Je, unafahamu Uhuru wa Mahakama unamaanisha nini?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
1607685399607.png

Uhuru wa Mahakama unamaanisha kuwa kila jaji au hakimu yuko huru kuamua kesi iliyopo mbele yake kwa mujibu wa sheria na ushahidi ulioletwa mbele yake, na katika kutekeleza
majukumu hayo, hapaswi kuingiliwa, kushawishiwa, au kushinikizwa na mtu au chombo chochote, ikiwemo Bunge na Serikali kama inavyoelezwa katika Ibara ya 107B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Hivyo, dhana ya uhuru wa mahakama inaitaka mahakama kutekeleza majukumu yake bila woga wala upendeleo. Uhuru wa mahakama unahifadhiwa na kulindwa katika maeneo
manne ambayo ni:

i) Kuzuia kuondolewa kwa Jaji au Hakimu katika ofisi bila ya sababu za msingi na bila ya kufuata taratibu zilizowekwa hata kama kuna sababu za kumuondoa,
ii) Kuweka kinga ya kutoshtakiwa kwa Jaji au Hakimu kwa makosa yoyote, yawe ya jinai au madai kutokana na maamuzi yake ya kimahakama aliyoyafanya,
iii) Kutopunguza au kuondoa mishahara na maslahi ya Jaji au Hakimu, na
iv) Kutokuwa na vyeo kwenye vyombo vingine vya dola au kushiriki katika shughuli za vyama vya siasa. Hata hivyo, ni vema ikafahamika kwamba uhuru wa mahakama sio kibali kwa jaji au hakimu kuamua kesi kwa namna anavyojisikia yeye au kwa matakwa yake.
 
Huwezi kumzuia jaji au hakimu kuamua kesi atakavyo huku anajua kuwa ana kinga ya kutoshtakiwa kwa jinai au madai kutokana na maamuzi yake.
 
Sasa ikawaje mtuhumiwa akatolewa usiku gerezani, hadi hakimu kashangaa katoka kwa amri ya nani?
Kuku kadonoa punje ya mchele kabla haijaimeza mtuhumiwa kala kiapo
Naomba ufafanuzi huo uhuru wa mahakama kwenye hiyo kesi.
 
Uhuru wa Mahakama unamaanisha kuwa kila jaji au hakimu yuko huru kuamua kesi iliyopo mbele yake kwa mujibu wa sheria na ushahidi ulioletwa mbele yake, na katika kutekeleza
majukumu hayo, hapaswi kuingiliwa, kushawishiwa, au kushinikizwa na mtu au chombo chochote, ikiwemo Bunge na Serikali kama inavyoelezwa katika Ibara ya 107B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Hivyo, dhana ya uhuru wa mahakama inaitaka mahakama kutekeleza majukumu yake bila woga wala upendeleo. Uhuru wa mahakama unahifadhiwa na kulindwa katika maeneo
manne ambayo ni:

i) Kuzuia kuondolewa kwa Jaji au Hakimu katika ofisi bila ya sababu za msingi na bila ya kufuata taratibu zilizowekwa hata kama kuna sababu za kumuondoa,
ii) Kuweka kinga ya kutoshtakiwa kwa Jaji au Hakimu kwa makosa yoyote, yawe ya jinai au madai kutokana na maamuzi yake ya kimahakama aliyoyafanya,
iii) Kutopunguza au kuondoa mishahara na maslahi ya Jaji au Hakimu, na
iv) Kutokuwa na vyeo kwenye vyombo vingine vya dola au kushiriki katika shughuli za vyama vya siasa. Hata hivyo, ni vema ikafahamika kwamba uhuru wa mahakama sio kibali kwa jaji au hakimu kuamua kesi kwa namna anavyojisikia yeye au kwa matakwa yake.
hayo ni ya mabeberu kwa Tanzania raisi ndo kila kitu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom