Je umemuona kijana huyu

Status
Not open for further replies.
MNDEE Sheria za kutangaza mtu aliepotea tena ukiambatanisha na picha zinakutaka kuweka na Taarifa ya polisi yaani RB.

Hapo nyuma iliwahi tokea kesi ya mtu kumdhalilisha rafiki yake kwenye TV kwa kumtangaza kapotea na ana matatizo ya akili.

Bila shaka hata uko kwenye VITUO vya TV waliwagomea kutoa tangazo bila RB.

Fanya hima utuwekee na hiyo RB hapa ili kutilia uzito wa kisheria bandiko lako mkuu!

Hii ndio XXXX
 
Mtoto kukutana na watoto wenzie pia ni sehemu ya kujifunza socialisation. Akiwa na private teacher hatajifunza kuishi na watu na itamuondoa confidence. Mbona wanaweza kuishi normal life? Except sio alazimishiwe kusoma hadi chuo kikuu. Akishajua kusoma na kuandika anaangaliwa hobby yake tu anasaidiwa kuanzisha project.
Huyo mdogo wenu academy anafuata nini? Mtafutieni private ticha home?
 
Wanajamii ahsanteni kwa ushauri, maoni na tips mlizotoa. Tunaendelea kufanyia kai, kikubwa sana tunahitaji sasa ni watu wa kjitolea kusaidia kwenye msako, kuweka matangazo na jinsi nyingine yoyote itakayosaidia kumpata kijana wetu. We are on our own hakuna branch yoyote ya serikali inasaidia katika hili,inabidi tujiorganize wenyewe na kutegemea watu kama nyie kusaidia. Tunatanguliza shukrani kwa yeyote atakayejitolea. Kama ungependa kusaidia kuungana na wanandugu wasiliana nasi kupitia xxx-xxxx-xxx.
 
Tunatanguliza shukrani kwa yeyote atakayeweza kutusaidia kwa aina yeyote iwe kushare hii taarifa, kugawa picha au hat kusaidia kuulizia misikitini, makanisani na shuleni. Tunaamini watu wengi wakifahamu hili itasaidia sana. Ahsante.
Mkuu tuko pamoja, hata hivyo kama ikitokea amepatikana basi tufahamishane hapa hapa ili zoezi lisimamishwe. Thanks.
 
Mkuu, tunajitahidi kutoa update as we go, hapalaliki ndugu yangu, niliko sasa hivi ni saa tisa na nusu usiku niko macho na sitegemei kulala, it has been this way since kijana amepotea. Believe me you will be the first to know kama utakuwa unacheki hii post.
 
tupo pamoja kumsaka huyo kijana na nime-note tatizo lake linafanana na la mdogo wangu ana miaka 10 anasoma academy lakini hawezi kuandika hata jina lake

Tumejifunza mengi baada ya kupatwa na haya matatizo, kwamba kuna 'GPS locator and tracking systems' za watoto au watu wenye autisim ambazo zinasaidia kukualert kama atakwenda umbali usiotakiwa au kusaidia kumpata akienda mbali. Tuwasiliane tuone cha kufanya. Pia tutajitahidi kadri Mungu atakavyotusaidia kuleta awareness na kusaidia pale tutakapoweza.
 
Poleni sana na msikate tamaa kumtafuta. Mungu atakuwa nanyi katika kumtafuta. Huu utaratibu wa polisi kutoa RB baada ya kupewa taarifa na kusema tatizo litashughulikiwa baada ya masaa 24 kupita haufai kwa dunia ya sasa! Nini maana ya kusema ni jeshi linalolinda watu na mali zao? Uongo mtupu!
 
Mngejaribu kwenda hospitali za karibu kama mwananyamala na muhimbili.. Iliwahi kutukuta tukatafuta mtu siku nzima kumbe yupo moi hajitambui.. Ila naamini atakuwa salama.
 
Mngejaribu kwenda hospitali za karibu kama mwananyamala na muhimbili.. Iliwahi kutukuta tukatafuta mtu siku nzima kumbe yupo moi hajitambui.. Ila naamini atakuwa salama.

Tumepita huko kote Mkuu.
 
Poleni sana na msikate tamaa kumtafuta. Mungu atakuwa nanyi katika kumtafuta. Huu utaratibu wa polisi kutoa RB baada ya kupewa taarifa na kusema tatizo litashughulikiwa baada ya masaa 24 kupita haufai kwa dunia ya sasa! Nini maana ya kusema ni jeshi linalolinda watu na mali zao? Uongo mtupu!

Hiyo RB inatolewa baada ya masaa 24 kupita. Kibaya zaidi haijalishi mtu anaspecial needs, kipofu, kiziwi, bubu au la - wote wanawekwa kundi moja na watu normal . Baada ya hayo masaa 24 unategemea kuna resource zozote wanatoa hakuna, tumeshangaa hayo masaa 24 walikuwa wanangoja nini - kutoa kipande cha karatasi? Tulitegemea serikali inatoa msaada zaidi ya kipande cha karatasi kwa walipa kodi wake.
 
Poleni, nimeona tangazo lake la kupotea kwenye gazeti la Guardian la leo. Hope mtapata details zake soon maana ni gazeti linalosomwa na wengi. All the best nawaombea mumuone akiwa salama.
 
Poleni, nimeona tangazo lake la kupotea kwenye gazeti la Guardian la leo. Hope mtapata details zake soon maana ni gazeti linalosomwa na wengi. All the best nawaombea mumuone akiwa salama.

Tunajaribu pia kuweka magazeti ambayo yanasomwa na wananchi wa kawaida - tunahitaji kulenga vijana wa vijiweni, wanafunzi, makondo, mama ntilie, wauza mitumba, wafanyabiashara wanaotembeza bidhaa kwa miguu na wengine katika hili kundi. Tunaamini juhudi hizi zitazaa matunda, na pia tuko kwenye maombi.
 
Hiyo RB inatolewa baada ya masaa 24 kupita. Kibaya zaidi haijalishi mtu anaspecial needs, kipofu, kiziwi, bubu au la - wote wanawekwa kundi moja na watu normal . Baada ya hayo masaa 24 unategemea kuna resource zozote wanatoa hakuna, tumeshangaa hayo masaa 24 walikuwa wanangoja nini - kutoa kipande cha karatasi? Tulitegemea serikali inatoa msaada zaidi ya kipande cha karatasi kwa walipa kodi wake.

Mtakuwa na bahati sana kama hamkuambiwa karatasi zimeisha,ili mtoe pesa za kwenda kununulia wakati karatasi wanazo na pesa inayotolewa kuwekwa kibindoni!
 
Wanajamii Bwana asifiwe kijana wetu amepatikana yuko hospitali hii taarifa nimeipata sasa hivi, sina details zaidi.
 
Wanajamii, naona niwapatie details zaidi muelewe kilichotokea napengine itakuja saidia mtu mwingine.

Kijana alipatikana hivi - mama mmoja msamalia mwema jana alikwenda hospitali ya Amana kumjulia hali mgonjwa , akiwa pale akasikia manesi wanamuongelea mgonjwa mmoja kuwa atapelekwa jela ya watoto kesho ( leo Jumamosi) kama ndugu zake hawatamchukua. Alipomuona kijana anayeongelewa akakumbuka aliwahi muona Kijitonyama. To cut the long story short yule mama akampiga picha kijana, akaanza safari ya kusaka wazazi wake nyumba hadi nyumba akionyesha picha kila alikopita hatimae akafika nyumbani kwa sister.

Unofficial report kijana alifikishwa pale na polisi siku aliyopotea, ana majeraha kichwani na miguuni assumption atakuwa alipigwa. Amana ni moja ya hospitali ndugu walipita zaidi ya mara moja kumtafuta, kila walipokwenda waligomewa kuingia wodini na kuishiwa kuambiwa kijana hayupo pale.

Baba kijana alirudi mara nyingi kituo cha polisi alichoripoti kupotea kwa kijana wake kuona kama kuna aliyeripoti kitu. Kila alipofika kituoni ilibidi aanze story upya. Hii ina maanisha nini – unapotoa ripoti polisi wakiandika ile ripoti chances are inaishia kwenye droo, hivyo wanapobadilishana shift hiyo ripoti yako si sehemu ya makabidhiano. Hivyo atakapokuja mtu kutoa taarifa itakayokusaidia haitakufikia.

What to take from this - juhudi binafsi na kujitoa kwa raia vinahitajika katika masuala ya jamii na matukio ya namna hii. The system is broken, branch za serikali haziko connected. Most probably ukiripoti kitu au kufuatilia kitu kwenye branch ya serikali mfano ukiambiwa jaza form, or ngojea ‘RB' masaa 24 ni fomality tu. Pia persistence inahitajika sana, usikate tamaa na uwe na imani na Mungu wako.


Ahsanteni sana kwa maombi na kwa kutia moyo.
Mndee
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom