kuna mdada yupo mahakama ya Usambara yule ni secretary hajielewi,amekua akinyanyasa watu wanaokuja hapo mahakamani aliwahi kumfanya mama yangu akalia kwa kuandaa mazingira ya rushwa na uzuri hata wafanyakazi wenzie wanamjua
Ana mdomo mchafu na kauli mbovu sana aliwahi kumjibu mama yangu hivi nilivyovaa unaona nafanania na kwenda kukutafutia file lako kwenye mavumbi?
Siku nyingine alimjibu file lako halionekani rudi nyumbani kalale, akaja mjibu tena ukiambiwa uje tarehe fulani unakuja kuchelewa sasa tarehe yako imerushwa njoo siku utakayojisikia mwenyewe kuja na anaanda mazingira ya rushwa ilibidi nivae njuga mimi nikaenda kuonana na hakimu ndio tena sikukutana na huyo dada face to face nilielekezwa tu nipande juu kwa hakimu nikapanda nikiwa na mama nikamweleza hakimu.
Sasa nilisema hili sakata la mama likimalizika nirudi kwa huyu dada hawezi mliza mama yangu mimi nipo hai na hata hakuna la maana ni kijihela kilichoingia kwenye akaunti ya mzee ni ya Saccoss fulani baada ya kufariki kwenye kufatilia tumeambiwa tupitie huko kwanza