Wont be the same
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,564
- 2,483
Unafahamu sio nchi zote husherekea Sikukuu ya Krismasi Desemba 25?
Wakristo wengi wa Madhehebu ya 'Orthodox' nchini Urusi, Ulaya ya Mashariki pamoja na nchi zilizopo Mashariki ya Kati husherehekea Krismasi siku ya Januari 7, ambayo kwa Kalenda ya Julian ni sawa na Desemba 25. Huku Kanisa la Kitume la Armenia wao husherehekea Krismasi Januari 6.
Aidha, Nchini Mexico, shamrashamra za Krismasi huanza Desemba 16 ikiwa ni sherehe ya siku tisa inayoenzi safari ya Maria na Yosefu kutoka Nazareti hadi Bethlehemu kabla ya kuzaliwa kwa Yesu.
Pia, Nchini Hispania, msimu wa Krismasi huanza Desemba 8 kupitia maadhimisho ya wiki moja ya Sikukuu ya Mkingiwa Dhambi ya Bikira Maria 'Immaculate Conception'.