Je, umefikia malengo uliyojiwekea mwaka 2019 kwa kiasi gani?

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
2,858
7,847
Hello wadau,
Tukiwa tumebakiza siku chache kuumaliza mwaka 2019, ni wakati wa kutafakari ni kwa kiasi gani tumeweza kufikia malengo tuliyojiwekea kuyafikia mwaka huu.

Kama utapenda, shiriki kwenye hii poll kwa kuchagua kati ya option 3, kama umetimiza malengo yako kwa zaidi ya asilimia 90, chagua hapo option ya kwanza, kama hujafikisha asilimia 90, ila umevuka asilimia 50, chagua option ya pili, kama ni chini ya asilimia 50, chagua option ya tatu ya bora uhai.

Mimi nimeanza kwa kuchagua option ya bora uhai, kwa sababu nimeweza kukamilisha asilimia 40 tu ya yale niliyojiwekea kuyakamilisha mwaka huu, hivyo mwaka huu nimekua mzembe sana. Nina kazi kubwa mwakani, ya kufukia mashimo ya mwaka huu, na kufikia pia malengo ya mwakani panapo majaliwa.
 
Mimi binafsi kutoka moyoni mwangu namshukuru Mungu nimeweza kuyatimiza kwa asilimia kati ya 50 na 90. Mungu ni mwema.
Naomba Mungu anipe afya njema, pia na nidhamu ya kutumia vema kipato changu halali.
 
Around 50% , Mungu mkubwa ...mambo mengi,changamoto nyingi..nimejipa mapumziko kama miez miwl hv nijipange upya kwa mwakani na kuweka malengo mapya , ku improve nilipo legea, mapambano yanaendelea
 
mwaka umekuwa mweusi sana,salary haitulii kabisa ukipokea leo wiki huna,business inakwenda kama gari bovu faida kidogo.
Mungu mkubwa amenipa afya ya kutosha pamoja na familia,kuna muda hata balance ya 10k bank sina.
 
Back
Top Bottom