Viatu vya shetani

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
13,759
20,153
Kampuni ya Nike inashitaki ubunifu wa kampuni ya MSCHF iliyopo Brooklyn juu ya uzinduzi wa kile kinachosemekana kuwa “Kiatu cha shetani” chenye tone la damu ya kweli ya binadamu kwenye soli za viatu.

117751674_satan-shoes1.jpeg
Viatu hivyo vinavyouzwa kwa dola 1,018 sawa na (Tsh 2358910.76), ambavyo vimechorwa alama ya msalaba iliyopinduliwa na pentagramu (nyota ya ncha tano katika duara) na maneno “Luka 10:18”, vimetengenezwa kwa kuboresha muundo wa kiatu cha Nike Air Max 97s.

Kampuni ya MSCHF ilitoa jozi ya viatu 666 Jumatatu ikishirikiana na mwanamuziki Lil Nas X na kusema kwamba vyote viliuzwa chini ya dakika moja.

Kampuni ya Nike imedai kuingiliwa kwa chapa au alama ya biashara ya kampuni yake.

Viatu vya rangi nyeusi na nyekundu “vilivyotolewa” na kampuni ya MSCHF Jumatatu, kulikwenda sambamba na uzinduzi wa nyimbo mpya ya mwanamuzi Lil Nas X ya Montero ya (Call Me By Your Name), ambayo ilitolewa kwa mara ya kwanza kwenye mtandao wa YouTube Ijumaa iliyopita.

Katika video ya muziki huo, mwanamuziki huyo wa rapa anateleza kwenye mlingoti kutoka peponi au mbinguni hadi jehanamu au motoni, akiwa amevaa viatu hivyo.

Taswira na hiyo na viatu ambavyo vimeandikwa andiko la Bibilia Luka 10:18 – “Akawaambia, ‘Nilimuona shetani akianguka kama radi kutoka mbinguni’.”

Kila kiatu kina soli maalum ya muundo wa kampuni ya Nike yenye sentimita za ujazo 60 za wino mwekundu na tone la damu ya binadamu, ambayo ilichangiwa na wanachama wa kampuni hiyo.

Kampuni ya Nike ambayo ni maarufu kwa viatu vya michezo imesema kuwa katika kesi yake iliyowasilishwa kwenye mahakama moja mjini New York, kuwa haiidhinishi au kuruhusu utengenezaji wa ‘Viatu vya Shetani’.

Lil Nas X and MSCHF's Satan Shoes sold out in less than a minute on Monday

Viatu vya shetani vilivyozinduliwa na Rapa Lil Nas X kwa ushirikiano na kampuni ya MSCHF viliuzwa vyote chini ya dakika moja Jumatatu

Kampuni ya Nike inataka mahakama kusitisha kampuni ya MSCHF kuuza viatu hivyo na pia kuwazuia kutumia nembo yao ya muda mrefu maarufu kama ‘Swoosh’.

“Kampuni ya MSCHF na viatu vyake vya shetani ambavyo havijaidhinishwa kuna uwezekano mkubwa kukasababisha mkanganyiko na dhana fulani na kutengeneza fikra mbaya kati ya bidhaa ya kampuni ya MSCHF na kampuni ya Nike,” Kampuni hiyo ya utengenezaji viatu vya michezo imesema katika kesi yake iliyowasilisha.

“Kwanza, tayari kuna ushahidi wa kutosha unaoonesha mkanganyiko na dhana potofu sokoni, ikiwemo simu zinazotaka watu kususia bidhaa za kampuni ya Nike kufuatia uzinduzi wa viatu vya shetani vya kampuni ya MSCHF, ambavyo inaonekana kana kwamba kampuni ya Nike ndiyo ambayo imeidhinisha na kuruhusu utengenezaji wa bidhaa za hiyo.”

Kesi iliyowasilishwa inarejelea ujumbe wa mtandao wa Twitter uliotumwa na mshawishi mkubwa wa viatu saint Ijumaa iliyopita, ambao ulianza kuarifu wateja wake kuhusu kuzinduliwa kwa viatu hivyo na kuvipa umaarufu zaidi kwa umma wikendi kwenye mtandao wa kijamii na hata vyombo vya habari vya Marekani.

Baadhi ya wenye msimamo mkali akiwemo gavana wa Dakota Kusini Kristi Noem, na wafuasi wengine wa kidini, wameshutumu viatu hivyo vyenye utata na kumkosoa rapa Lil Nas X na kamupuni ya MSCHF kwenye mtandao wa Twitter.

Hata hivyo, Lil Nas X alimjibu gavana huyo pamoja na viongozi wa kidini kwenye mtandao wa Twitter, na Jumatatu katika mtandao huo, kulikuwa na vibonzo vya mzaha kwenye wasifu wake baada ya kampuni ya Nike kusema kwamba imechukua hatua ya kisheria.

Yaah habari haieleweke eleweki....nadhan huo ushetani wanaoupigania ndo maana sijaelewa. Dam inatengeneza kiatu?
 
Ushetani kwa 100%
1) kwanza huyo msanii anayetangaza ni Gay

2) Tone la damu chini ya Soli ya kiatu nadhani mnajua maana ya kukanyaga tone la damu au damu yenyewe

3) Namba 666 mnajua inamaanisha nn ambayo kwao ndio ilikuwa jumla ya viatu vilivyotolewa.

4) Hyo chata ya nyota 6 mbele ya Kiatu ni ishara ya ufree mason

5) Boksi linalobeba viatu lina charter ya Free mason pia.
 
Kampuni ya Nike inashitaki ubunifu wa kampuni ya MSCHF iliyopo Brooklyn juu ya uzinduzi wa kile kinachosemekana kuwa "Kiatu cha shetani" chenye tone la damu ya kweli ya binadamu kwenye soli za viatu.

Viatu hivyo vinavyouzwa kwa dola 1,018 sawa na (pauni 740), ambavyo vimechorwa alama ya msalaba iliyopinduliwa na pentagramu (nyota ya ncha tano katika duara) na maneno "Luka 10:18", vimetengenezwa kwa kuboresha muundo wa kiatu cha Nike Air Max 97s.

Kampuni ya MSCHF ilitoa jozi ya viatu 666 Jumatatu ikishirikiana na mwanamuziki Lil Nas X na kusema kwamba vyote viliuzwa chini ya dakika moja.

Kampuni ya Nike imedai kuingiliwa kwa chapa au alama ya biashara ya kampuni yake.

Viatu vya rangi nyeusi na nyekundu "vilivyotolewa" na kampuni ya MSCHF Jumatatu, kulikwenda sambamba na uzinduzi wa nyimbo mpya ya mwanamuzi Lil Nas X ya Montero ya (Call Me By Your Name), ambayo ilitolewa kwa mara ya kwanza kwenye mtandao wa YouTube Ijumaa iliyopita.

Katika video ya muziki huo, mwanamuziki huyo wa rapa anateleza kwenye mlingoti kutoka peponi au mbinguni hadi jehanamu au motoni, akiwa amevaa viatu hivyo.

Taswira na hiyo na viatu ambavyo vimeandikwa andiko la Bibilia Luka 10:18 - "Akawaambia, 'Nilimuona shetani akianguka kama radi kutoka mbinguni'."

Kila kiatu kina soli maalum ya muundo wa kampuni ya Nike yenye sentimita za ujazo 60 za wino mwekundu na tone la damu ya binadamu, ambayo ilichangiwa na wanachama wa kampuni hiyo.

Kampuni ya Nike ambayo ni maarufu kwa viatu vya michezo imesema kuwa katika kesi yake iliyowasilishwa kwenye mahakama moja mjini New York, kuwa haiidhinishi au kuruhusu utengenezaji wa 'Viatu vya Shetani'.

Kampuni ya Nike inataka mahakama kusitisha kampuni ya MSCHF kuuza viatu hivyo na pia kuwazuia kutumia nembo yao ya muda mrefu maarufu kama 'Swoosh'.

"Kampuni ya MSCHF na viatu vyake vya shetani ambavyo havijaidhinishwa kuna uwezekano mkubwa kukasababisha mkanganyiko na dhana fulani na kutengeneza fikra mbaya kati ya bidhaa ya kampuni ya MSCHF na kampuni ya Nike," Kampuni hiyo ya utengenezaji viatu vya michezo imesema katika kesi yake iliyowasilisha.

"Kwanza, tayari kuna ushahidi wa kutosha unaoonesha mkanganyiko na dhana potofu sokoni, ikiwemo simu zinazotaka watu kususia bidhaa za kampuni ya Nike kufuatia uzinduzi wa viatu vya shetani vya kampuni ya MSCHF, ambavyo inaonekana kana kwamba kampuni ya Nike ndiyo ambayo imeidhinisha na kuruhusu utengenezaji wa bidhaa za hiyo."

Kesi iliyowasilishwa inarejelea ujumbe wa mtandao wa Twitter uliotumwa na mshawishi mkubwa wa viatu saint Ijumaa iliyopita, ambao ulianza kuarifu wateja wake kuhusu kuzinduliwa kwa viatu hivyo na kuvipa umaarufu zaidi kwa umma wikendi kwenye mtandao wa kijamii na hata vyombo vya habari vya Marekani.

Baadhi ya wenye msimamo mkali akiwemo gavana wa Dakota Kusini Kristi Noem, na wafuasi wengine wa kidini, wameshutumu viatu hivyo vyenye utata na kumkosoa rapa Lil Nas X na kamupuni ya MSCHF kwenye mtandao wa Twitter.

Hata hivyo, Lil Nas X alimjibu gavana huyo pamoja na viongozi wa kidini kwenye mtandao wa Twitter, na Jumatatu katika mtandao huo, kulikuwa na vibonzo vya mzaha kwenye wasifu wake baada ya kampuni ya Nike kusema kwamba imechukua hatua ya kisheria.

Screenshot_20210330-120010_Facebook.jpg
Screenshot_20210330-115914_Facebook.jpg
 
Nimeangalia hiyo video huyu jamaa sijui limeshakua shoga maan ile kumkatikia shetani ni noma, alafu mavideo yake sikuhizi lazima yahusishe alama za mpinga kristo
 
Back
Top Bottom