Je unampenda mama yako???

CharmingLady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
18,304
Reaction score
12,999
Soma kisa hiki kisha utajibu kama unampenda mama yako au la!

Siku moja dada fulani alianza kumwambia mama yake,

"Mama mie sikupendi, uso umekunjamana, sura yako mbaya, wewe sio mzuri kama wamama wa rafiki zangu. Mikono yako ina makovu. Hakika sikupendi hata kidogo. Ninakuchukia sana"

Yule mama alilia kwa uchungu sana kisha akamwambia,

"Mwanangu, baba yako alifariki wakati ukiwa mdogo sana. Alituacha tukiwa tunaishi kwenye kijumba cha nyasi nje kabisa ya mji, tulikuwa fukara sana. Siku moja niliondoka na kukuacha ndani ukiwa umelala nikaenda shamba jirani na kijumba tulichokuwa tunaishi. Ghafla nilisikia watu wakipiga yowe MOTOOO MOTOOO..... Nikarudi ili nitizame wapi kunawaka moto. Ndipo nikaona ni kijumba chetu ndicho kinawaka moto ilhali wewe ukiwa ndani yake umelala.

Nilipofik wanakijiji walinizuia nisiingie ndani kwani moto ulikuwa mkubwa, lakini nilipambana nao nikafanikiwa kuingia na kukuta moto haujafika mahali ulipolala. Nilikuchukua nikakukumbatia vyema ili moto usikupate. Nilifanikiwa kutoka ndani bila mwale wowote wa moto kukupata wewe.

Na haya majeraha uyaonayo niliungua na moto ili wewe upone"

Alipomaliza kumsimulia ile habari, yule dada alilia saaaanaaaa na kumuomba mama yake msamaha na tangu siku hiyo alimpenda mama yake....

Hebu turudi katika maisha yetu, kuna watu wanaowachukia wazazi wao kwa sababu mbalimbali.... Ni kweli wakati mwingine wanakosea kwani hata wao ni binadamu, ila hatuna budi kuwasamehe kwa wamepitia mengi ili kutufikisha hapa tulipo.

Wazazi wetu wengine waliteseka wakati wa ujauzito lakini hawakukata tamaa, wengine walifukuzwa na wazazi wao lakini walivumilia mateso hayo na kutuzaa, wengine walitelekezwa na baba zetu lakini hawakuthubutu kutuua, Wengine hata kupata ulemavu kwa ajili yetu... Na mengine meeengi sana.

HEBU TUWAPENDE MAMA ZETU KULIKO KITU CHOCHOTE.... MAKE KUNA WANAOTAMANI KUWAONA MAMA ZAO LAKINI WALISHALALA MAUTI NA HATA WENGINE HAWAKUWAHI KUWAONA. LAKINI MIMI NA WEWE TUNAWACHUKIA..

TUBADILIKE WAPENDWA
 
Dah Kwa kweli Mama ni Mama tu,Mpaka leo nakumbuka neno la mwisho la Mama kuniambia Rafiki yangu naumwa hiyo ilikuwa ni kipindi yupo hospital nami nilikuwa shule ubungo islamic nilipata ruksa ya kwenda kumwona.na ndio ilikuwa kauli ya mwisho ya mpendwa Mama yetu hakika Mama alikwenda ingali ajapata hata kufaidi cha wanae,Mama ulikuwa Msuluhisho ndani ya ukoo wetu.Mama endelea kupumzika kwa Amani hakika bado upo ndani ya nafsi za watoto wote,Dua zetu zitaendelea mpaka pale tutakapokufata Pumzika Mama,Tulikupenda.Kwahiyo anaemchukia Mama yake kwa lolote Plz badilika.
 
Pole sana mkuu kwa kuondokewa na mama yako kipenzi... Najua huzuni uipatayo mara tu unapomkumbuka mama yako hakuna mtu anayeweza kuidefine... Lakini cha ajabu kuna watu wanathubutu kusema wanawachukia mama zao... Dah inauma sana!
 
Mama ndo kila kitu. Nampenda mama yangu ma-kokutola
 
charminglady asante kwa uzi huu
Mama ni mama tuu na nampenda sana mama yangu maana najua masahibu aliyoyapata mpaka kufanya mimi nifike hapa
Asante sana
 
Last edited by a moderator:
Pole sana mkuu kwa kuondokewa na mama yako kipenzi... Najua huzuni uipatayo mara tu unapomkumbuka mama yako hakuna mtu anayeweza kuidefine... Lakini cha ajabu kuna watu wanathubutu kusema wanawachukia mama zao... Dah inauma sana!

Asante sana ni kweli uwa inauma sana ila inabidi tu ukubali na hali halisi Asante sana
 
mama ni mama tu hata mtu aende wapi mtoto wangu wa miaka minne anaweza kukuambia hilo. haongei vizuri sana alichelewa kuanza kuongea. nilimnyanganya kitabu alikuwa anachana akaniambia 'mama mimi sio rafiki yangu tena" na akawa amekasirika sana. lakini after a short while alirudi akasema "mama nakupenda".
 
Anayemchukia mama yake namfananisha na mavi i.e hajui atokako na pia ana dark future.
 

Kitu cha kwanzaunachotakiwa kukipenda kuliko chochote ni MUNGU! prove me wrong! lakini mpendwa katika mfano wako mzuri ndivyo YESU alivyofanya msalabani, alipigwa, alichubuliwa, alitukana, alitemewa mate, alidharauliwa hadi kuuwawa taja nini tena, kwa ajili yetu sote wanadamu mm na ww Charminglady! nitashangaa kweli kama umetoa mfano huu na hujampokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yako na mbingu pia zitashangaa! maana Yesu alifanya zaidi ya huyo mama maana yeye hata hakufa ila Yesu alikufa kwa ajili yetu ss wote members wa JF na wengine wote.
 
Pole sana mkuu kwa kuondokewa na mama yako kipenzi... Najua huzuni uipatayo mara tu unapomkumbuka mama yako hakuna mtu anayeweza kuidefine... Lakini cha ajabu kuna watu wanathubutu kusema wanawachukia mama zao... Dah inauma sana!

kila mtu na mawazo yake juu yaliyomkuta kwa mama yake je yule alietupwa na mamaye chooni akaokolewa na wasamalia huyo je atamchukuliaje sasa mama yake..
 
Tz hatuna haki za watoto kabisa

wakubwa wanajifikiria wao tu ndio wenye haki, mizazi mingine ni

mishenzi sana haifai hata kidogo
 
''Waheshimu baba na mama yako upate miaka mingi na heri duniani''
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…