SIREN
Member
- Sep 5, 2013
- 80
- 46
Je, ulishawahi kujiuliza siku ukifa historia yako itasomwaje? Ukisoma kitabu cha Matendo ya Mitume 9:39 Biblia inasema “Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani, wajane wote walisimama karibu naye, wakilia na kumuonesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao. Hii ni habari ya mwanamke aliyeitwa Dorkasi ambaye alikuwa mwadilifu na alitenda mema kwa jamii yake kiasi kwamba hata alipokufa watu walihuzunika sana na hawakutaka kuamini kuwa ndio wamempoteza, hivyo wakaamua kumfuata Petro aliyekuwa akitoa huduma mji wa jirani na maeneo yao. Lengo la kumuita Petro ilikuwa ni kuja kumwombea mpendwa wao. Ni wazi kuwa waliona wazi pengo la kumpoteza mpendwa wao. Hata Petro alipofika, waombolezaji walimuonesha Petro kazi za mpendwa wao alizozifanya akiwa hai. Jiulize wewe watu wataonesha nini siku ukifa? Watahuzunika kwa lipi siku umauti ukikukuta? Au siku hiyo ndugu na jamaa watalia kinafiki huku moyoni wakifurahia kuwa “afadhali amekufa maana alipokuwa hai alitusumbua kwa vurugu zake, tulichoka na matusi yake, tulichoshwa na umbea wake, n.k.” Hakikisha unaandika historia yako vizuri ili siku itakaposomwa iwe nzuri na iwavutie watu na kumtukuza Mungu kwaajili ya huduma iliyokuwa ndani yako. Wewe ndiyo mwandishi wa historia yako siku ya mazishi huwa ni kusomwa tu kwa kile kilichoandikwa na wewe enzi za uhai wako. Omba hekima ya KiMungu ili uweze kuandika historia iliyo nzuri kwa utukufu wa Mungu.