Je umemuona kijana huyu

Status
Not open for further replies.
Mkuu kuna mtu ameshauri kuwa mjaribu kwenye kutangaza redioni.
Nadhani inaweza kusaidia kuharakisha kupatikana kwa ndugu yetu.
Sidhani kama gharama zitakua kubwa sana.
Pia nina imani wanaweza kusaidia kutangaza hata bure maana nao ni binadamu sio kila kitu watataka pesa.

Matangazo yameshapelekwa kwenye vyombo vya habari, TV na redio. Ahsante.
 
Update 6:31CST - bado hatujafanikiwa kumpata kijana wetu. Tunaomba muendelee kumuweka kwenye maombi, kushare hii taarifa kwa familia, majirani na ndugu. Kwa wale wanaotumia usafiri wa mabasi tutashukuru sana kama mtawaeleza madereva au makonda. Ahsanten, Mndee.
 
Poleni sana. Kwa uwezo wa Mungu kijana atapatikana, msikate tamaa kumtafuta
 
So you know- baada ya yale masaa 24 polisi waliyodai tungojee tulirudi tena polisi, tulishangazwa kuona tunapewa kitu inaitwa RB na kuambiwa sasa tunaweza kwenda tangaza popote. Swali je tulichokuwa tunangojeshwa masaa 24 ni hiki kipande cha karatasi? Nini tena kingine polisi wanafanya hakuna. Huwezi elewa nini matatizo yaliyoko kwenye system mpaka kitu kama hiki kitokee kwenye familia yako au mtu wa karibu.

Mbali na matangazo wanafamilia wanapita sehemu mbali mbali kumsaka kijana. Dar ni kubwa na resource tulizonazo in terms ya watu kufanya msako ni ndogo. Kama uko tayari kutusaidi kwenye msako kwa kuorganize watu sehemu ulipo tutashukuru sana. Njia nyingine ya kusaidia ni kuprint picha na kugawa mfano mashuleni, viwanja vya mipira, vituo vya mabasi au masokoni.

Sehemu tulizofocus kutokana na leads tulizopata ni Tandale, Sinza, Mazense, Ubungo, Mwenge na maeneo mengine kuzunguka. Inawezekana amekwenda mbali na sehemu hizi. Leads zimekomea uwanja mmoja wa mpira Tandale, vijana waliokuwa mpirani hapo walimuacha wakati wanaondoka saa moja usiku juzi, baada ya hapo hatujapata mtu ambaye amemuona tena. Tumeendelea kurudi hapo kwa imanii kuwa atapatikana mtu ambaye alimuona. Ahsanteni.
 
Kama ugependa kujiunga nasi kwenye msako wewe peke yako au na kikundi chako unaweza kupm.
 
Webmaster naomba msaada uniwekee link ya hili tangazo home page.
 
Mungu ni mwema na mwaminifu amemlinda na kumtunza kwa Mkono wake uliohodari kwa JINA LA YESU ALIYE HAI.
 
Kwa kuwa ss wote ni ndugu nafeel kama ingekuwa mm ngoja ni-print hii picha niwape vijana wangu wawe nayo njiani nadhani tunaweza kusaidiana katika hili. Usihofu Mungu ndiye tumaini letu la kwanza.
 
Nimewaza mambo milioni. Poleni sana. Mungu amtunze na kuwashangaza kwa kumpata salama. Kila la kheri.

Mmewasiliana na ndugu zenu walio nje ya dsm? Anaweza kuwa alipanda basi pia.
 
tupo pamoja kumsaka huyo kijana na nime-note tatizo lake linafanana na la mdogo wangu ana miaka 10 anasoma academy lakini hawezi kuandika hata jina lake
 
tupo pamoja kumsaka huyo kijana na nime-note tatizo lake linafanana na la mdogo wangu ana miaka 10 anasoma academy lakini hawezi kuandika hata jina lake

Huyo mdogo wenu academy anafuata nini? Mtafutieni private ticha home?
 
Kwa kuwa ss wote ni ndugu nafeel kama ingekuwa mm ngoja ni-print hii picha niwape vijana wangu wawe nayo njiani nadhani tunaweza kusaidiana katika hili. Usihofu Mungu ndiye tumaini letu la kwanza.

Tunatanguliza shukrani kwa yeyote atakayeweza kutusaidia kwa aina yeyote iwe kushare hii taarifa, kugawa picha au hat kusaidia kuulizia misikitini, makanisani na shuleni. Tunaamini watu wengi wakifahamu hili itasaidia sana. Ahsante.
 
mkuu, toa NAMBA za mitandao TTCL haitapigika unless unatania!

Wamejitokeza wahuni wanapiga simu hata usiku wa manane kutoa leads za uongo. Hii imepelekea wanafamilia kwenda vituo mbalimbli vya polisi usiku kucha na kukuta taarifa hazikuwa za kweli. Kwa vile vituo vyote vya polisi vina taarifa tunategemea atakayemuona kijana wetu atatoa taarifa huko au atampeleka kwenye hivyo vituo. Hii itatusaidia kuzitumia vyema resource chache tulizonazo katika juhudi za kumpata kijana wetu. Ahsante.
 
namba hamjatoa sasa wamezipataje? I am just saying.
 
Tunatanguliza shukrani kwa yeyote atakayeweza kutusaidia kwa aina yeyote iwe kushare hii taarifa, kugawa picha au hat kusaidia kuulizia misikitini, makanisani na shuleni. Tunaamini watu wengi wakifahamu hili itasaidia sana. Ahsante.
MNDEE Sheria za kutangaza mtu aliepotea tena ukiambatanisha na picha zinakutaka kuweka na Taarifa ya polisi yaani RB.

Hapo nyuma iliwahi tokea kesi ya mtu kumdhalilisha rafiki yake kwenye TV kwa kumtangaza kapotea na ana matatizo ya akili.

Bila shaka hata uko kwenye VITUO vya TV waliwagomea kutoa tangazo bila RB.

Fanya hima utuwekee na hiyo RB hapa ili kutilia uzito wa kisheria bandiko lako mkuu!
 
Last edited by a moderator:
namba hamjatoa sasa wamezipataje? I am just saying.

Namba zimetolewa sehemu nyingi, kama utakuwa umesoma hii post utakuwa umeona. Nimeeleza kwa nini tumefanya hivyo, hii ni baada ya ushauri kutolewa na watu wenye background na masuala haya. Wako watu wanatumia matukio kama haya si kusaidia bali kuleta madhara au kutafuta jinsi ya kunufaika binafis. Vituo vya polisi na vyombo vya habari ndio zitakuwa sehemu kubwa za kuwasilisha lead yoyote. Wenye nia ya kusaidia tayari wameshainga barabarani na wanaweka matangazo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom