Je Umewahi kudaiwa?

Smarter

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
527
110
Je Umewahi kudaiwa?, ukapata Machungu na ukakosa Amani? Mahusiano na Mdeni yakaharibika?, Je alipokuwa anakudai na wewe huna cha kulipa ulikuwa ukijibu nini?

Kama huto jali share experience yako please.
 
Mmh sijawahi.

Ila kuna watu nawadai embu ngoja niwatafute.
Ahsante kwa kunikumbusha.
 
nishadaiwaga canteen ya shule nikiwa form two,nilikaa mwezi mzima bila kukanyaga hapo na nilihama njia.
 
Dah?
Mimi ni bingwa wa kupiga sound kama nadaiwa, huwa najitahidi sana kuchagua watu wa kuwakopa.
Na huwa najitahidi kumkumbusha mdeni kuwa I'm concerned na deni lake, hata kama sina uwezo wa kumlipa for the time being...
Ila all in all,
"...dawa ya deni kulipa!"
 
Kusema ukweli dawa ya deni ni kulipa. Lakini kuna wakati mtu unakosa hata cha kulipa, na kama deni ni kubwa au mdai ni mkorofi hapo kasheshe.

Kikubwa cha kufanya ni kumsihi na mara kwa mara kufanya naye mawasiliano ili aone kuwa unamjali, kwani kukaa kimya inampa mashaka mdai.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
nishadaiwaga canteen ya shule nikiwa form two,nilikaa mwezi mzima bila kukanyaga hapo na nilihama njia.

Sasa hapo shule ukihama njia, je, siku ungelikutana na huyo mdai uso kwa uso katika mlango wa kuingia Toilet, wewe unaingia na yeye anatoka, Je, ungeghairi NIA ya kwenda Toilet na kukimbia au...........

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!
 
Nikiwa nadaiwa huwa najitahidi kulipa pindi tu nipatapo cha kulipia deni, lakini kwa watu ninaowadai huwa sina taimu ya kuwakumbusha hata kama deni limedumu kwa miezi mingapi.
 
Tatizo kudaiwa ni kawaida na Saa nyingine ni kipimo cha kujua Kama unaaminika na kukopesheka...
Ila hapa tatizo liko baadhi ya wadai huwa ni wageni wa kudai na anahisi lazima alipwe kwa wakati kumbe Saa nyingine mtu hali inakua mbaya hapo ndio kazi inakua kubwa,

Wadai wengine ni wale wa kutaka jamii yote ijue unadaiwa nalo hili ni tatizo
Kingine ni kua hakuna mtu asie na madeni na hupaswi kuogopa kudaiwa na pia Kama si lazima Ukope sio kitu cha kikimbilia...

Ila nchi za wenzetu kukopa ni sehemu ya maisha kutegemeana na Uwezo wako wa kulipa, na kuna viwango mfano... Nchi nyingi wanaanzia kukopa hata simu , furnitures na mpaka Magari watu wanakopeshwa ....
Kwahiyo kukopa sio tatizo ni mfumo tu ukiwa nzuri na dawa ya deni ni kulipa tu Kama wengi wasemavyo.
 
naogopa sana kudaiwa nakosa amani, haswa nikijua nitakutana na anaenidai...so nakereka mpaka mwisho wa siku nalipa tu...
maana hata ukiona simu yake na yamkini anataka tu kukujulia hali, au kuna jambo tofauti anataka kukuuliza, basi ww unaiangalia tu simu hutaki kupokea, kumbe wala mdau hana tym...
waweza pata ugonjwa wa moyo mkuu, kama ipo unalipa, kama huna sasa inabidi ufanye mbinu...
uhamishe deni, unamkopa mwingine unalipa mwingine...ha ha!!
 
Acha kabisa kitu kudaiwa maana unajiona kama vile uko uchi. Kwanza usiombe ukadaiwa na mchaga utaipata ya jiji
 
Je Umewahi kudaiwa?, ukapata Machungu na ukakosa Amani? Mahusiano na Mdeni yakaharibika?, Je alipokuwa anakudai na wewe huna cha kulipa ulikuwa ukijibu nini?

Kama huto jali share experience yako please.
Nishawahi kudaiwa sana tu........ an kwa hahkika anayeogopa madeni mara nyingi huwa anaishi maisha asiyoyatarajia........ KWANGU KAMA NADAIWA NA NIMEAHIDI KUWA NALIPA SIKU FULANI, KAMA NAONA UWEZEKANO WA KULIPA SIKU HIYO NI MDOGO.... HUWA NAMTAFUTA ANAYENIDAI KABLA YA SIKU YA AHADI NA KUTOA MAELEZO YALIYONYOOKA JUU YA KUSHINDWA KWANGU KULIPA SIKU YA AHADI............ Tatizo la walio wengi ni kutotoa taarifa ya kushindwa kulipa siku ya ahadi mapema au kabla ya siku hiyo.
 
Mimi nina madeni kibao hapa nilipo na maisha yanaendelea lakini sijakopa kwa watu binafsi! nimekopa kwenye taasisi hahaha:lol:

Ila kwa wale washikaji ninaowadai yaani hata kunitafuta hawanitafuti tena na urafiki na mimi baasi! nadhani wanaomba hata nife leo ili wasirudishe pesa zangu hahahaha kweli ukiwa na watu wako wa karibu usiwakopeshe pesa utaharibu undugu na urafiki. Kipindi ukiwa single unamake decisions on ur own kibaya sana coz washikaji wanakurupuka tu unawapa pesa unajikuta miaka 3 ishapita shilingi imeshuka thamani na hela yako haijarudi na huna uhakika kama itarudi na hata ikirudi itarudi ile ile inakula kwako.

Ndugu ukimkopesha ndio kabisa anaona ana haki ya kuuchuna. Mwengine huyu nampigia simu simpati anabadilisha namba , unampigia waifu wake ambaye ndio ndugu yangu wa damu eti ananidanganya jamaa kasafiri hehehehe wakati watu wanamuona town.
 
Aisee, nina madeni sana
na wala siogopi, hata makampuni makubwa yana madeni.
 
Jamani msiombe kudaiwa kodi ya nyumba na mama wa kimanyema... Kudadeki huli samaki wala mayai ukatupa maganda au miba nje. Anazoa kuja kukuonyesha kua unajaza choo wakayi hela ua kulipa unayo
 
Hii Thread ni mtambuka, sidhani kama kuna ambae amekua mtu mzima akawa hajawahi kudaiwa.
Mimi niliwahi kukopwa M. 2 na mjomba wangu alinitumia through M-Pesa ambapo period ilikua 1 month ilipofika due date mi vyanzo vyote vimegoma!
Kilichofata uncle akawa ananipigia kama hana akili nzuri, nikafikia ku'off my two lines.
Nikawa natumia Zantel No ambayo haikuijui.
Mara chache nilikua nafungua kwa kuvizia lines zangu nikawa nakutana na msg za mistari ya Nyimbo ya bongo Fleva "NILIPE NISEPE"
Kitu ambacho kilinishangaza kwani mjomba ni mtu mwenye umri mkubwa over 65 sijui aliwezaje kuijua mistari ya nyimbo hii.
Aidha nilimlipa miezi mitatu baada muda wa ahadi kupita, hata hivyo deni hili limeniachia athari hadi leo ile "receive call tone" niliokua nikitumia wakati nadaiwa na huu mwimbo wa "Nilipe nisepe" ni sound ambazo nafsi yangu imevichukia hadi leo.
 
KUNAA JAMAA ALIKUWA ANANIDAI...OYA VIPI CHANGU,NIKA MWAMBIA MWANA AKIJA SANUKAA NIKOPE ELFU HAMSINI TENA IWEE LAKI TATU,NIFUKUZIE DILI FLANI THEN NA KUJAA KUKUPA YOTE.jamaa akasema hana nikamwambiaa skopaa vumilia kidogo master...
 
Back
Top Bottom