Je, ulokole una nafasi gani katika mahusiano?

Je, ulokole una nafasi gani katika mahusiano?

Mkuu upo huru kuongea chochote.
Ila huo mstari kwa kiasi fulani unatetea watu fulani wasio na ndoa kufanya kile kitendo pendwa bila ndoa, ili mradi muwe mmekubaliana
not true, huo mstari unawahusu wenye ndoa na hakika umeeleza vyema ikiwa wamekubaliana, meaning hata kama mmojawapo anataka kuingia kwenye mafungo amshirikishe mwenzake na wakubaliane kwanza na si kumnyima mwenzie bila maridhiano.

Sasa kama mfungo ni wa siku 3 seriously inaweza kuleta malalamiko? let us be patient on papuchi's jamani tusilalamike kama ni chakula.
 
not true, huo mstari unawahusu wenye ndoa na hakika umeeleza vyema ikiwa wamekubaliana, meaning hata kama mmojawapo anataka kuingia kwenye mafungo amshirikishe mwenzake na wakubaliane kwanza na si kumnyima mwenzie bila maridhiano.

Sasa kama mfungo ni wa siku 3 seriously inaweza kuleta malalamiko? let us be patient on papuchi's jamani tusilalamike kama ni chakula.
Ahsante shem wangu kwa kunifafanulia
 
Kuna uncle wangu mkatoliki mke wake kaokoka. Duh! Yule mama kuanzia J5 mpaka Jumapili anashinda kanisani na kurudi nyumbani saa 3 usiku. Mume anarudi home saa 12 jioni. Hajui mumewe anakula chakula gani au kama ana mahitaji mengine. Anasali kwa 'nabii' fulani hivi. Huyo nabii anaweza piga simu anytime akiomba usafiri in case gari yake ina matatizo. Aunt yangu ndiye anakuwa dereva. And when things go wrong you start cursing the poor devil. Kweli watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
Huu ndo ulokole wa kijinga!
Yaani nikuwa amekosa maarifa!

Huwezi shinda kanisani hujui mume anakula nn,ni upumbavu na wala hatufundishwi hivyo kanisani ,huyo nabii nae anajua kabisa anakosea!
Adui ana mbinu nyingi za kuvunja ndoa za watu pamoja na hiyo!
Huo sio ulokole ujinga!

Uncle ako anatakiwa ampige makofi kwanza akili imkae sawa!
 
Kweli mkuu jambo hili nimelizungumzia juu juu. Ni mambo mengi sana hutokea kwenye ndoa hasa za walokole... Nakumbuka juzi nilisoma habari kwenye mtandao (jina nimesahau) Mama mchungaji anamlalamikia mumewe kwa kutompa haki yake kwa takribani miaka mitatu... Just imagine unaishi na mume ndani mnamaliza miaka mitatu hajakugusa si huuaji huo,jana pia huku jf nimeona dada yetu mmoja akilalamika mumewe hajishughulushi na maswala ya familia wote wakitumia kivuli cha ulokole kutokutimiza majukumu yao.
Hili ndo tatizo sasa...

Ndo maana mwisho wachungaji inabidi watoe hadi na hii huduma ya kimwili...
 
Kwahiyo unapenda ulokole mpaka kwa bed????
Nadhani ni busara kila kitu kikapewa nafasi yake...!

Wakati wa ibada watu wafanye ibada

Wakati wa faragha watu wafanye faragha...

[emoji116][emoji116][emoji116] Biblia inasema kabisa kwenye huo mstari..

1Kor 7: 5

Msinyimane......


1kor 7: 5b mkajiane tena, shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu...
 
Habari zenu wanaMMU,

Jioni ya leo ningependa tuweze kushiriki katika mada twajwa "Ulokole". Umekuwa ni mwiba kwa baadhi ya ndoa pia ulokole umeweza kuzisaidia ndoa nyingi. Mimi haswa nitazungumzia utumikaji vibaya wa ulokole katika ndoa.

Namquote Paulo katika 1Wakorintho 7:5 "Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha ya kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawaharibu kwa kutokuwa na kiasi kwenu."

Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya watu waliokoka wanautumia Ulokole kama kisingizio cha kutokutimiza majukumu yao na hii husababisha mahusiano kati yao na wenza wao kuzorota na mwisho kufikia kuvunjika huku lawama zote wakimwangushia Shetani huku wanasahau kuwa wao wenyewe ndio chanzo cha tatizo.

Hivyo nawaomba walokole wenzangu mkaupitie huo mstari kwenye bibilia kupunguza wimbi kubwa la ndoa zilizovunjika na zinazoendela kuvunjika.

Matumaini yangu kwa namna moja ama nyingine sitakuwa nimemkwanza yeyote kwa Bandiko hili.

Shukrani wakuu
Ulokole hauna faida yoyote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom