Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,372
Huyu aliwahi kuwa waziri mkuu wa Israel kati ya mwaka 2001 na 2006 kabla ya kulazimika kuondolewa madarakani baada ya kuugua kiharusi(stroke) mwezi March mwaka 2006.
Kwa kifupi, huyu bwana alipendwa sana na wayahudi mpaka wakampa hayo majina lakini alichukiwa sana na waarabu hasa kwa jinsi alivyokuwa akiwatendea wapalestina.
Huyu bwana mwaka 1982 wakati huo akiwa Waziri wa Ulinzi wa Israel, alifumbia macho mauji ya wakimbizi wa kipalestina huko Lebanoni ambapo wapalestina kati ya 800 mpaka 1200 waliuwawa na Wakiristo huku majeshi ya Israel yakitazama tu.
Hata hivyo, sijui ndio nguvu ya karma, kwani bwana huyu alikuja kuugua kiharusi na kusababisha awe kwenye "coma"kwa kipindi cha miaka 8 kuanzia January 2006 mpaka January 11, 2014 alipooaga dunia.
Kwa vyovyote vile itakavyotasiriwa,watawala dunia kote wana somo la kujifunza hapa kuwa hata wao wanaweza kupata mateso kama binadamu wengine waliowaumiza katika tawala zao na pengine kupata tabu na mateso makali zaidi ya yale waliyoyasabisha kwa binadamu wenzao.
Ni habari ya kusikitisha, kuhuzunisha na kuumiza sana ila bado tunapaswa kuitafakari kwa mapana yake maana huenda kuna somo kwa sisi ambao bado tuko hai hasa kwa wenzetu wenye madaraka katika hii dunia.